< Yakobo 1 >
1 Yakobo, mtumwa wa Mungu na wa Bwana Yesu Kristo, kwa makabila kumi na mbili yaliyotawanyika, salaam.
James, a servant of God and of the Lord Jesus Christ, to the twelve tribes who are in the dispersion: Health.
2 Hesabuni kuwa ni furaha zaidi, ndugu zangu, mnapopita katika matatizo mbali mbali,
My brethren, count it all joy, when you fall into diverse trials;
3 mkijua kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huwapa uvumilivu.
knowing that the proof of your faith works out patience.
4 Acheni uvumilivu uikamilishe kazi yake, kwamba muweze kukomaa kikamilifu, bila kupungukiwa katika lolote.
Let patience, therefore, have a perfect effect, that you may be perfect and complete, deficient in nothing.
5 Lakini kama mtu kati yenu anahitaji hekima, aiombe kutoka kwa Mungu, ambaye hutoa kwa ukarimu na pasipo kukemea kwa wote wamwombao, na atawapa hekima.
If any of you be deficient in wisdom, let him ask it of God: who gives to all men liberally, and upbraids not, and it shall be given to him.
6 Lakini omba kwa imani, bila shaka, kwa kuwa mwenye kutia shaka ni kama mawimbi katika bahari, huchukuliwa na upepo na kutupwa huku na huko.
But let him ask in faith, being not at all irresolute: for he who is irresolute, is like a wave of the sea, driven by the wind and tossed.
7 Kwa hakika mtu huyu asifikirie kwamba atapokelewa ombi lake kutoka kwa Bwana;
Now let not that man think, that he shall receive anything from the Lord.
8 mtu huyu ana nia mbili, si imara katika njia zake zote.
A man of two minds, is unstable in all his ways.
9 Ndugu maskini anapaswa kujivuna katika kusimama kwake juu,
Moreover, let the brother of humble condition glory in his exaltation,
10 wakati huo huo ndugu tajiri katika unyenyekevu wake, kwa sababu atatoweka kama ua la kondeni katika shamba analopita.
and the rich in his humiliation; for as a garden flower he shall pass away.--
11 Jua huchomoza na joto la kuunguza kukausha mimea, na maua huanguka na uzuri wake hufa. Vivyo hivyo watu matajiri watachakaa katikati ya kazi zao.
For the sun rises with a burning heat, and withers the herb, and its flower falls down, and the beauty of its appearance perishes: so also shall the rich man fade in his ways.
12 Amebarikiwa mtu yule anayevumilia majaribu, kwa kuwa baada ya kushinda jaribu hilo, atapokea taji ya uzima, ambayo imeahidiwa kwa wale wampendao Mungu.
Blessed is the man who sustains trial, for becoming an approved person, he shall receive the crown of life, which the Lord has promised to them who love him.
13 Mtu yeyote hapaswi kusema anapojaribiwa, “Jaribu hili linatoka kwa Mungu,” kwa sababu Mungu hajaribiwi na uovu, na Mungu mwenyewe hamjaribu yeyote.
Let no one who is tempted say, Certainly I am tempted by God: for God is incapable of being tempted by evil things, and he tempts no one.
14 Kila mtu hujaribiwa na tamaa zake mbaya zinazomshawishi na kumvuta mbali.
But every one is tempted, when he is drawn away, and enticed by his own lust:
15 Ndipo baada ya tamaa ya dhambi kubeba mimba, dhambi huzaliwa, na baada ya dhambi kukomaa sawasawa, huishia katika mauti.
then lust having conceived, brings forth sin, and sin, being perfected, brings forth death.
16 Ndugu zangu wapendwa, msidanganyike.
Be not deceived, my beloved brethren;
17 Kila zawadi iliyo nzuri na kila zawadi iliyokamilika hutoka juu, hushuka chini kutoka kwa Baba wa nuru. Kamwe habadiliki kama kivuli kibadilikavyo.
every good gift, and every perfect gift, is from above, descended from the Father of lights, with whom there is no variableness, nor shadow of turning.
18 Mungu alichagua kutupa sisi uzima kwa Neno la kweli, ili kwamba tuweze kuwa kama uzao wa kwanza miongoni mwa viumbe vyake.
Of his own will, he begot us by the word of truth, that we should be a kind of fruits of his creatures.
19 Mnajua hili, ndugu zangu wapendwa. Kila mmoja anapaswa kuwa mwepesi wa kusikia, siyo mwepesi wa kuongea wala kukasirika,
Wherefore, my beloved brethren, let every man be swift to hear, slow to speak, slow to wrath;
20 kwa kuwa hasira ya mwanadamu haiwezi kutenda haki ya Mungu.
for the wrath of man works not out the righteousness of God.
21 Kwa hiyo wekeni mbali uchafu wa dhambi na ubaya wote ulio mahali popote, na kwa unyenyekevu lipokeeni neno lililopandwa ndani yenu, ambalo lina uwezo wa kuokoa roho zenu.
Wherefore, putting away all filthiness, and overflowing of maliciousness, embrace with meekness the implanted word, which is able to save your souls.
22 Litiini neno, msilisikie tu, mkijidanganya nafsi zenu wenyewe.
And be doers of the word, and not hearers only, deceiving yourselves by false reasoning.
23 Kwa kuwa kama yeyote alisikiaye neno bila kulitendea kazi ni sawa na mtu ajiangaliaye uso wake halisi katika kioo.
For if any one be a hearer of the word, and not a doer, he is like a man who views his natural face in a mirror;
24 Hujitathimini uso wake, na huenda zake na baada ya muda mfupi husahau anavyofanana.
for he who looks at himself and goes away, and immediately forgets what kind of person he was.
25 Bali mtu yule anayeiangalia kwa uangalifu sheria kamili, sheria ya uhuru, na kuendelea kuitii, si kwa sababu yeye ni msikilizaji anayesahau, huyu mtu atabarikiwa anapoitenda.
But he who looks narrowly into the perfect law of liberty, and perseveres, not becoming a forgetful hearer, but a doer of its work, shall, in so doing, be happy.
26 Ikiwa mtu yeyote atafikiri mwenyewe kuwa ni mtu wa dini, lakini hawezi kuutawala ulimi wake, huudanganya moyo wake na dini yake ni bure.
If any one among you think to be religious, who bridles not his tongue, but deceives his own heart, the religion of this person is vain.
27 Dini iliyo safi na isiyoharibiwa mbele za Mungu wetu na Baba ni hii: kuwasaidia yatima na wajane katika mateso yao, na kujilinda wenyewe na ufisadi wa dunia.
Pure religion, and undefiled, with God, even the Father, is this: To take care of orphans and widows in their affliction, and to keep one's self unspotted from the world.