< Yakobo 5 >
1 Njoni sasa, enyi mlio matajiri, lieni kwa sauti ya juu kwa sababu ya taabu inayokuja juu yenu.
ⲁ̅ⲧⲉⲛⲟⲩ ϭⲉ ⲛⲉⲣⲙ̅ⲙⲁⲟ ⲣⲓⲙⲉ ⲛ̅ⲧⲉⲧⲛ̅ⲱϣ ⲉⲃⲟⲗ ⲉϫⲛ̅ⲛⲉⲧⲛ̅ⲧⲁⲗⲁⲓⲡⲟⲣⲓⲁ ⲛⲏⲩ ⲉϩⲣⲁⲓ [
2 Utajiri wenu umeharibiwa na mavazi yenu yametafunwa na wadudu waharibifu.
ⲃ̅ⲧⲉⲧⲛ̅ⲙⲛ̅ⲧⲣⲙ̅ⲙⲁⲟ ] ⲧⲁⲕ[ⲟ ]
3 Dhahabu zenu na fedha zenu zimekosa thamani, na uharibifu wake utashuhudia dhidi yenu na kuangamiza miili yenu kama moto. Mmejiwekea hazina yenu katika siku za mwisho.
ⲅ̅
4 Tazameni, malipo ya watendakazi-wale ambao hamjawalipa kwa kuvuna katika mashamba yenu- wanalia! Na kilio cha wale waliovuna mazao yenu kimeyafikia masikio ya Bwana wa Majeshi.
ⲇ̅ⲡⲉⲛⲧⲁⲧⲛ̅ϩⲟⲩⲣⲱⲟⲩ ⲙ̅ⲙⲟϥ ϥϫⲓϣⲕⲁⲕ ⲉⲃⲟⲗ. ⲁⲩⲱ ⲛ̅ⲁϣⲕⲁⲕ ⲛ̅ⲛⲉⲛⲧⲁⲩⲱϩⲥ̅ ⲁⲩⲃⲱⲕ ⲉϩⲟⲩⲛ ⲉⲙ̅ⲙⲁⲁϫⲉ ⲙ̅ⲡϫⲟⲉⲓⲥ ⲥⲁⲃⲃⲁⲱⲑ.
5 Mmeishi kwa anasa duniani na kujifurahisha ninyi wenyewe. Mmejinenepesha mioyo yenu kwa siku ya machinjo.
ⲉ̅ⲁⲧⲉⲧⲛ̅ⲧⲣⲩⲫⲁ ⲉϩⲣⲁⲓ ⲉϫⲙ̅ⲡⲕⲁϩ. ⲁⲩⲱ ⲁⲧⲉⲧⲛ̅ⲥⲡⲁⲧⲁⲗⲁ. ⲁⲧⲉⲧⲛ̅ⲥⲁⲁⲛϣ ⲛ̅ⲛⲉⲧⲛ̅ϩⲏⲧ ⲉⲡⲉϩⲟⲟⲩ ⲙ̅ⲡⲕⲱⲛⲥ̅.
6 Mmemhukumu na kumuua mwenye haki asiyeweza kuwapinga.
ⲋ̅ⲁⲧⲉⲧⲛ̅ϭⲁⲓⲟ. ⲁⲧⲉⲧⲛ̅ϩⲱⲧⲃ̅ ⲙ̅ⲡⲇⲓⲕⲁⲓⲟⲥ. ⲛ̅ϥϯ ⲟⲩⲃⲉⲧⲏⲩⲧⲛ̅ ⲁⲛ.
7 Kwa hiyo vumilieni, ndugu, mpaka ujio wa Bwana, kama mkulima husubiri mavuno ya thamani toka katika nchi, akisubiri kwa uvumilivu kwa ajili yake, mpaka mvua za kwanza na zile za mwisho zikinyesha.
