< Yeremia 13 >
1 Bwana aliniambia hivi, “Nenda ukape nguo ya kitani na kuiweka karibu na kiuno chako, lakini usiiweke kwenye maji kwanza.”
上主對我這樣說:「你去買條麻帶,束在腰間,但是不要浸在水裏。」
2 Kwa hiyo nilinunua vazi kama vile Bwana alivyoagiza, na nikafunga karibu na kiuno changu.
我就照上主的話去買了根麻帶, 。
3 Ndipo neno la Bwana likanijia mara ya pili, kusema,
上主的話第二次傳給我說:
4 “Twaa vazi lako ulilolinunua lililo karibu na kiuno chako, uinuke, ukasafiri mpaka Frati. Ukaifiche huko katika mwamba wa jabali.
「拿你買來束在腰間的帶子,起身往幼發拉的去,藏在那裏的嚴石縫裏」。
5 Basi nikaenda na kuificha katika Frati kama vile Bwana alivyoniamuru.
我照上主吩咐我的去了;將帶子藏在幼發拉的近旁。
6 Baada ya siku nyingi, Bwana akaniambia, “Simama, urudi Frati. Ukaichukue nguo ambayo nilikuambia ufiche.”
過了多日,上主對我說:「你起身往幼發拉的去,拿回我吩咐你藏在那裏的帶子」。
7 Kwa hiyo nikarudi Frati na kuchimba na kuchukua nguo mahali pale nilipoificha. Lakini tazama! Nguo hiyo ilikuwa imeharibika; haikuwa nzuri kabisa.
我便往幼發拉的去了,我由藏下的地方挖出那帶子;看,已經腐爛,毫無用處了。
8 Ndipo neno la Bwana likanijia tena, kusema,
於是有上主的話傳給我說:
9 “Bwana asema hivi, Nitakiangamiza kiburi cha Yuda na Yerusalemu.
「上主這樣說:我也要這樣毀滅猶大的驕傲,和耶路撒冷極度的高傲。
10 Watu hawa waovu wanaokataa kusikia neno langu, ambao huenda katika ugumu wa mioyo yao, ambao hufuata miungu mingine ili kuabudu na kuinama-watakuwa kama hii nguo isiyofaa kwa lolote.
這個拒絕我的話,而隨從自己固執的心行事,追隨事奉,朝拜其他神祗的邪惡人民,必要如這毫無用處的帶子木樣。
11 Kwa maana kama vile vazi lililofungwa kwenye viuno vya mtu, ndivyo nimefainya nyumba yote ya Israeli na nyumba yote ya Yuda zimefungwa kwangu- hili ndilo tamko la Bwana-wawe watu wangu, ili kunifanya jina, sifa, na heshima. Lakini hawakunisikiliza.
因為正如帶子緊貼在人的腰間,同樣我也錔使以色列全 家和猶大全家緊緊依附我──上主的斷語──成為我的人民,我的名譽,我的讚美和我的光榮;但是他們卻沒有聽從。
12 Basi uwaambie neno hili, 'Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi Kila chupa itajazwa divai.' Watakuambia, 'Je, hatujui kwamba kila chupa itajazwa divai?'
你應向他們宣佈這話:上主以色列的天主這樣說:每個壺應盛滿酒。如果他們對你說:難道我們不知道,每個壺都應盛滿酒嗎﹖
13 Basi uwaambie,' Bwana asema hivi: Tazama, nitawajaza kila mkaaji wa nchi hii ulevi, na wafalme wanaokaa kiti cha Daudi, na makuhani, na manabii, na wenyeji wote wa Yerusalemu.
你就答覆他們說:上主這樣說:看,我要使這地上的一切居民,坐在達味寶座上的君王,以及司祭和先知並耶路撒冷的一切居民,都酩酊大醉,
14 Ndipo nitawagonganisha kila mtu na mwenzake baba na watoto wao pamoja; hili ndilo tamko la Bwana-sitawahurumia au kuwa na huruma, wala sitawarehemu kutoka kwenye uharibifu.
