< Isaya 66 >
1 Yahwe asema hivi, ''Mbinguni ni makao yangu, na nchi ni miguu yangu. Iko wapi nyumba uliyonitengenezea mimi? iko wapi sehemu amabayo ninaweza kupumzika?
Thus saith Jehovah: Heaven is my throne, And the earth my footstool; Where is the house that ye can build me, And where is the place of my rest?
2 Mkono wangu umeyafanya haya yote; hivi ndovyo jinsi ambavyo vitu vitatokeavyo—hili ndilo tamko la Yahwe. Mtu niliyempitisha, mwenye roho iliyopondeka na mwenye kujutia roho, na atetemekaye kwa ajili ya neno langu.
For all these things hath my hand made; By it do all these things exist, saith Jehovah. But to this man will I look, Even to him who is humble and of a contrite spirit, And who trembleth at my word.
3 Yeyote achinjae ng'ombe humuua mtu pia; yeye anayetoa sadaka ya kondoo huvunja shingo ya mbwa pia; yeye anayetoa sadaka ya mavuno anatoa sadaka ya damu yangurue; yeye anayetoa kumbukumbuvumba huwabariki wakosaji pia. Wamechagua njia zao wenyewe wanachukua radhi kwa uchafu wao wenyewe.
He that slayeth an ox killeth a man; He that sacrificeth a lamb beheadeth a dog; He that maketh an oblation offereth swine's blood; He that burneth incense blesseth an idol. Yea, they have chosen their own ways, And in their abominations their souls delight.
4 Katika njia hiyo hiyo nitachagua adhabu yao wenyewe; Nitaleta juu yao kitu wanachokiogopa, maana niilpowaita, hakuna aliyeitika; nilipozungumza aliyenisikiliza mimi. Walifanya yaliyo maovu mbele yangu, na kuchagua yasiyo nipenindeza mimi.''
I also will choose their calamities; What they dread I will bring upon them; Because I called, and no one answered, I spake, and they did not hear; But they did what is evil in my sight, And chose that in which I have no delight.
5 Sikiliza neno la Yahwe, ewe utemekae kwa neno lake, ''Kaka zako wanaonichukia na kukutenga wewe kwa ajili ya jina langu walisema, 'Na atukuzwe Yahwe, halafu tutaiona furaha yenu; lakini mtatiwa katika aibu.
Hear the word of Jehovah, Ye that tremble at his word! “Your brethren that hate you, And thrust you out for my name's sake, have said, “May Jehovah be glorified, that we may see your joy!” But they shall be confounded.
6 Sauti ya vita vya ghasi vinakuja katika mji, sauti kutoka hekaluni, sauti ya Yahwe anawarudia maadui zake.
A voice of tumult from the city! A voice from the temple! The voice of Jehovah, rendering recompense to his enemies!
7 Kabla ajaenda katika chumba, hujifungua; kabla ya uchungu kumtoka hujifungua mtoto wa kiume.
Before she was in travail, she brought forth, Before her pangs came, she was delivered of a son.
8 Ni nani asikiaye mambo haya? Ni nani aonae mambo haya? Je taifa linaweza kuanzishwa kwa wakati mmoja? lakini kwa haraka Sayuni inapokwenda katika chumba, hujifungua watoto wake.
Who hath heard such a thing? Who hath seen such things? Is a country brought forth in a day? Is a nation born at once? For as soon as Zion was in travail, she brought forth her children.
9 Ninawezaje kumleta mtoto azaliwe na nisimruhusu mtoto azaliwe? Yahwe auliza? — au Je ninamleta mtoto wakati tu wa kujifungua na halafu nimshikilie tena - anauliza Yahwe.''
Shall I bring to the birth, and not cause to bring forth, saith Jehovah; Shall I, who beget, restrain the birth? saith thy God.
10 Furahia na Yerusalemu na fuhahia kwa ajili yake, ninyi nyote mnaopenda yeye; furahia pamoja na yeye, ninyi mnaomboleza juu yake!
Rejoice ye with Jerusalem, And exult for her, all ye that love her! Be very joyful with her, all ye that mourn for her!
11 Maana utamuuguza na ataridhika, katika maziwa yake atakufariji; utakunywa mpaka ushibe na kufurahia kwa wingi wa utukufu wake.
That ye may suck, and be satisfied, from the breast of her consolations, That ye may suck and be delighted with the fulness of her glory.