ⲍ̅ϩⲣⲟϣ ϭⲉ ⲛ̅ϩⲏⲧ. ⲛⲁⲥⲛⲏⲩ. ϣⲁⲧⲡⲁⲣⲟⲩⲥⲓⲁ ⲙ̅ⲡⲉⲛϫⲟⲉⲓⲥ ⲉⲓⲥϩⲏⲏⲧⲉ ⲡⲟⲩⲟⲉⲓⲉ ϭⲱϣⲧ̅ ⲉⲃⲟⲗ ϩⲏⲧϥ̅ ⲙ̅ⲡⲕⲁⲣⲡⲟⲥ ⲉⲧⲧⲁⲉⲓⲏⲩ ⲛ̅ⲧⲉⲡⲕⲁϩ ⲉϥϩⲁⲣϣ̅ ⲛ̅ϩⲏⲧ ⲉϩⲣⲁⲓ ⲉϫⲱϥ. ϣⲁⲛⲧⲉϥϫⲓⲧϥ̅ ⲛ̅ϣⲟⲣⲡ̅ ⲁⲩⲱ ⲛ̅ϩⲁⲉ.
8 Pia ninyi muwe wavumilivu; kazeni mioyo yenu, kwa sababu kuja kwake Bwana ni karibu.
ⲏ̅ϩⲣⲟϣ ⲛ̅ϩⲏⲧ ϩⲱⲧⲧⲏⲩⲧⲛ̅ ⲛ̅ⲧⲉⲧⲛ̅ⲧⲁϫⲣⲟ ⲛ̅ⲛⲉⲧⲛ̅ϩⲏⲧ. ϫⲉ ⲁⲥϩⲱⲛ ⲉϩⲟⲩⲛ ⲛ̅ϭⲓⲧⲡⲁⲣⲟⲩⲥⲓⲁ ⲙ̅ⲡⲉⲛϫⲟⲉⲓⲥ.
9 Ndugu, msinung'unikiane ninyi kwa ninyi, kusudi msije mkahukumiwa. Tazama, hakimu anasimama mlangoni.
ⲑ̅ⲙ̅ⲡⲣ̅ⲁϣⲁϩⲟⲙ ⲉⲛⲉⲧⲛ̅ⲉⲣⲏⲩ. ⲛⲁⲥⲛⲏⲩ. ϫⲉⲕⲁⲥ ⲛ̅ⲛⲉⲩⲕⲣⲓⲛⲉ ⲙ̅ⲙⲱⲧⲛ̅. ⲉⲓⲥϩⲏⲏⲧⲉ ⲡⲉⲕⲣⲓⲧⲏⲥ ⲁϩⲉⲣⲁⲧϥ̅ ϩⲓⲣⲙ̅ⲡⲣⲟ.
10 Kwa mfano, ndugu, angalieni mateso na uvumilivu wa manabii walionena katika jina la Bwana.
ⲓ̅ϫⲓ ⲙ̅ⲡⲉⲥⲙⲟⲧ. ⲛⲁⲥⲛⲏⲩ. ⲙ̅ⲡϩⲓⲥⲉ ⲙⲛ̅ⲧⲙⲛ̅ⲧϩⲁⲣϣ̅ϩⲏⲧ ⲛ̅ⲛⲉⲡⲣⲟⲫⲏⲧⲏⲥ. ⲛⲁⲓ ⲛ̅ⲧⲁⲩϣⲁϫⲉ ϩⲙ̅ⲡⲣⲁⲛ ⲙ̅ⲡϫⲟⲉⲓⲥ.
11 Tazama, twawaita wale wanaovumilia, “heri.” Mmesikia uvumilivu wa Ayubu, na mnalijua kusudi la Bwana kwa ajili ya Ayubu, ni kwa jinsi gani Bwana amejaa huruma na rehema.
ⲓ̅ⲁ̅ⲉⲓⲥϩⲏⲏⲧⲉ ⲧⲛ̅ⲙⲁⲕⲁⲣⲓⲍⲉ ⲛ̅ⲛⲉⲛⲧⲁⲩϩⲩⲡⲟⲙⲓⲛⲉ. ⲁⲧⲉⲧⲛ̅ⲥⲱⲧⲙ̅ ⲉⲑⲩⲡⲟⲙⲟⲛⲏ ⲛ̅ⲓⲱⲃ. ⲁⲩⲱ ⲁⲧⲉⲧⲛ̅ⲛⲁⲩ ⲉⲑⲁⲏ ⲙ̅ⲡϫⲟⲉⲓⲥ. ϫⲉ ⲟⲩϣⲛ̅ϩⲧⲏϥ ⲡⲉ ⲡϫⲟⲉⲓⲥ ⲁⲩⲱ ⲟⲩⲛⲁⲏⲧ ⲡⲉ.