使他們彼此衝突,連父子也彼此衝突──上主的斷語──我毫不憐憫、不慈悲、不留情地將他們消滅」。
15 Sikilizeni na makini. Msiwe na kiburi, kwa kuwa Bwana amesema.
你們側耳傾聽,不要傲慢,因為是上主在說話。
16 Mtukuze Bwana, Mungu wako, kabla ya hajaleta giza, na kabla ya kuifanya miguu yako kuwa na mashaka juu ya milima wakati wa jioni. Kwa maana unatarajia mwanga, lakini ataugeuza kuwa mahali pa giza, na kuwa giza nene.
黑暗來臨以前,在你的腳還沒有在黑暗中撞在石上以前,應將光榮歸於上主的天主;不然,你們期待光明,衪反發放死影,使它變得漆黑。
17 Kwa hiyo ikiwa husikilizi, nitaomboleza peke yangu kwa sababu ya kiburi chako. Hakika macho yangu yatalia na kutoa machozi, kwa sababu kundi la Bwana limechukuliwa mateka.
假使你們還不聽從這警告,對你的驕傲,我只有暗自痛哭,眼淚直流,因為上主的羊群已被擄去。
18 “Mwambieni mfalme na mama wa malkia, 'Jinyenyekezeni, na kukaa chini, kwa maana taji juu ya kichwa chako, kiburi chako na utukufu wako, umeanguka.'
你應對君王和太后說:「你們應坐低位,因為你們華麗的王冠已由你們頭上落下」。
19 Miji ya Negebu itafungwa, bila mtu wa kufungua. Yuda watachukuliwa mateka, wote uhamishoni.
南部的城邑已被封鎖,沒有人去打開,全猶大已被擄去。
20 Inua macho yako na angalia wale wanaokuja kutoka kaskazini. Je, ni kundi gani alilokupa, kundi ambalo lilikuwa zuri sana kwako?
請你舉目觀望那來自北方的人;昔日委託給你的羊群,那壯麗的羊群,如今在那裏﹖
21 Je, unasema nini wakati Mungu anawaweka wale ambao uliwafundisha kuwa marafiki? Je, huu si mwanzo wa maumivu ya utungu ambayo yatakuchukua kama mwanamke aliye katika kuzaa?
衪懲罰你,你還有什麼話說﹖是你教導了昔日的盟友來統治你,豈能不使你痛苦得像個臨產的婦女﹖
22 Kisha unaweza kusema moyoni mwako, 'Kwa nini mambo haya yanatokea kwangu?' Itakuwa kwa uovu wa maovu yako ambapo marinda yako yamefunuliwa na umeumizwa.
假使你心裏說:為什麼我遭遇了此事──是因你罪大惡極,你的衣邊才被掀起,你的腳才受到污辱。
23 Je, watu wa Kushi hubadilisha rangi yao ya ngozi, au chui hubadilisha madoa yake? Ikiwa ndivyo, basi wewe mwenyewe, ingawa unazoea uovu, utaweza kufanya mema.
雇士人豈能改變牠的斑點﹖那你們這些習於作惡的人,豈能行善﹖
24 Kwa hiyo nitawaangamiza kama makapi ambayo yanaangamia katika upepo wa jangwa.
為此,我必使他們四散,像被曠野裏的風捲去的草芥。
25 Hii ndiyo niliyokupa, sehemu ambayo nimekuagiza kwako-hili ndilo tamko la Bwana - kwa sababu umenisahau na kuamini katika udanganyifu.
這是你的命運,是我量給你的分子──上主的斷語──因為你忘記了我,信賴了「虛無」;
26 Kwa hiyo mimi mwenyewe nitaondoa nguo zako, na sehemu zako za siri zitaonekana.
故此我也要將你的衣邊掀到你面上,使人見到你的羞恥。
27 Uzinzi na ubembe wako, aibu ya tabia yako ya uasherati kwenye milima na katika mashamba! Nitayafanya yaonekane, mambo haya ya machukizo! Ole wako, Yerusalemu! Hutaki kuwa safi. Je! Hili litaendelea kwa muda gani?”
你的姦淫,你春情的嘶鳴,你猥褻的淫亂,你在高丘上和田野間可恥的行為,我都看見了。禍哉,耶路撒冷! 你不肯自潔,要到何時﹖