12 Zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, aidha kwa mbingu ama kwa nchi, au kwa kiapo cha aina nyingine. Bali hebu “ndiyo” yenu na imaanishe “ndiyo” na “hapana” yenu na imaanishe “hapana,” ili kwamba msije kuangukia chini ya hukumu.
ⲓ̅ⲃ̅ϩⲁⲑⲏ ⲇⲉ ⲛ̅ϩⲱⲃ ⲛⲓⲙ. ⲛⲁⲥⲛⲏⲩ. ⲙ̅ⲡⲣ̅ⲱⲣⲕ̅ ⲛ̅ⲗⲁⲁⲩ. ⲟⲩⲇⲉ ⲧⲡⲉ ⲟⲩⲇⲉ ⲡⲕⲁϩ ⲟⲩⲇⲉ ⲗⲁⲁⲩ ⲛ̅ⲁⲛⲁϣ. ⲙⲁⲣⲉϥϣⲱⲡⲉ ⲇⲉ ⲛ̅ϭⲓⲡⲉⲧⲛ̅ⲥⲉ ⲛ̅ⲥⲉ ⲁⲩⲱ ⲡⲉⲧⲛ̅ⲙ̅ⲙⲟⲛ ⲛ̅ⲙ̅ⲙⲟⲛ. ϫⲉⲕⲁⲥ ⲛ̅ⲛⲉⲩⲕⲣⲓⲛⲉ ⲙ̅ⲙⲱⲧⲛ̅.
13 Kuna yeyote miongoni mwenu ana mateso? Lazima aombe. Je, mtu yeyote ni mwenye kuchangamka? Na aimbe sifa.
ⲓ̅ⲅ̅ⲡⲉⲧϣⲡ̅ϩⲓⲥⲉ ⲛ̅ϩⲏⲧⲧⲏⲩⲧⲛ̅ ⲙⲁⲣⲉϥϣⲗⲏⲗ. ⲡⲉⲧⲣⲟⲟⲩⲧ ⲙⲁⲣⲉϥⲯⲁⲗⲗⲉⲓ.
14 Je, kuna yeyote miongoni mwenu aliye mgonjwa? Na awaite wazee wa kanisa, nao wazee wa kanisa waombe juu yake, wakimpaka mafuta katika jina la Bwana,
ⲓ̅ⲇ̅ⲡⲉⲧϣⲱⲛⲉ ⲛ̅ϩⲏⲧⲧⲏⲩⲧⲛ̅ ⲙⲁⲣⲉϥⲙⲟⲩⲧⲉ ⲉⲛⲉⲡⲣⲉⲥⲃⲩⲧⲉⲣⲟⲥ ⲛ̅ⲧⲉⲕⲕⲗⲏⲥⲓⲁ. ⲛ̅ⲥⲉϣⲗⲏⲗ ⲉϩⲣⲁⲓ ⲉϫⲱϥ. ⲉⲁⲩⲧⲁϩⲥϥ̅ ⲛ̅ⲟⲩⲛⲉϩ ϩⲙ̅ⲡⲣⲁⲛ ⲙ̅ⲡϫⲟⲉⲓⲥ.
15 na maombi ya imani yatamponya mgonjwa, na Bwana atamwinua. Na kama atakuwa ametenda dhambi, Mungu atamsamehe.
ⲓ̅ⲉ̅ⲁⲩⲱ ⲡⲉϣⲗⲏⲗ ⲙⲛ̅ⲧⲡⲓⲥⲧⲓⲥ ⲛⲁⲧⲟⲩϫⲉⲡⲉⲧϣⲱⲛⲉ. ⲁⲩⲱ ⲡϫⲟⲉⲓⲥ ⲛⲁⲧⲟⲩⲛⲟⲥϥ̅. ⲕⲁⲛ ⲉϣⲱⲡⲉ ⲁϥⲣ̅ϩⲉⲛⲕⲉⲛⲟⲃⲉ ⲥⲉⲛⲁⲕⲁⲁⲩ ⲛⲁϥ ⲉⲃⲟⲗ.
16 Kwa hiyo ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana kila mmoja na mwenzake, ili muweze kuponywa. Maombi ya mwenye haki huzaa matokeo makubwa.
ⲓ̅ⲋ̅ⲟⲩⲱⲛϩ̅ ϭⲉ ⲉⲃⲟⲗ ⲛ̅ⲛⲉⲧⲛ̅ⲛⲟⲃⲉ ⲛ̅ⲛⲉⲧⲛ̅ⲉⲣⲏⲩ ⲛ̅ⲧⲉⲧⲛ̅ϣⲗⲏⲗ ϩⲁⲛⲉⲧⲛ̅ⲉⲣⲏⲩ. ϫⲉⲕⲁⲥ ⲉⲩⲉⲕⲱ ⲛⲏⲧⲛ̅ ⲉⲃⲟⲗ. ⲡⲥⲟⲡⲥ̅ ⲙ̅ⲡⲇⲓⲕⲁⲓⲟⲥ ϭⲙ̅ϭⲟⲙ ⲉⲙⲁⲧⲉ ⲁⲩⲱ ⲉϥⲉⲛⲉⲣⲅⲉⲓ.
17 Eliya alikuwa mtu mwenye hisia kama zetu, aliomba kwa juhudi kwamba mvua isinyeshe, na haikunyesha katika nchi kwa muda wa miaka mitatu na miezi sita.
ⲓ̅ⲍ̅ϩⲏⲗⲓⲁⲥ ⲛⲉⲟⲩⲣⲱⲙⲉ ⲡⲉ ⲛ̅ⲧⲛ̅ϩⲉ. ⲁⲩⲱ ϩⲛ̅ⲟⲩϣⲗⲏⲗ ⲁϥϣⲗⲏⲗ ⲉⲧⲙ̅ⲧⲣⲉⲧⲡⲉ ϩⲱⲟⲩ. ⲁⲩⲱ ⲙ̅ⲡⲉⲥϩⲱⲟⲩ ⲉϩⲣⲁⲓ ⲉϫⲙ̅ⲡⲕⲁϩ ⲛ̅ϣⲟⲙⲛ̅ⲧ ⲛ̅ⲣⲟⲙⲡⲉ ⲙⲛ̅ⲥⲟⲟⲩ ⲛ̅ⲉⲃⲱⲧ.
18 Na Eliya aliomba tena, na mbingu zilimwaga mvua juu ya nchi na nchi ikatoa mavuno.
ⲓ̅ⲏ̅ⲙⲛ̅ⲛ̅ⲥⲱⲥ ⲟⲛ ⲁϥϣⲗⲏⲗ. ⲁⲧⲡⲉ ϯ ⲛ̅ⲛⲉⲥϩⲱⲟⲩ. ⲁⲡⲕⲁϩ ϯⲟⲩⲱ ⲙ̅ⲡⲉϥⲕⲁⲣⲡⲟⲥ.
19 Ndugu zangu, kama yeyote miongoni mwenu anapotoka kutoka kwenye ukweli, lakini mtu mwingine akamrejesha,
ⲓ̅ⲑ̅ⲛⲁⲥⲛⲏⲩ. ⲉⲣϣⲁⲛⲟⲩⲁ ⲛ̅ϩⲏⲧⲧⲏⲩⲧⲛ̅ ⲡⲗⲁⲛⲁ ⲉⲃⲟⲗ ϩⲛ̅ⲧⲙⲉ. ⲛ̅ⲧⲉⲟⲩⲁ ⲕⲧⲟϥ.
20 hebu na ajue kuwa yeyote amwongozaye mwenye dhambi kuondoka katika njia yake ya ukosaji ataponya nafsi yake kutoka katika mauti na atafunika wingi wa dhambi.
ⲕ̅ⲡⲉⲧⲛⲁⲕⲧⲟ ⲇⲉ ⲛ̅ⲟⲩⲣⲉϥⲣ̅ⲛⲟⲃⲉ ⲉⲃⲟⲗ ϩⲛ̅ⲧⲉϩⲓⲏ ⲛ̅ⲧⲉϥⲡⲗⲁⲛⲏ ϥⲛⲁⲧⲟⲩϫⲟ ⲛ̅ⲟⲩⲯⲩⲭⲏ ⲉⲃⲟⲗ ϩⲙ̅ⲡⲙⲟⲩ. ⲛϥ̅ϩⲱⲃⲥ̅ ⲉⲃⲟⲗ ⲉϫⲛ̅ⲟⲩⲙⲏⲏϣⲉ ⲛ̅ⲛⲟⲃⲉ.