12 Yahwe asema hivi, ''Ni nanakaribia kutawanya mafanikio juu katika mto, na utajiri wa mataifa kama wingi wa mkondo wa maji. Utamuuguza kwa upande wake, na kubebwa katika mikono yake, mtabebwa juu ya magoti yake.
For thus saith Jehovah: Behold, I will bring prosperity to her like a river, And the wealth of the nations like an overflowing stream; Ye shall suck at the breast, Ye shall be carried on the arm, And on the knees shall ye be dandled.
13 Kama vile mama anavyomfariji mtoto wake, hivyo basi nami nitawafariji ninyi, na mtapata faraja katika Yerusalemu.''
As one whom his mother comforteth, So will I comfort you; And in Jerusalem shall ye be comforted.
14 Utayaona haya, na moyo wako utafurahia, na mifupa yako itachipukia kama zabuni ya nyasi. Aridhi ya Yahweitajulikana kwa watumishi wake, lakini atawaonyesha hasira yake dhidi ya maadui zake.
Ye shall see, and your heart shall rejoice, And your bones shall flourish like a green plant, And the hand of Jehovah shall be manifested to his servants, And be moved with indignation against his enemies.
15 Kwa kutazama, Yahwe anakuja kwa moto, na gari lake linakuja kama upepo wa dhoruba kuleta joto katika hasira yake na kukemea kwake ni kama moto uwakao.
For behold, Jehovah cometh with fire, Like a whirlwind are his chariots, To breathe forth his anger in a glowing heat, And his rebuke in flames of fire.
16 Maana Yahwe ametekeleza hukumu juu ya watu kwa moto na kwa upanga wake. Wale watakaouliwa na Yahwe watakuwa wengi.
For with fire will Jehovah contend, And with his sword, with all flesh, And many shall be the slain of Jehovah.
17 Watajiweka wakfu wenyewe na kujisafisha wenywe, ili waweze kuingia katika bustani, kumfuata aliyeko katikati ya wale walao nyama ya nguruwe na vitu haramu kama panya. ''Watafika mwisho - hili ni tamko la Yahwe.
They who sanctify and purify themselves in the groves, Following one in the midst, Who eat swine's flesh, and the abomination, and the mouse. They shall all perish together, saith Jehovah.
18 Maana ninayajua matendo yao na mawazo yao. Wakatiutafika nitakapoyakusanya mataifa yote na lugha zote. Watakuja na kuona utukufu wangu.
For I know their works, and their thoughts; The time cometh to gather all nations and tongues together; They shall come, and behold my glory.
19 Nitaweka ishara ya ukuu wangu miongoni mwao. Halafu nitawatuma wakazi kutoka miongoni mwao kwa mataifa. Kwa Tarshishi, Puti, na Ludi, upinde wale wanaochukua upinde wao, kwa Tubali, Javani, na umbali kuelekea katika pwani kule ambapo hawajasikia chochote kuhusu mimi wala kuona utukufu wangu. Watatangaza utukufu wangu miongoni mwa mataifa.
And I will give a sign among them, And of those that escape I will send to the nations, To Tarshish, Phul, and Lud, who draw the bow, to Tubal and Javan, To the distant coasts, who never heard my name, And who never saw my glory; And they shall declare my glory among the nations.
20 Watawaleta kaka zako wote nje ya mataifa yote, kama sadaka kwa Yahwe. Watakuja kwa farasi na kwa gari, na kwa gari, juu ya nyumbu na juu ya ngamia, kuelekea mlima wangu mtakatifu Yerusalemu - asema Yahwe. Maana watu wangu wa Israeli wataleta sadaka ya mavuno kwenye vyombo visafi katika nyumba ya Yahwe.
And they shall bring all your brethren From all the nations, an offering to Jehovah, Upon horses, and in chariots, and in litters, and upon mules and dromedaries, To my holy mountain, Jerusalem, saith Jehovah, As the sons of Israel bring their gifts In pure vessels to the house of Jehovah.
21 Baadhi ya vitu hivi nitavichagua kama makuhani na walawi — asema Yahwe.
And of them will I also take For priests and for Levites, saith Jehovah.
22 Maana itakuwa mbingu mpya na nchi mpya ambayo nitakayoifanya ibaki mbele zangu— Hili ndilo tamko la Yahwe— Hivyo ndivyo ukoo wenu utakavyobakia, na jina lenu litabaki.
For as the new heavens, And the new earth, which I make, Endure before me, saith Jehovah, So shall your race and your name endure.
23 Kutoka mwenzi mmoja mpaka mwingine, na kutoka sabato moja mpaka nyingine, watu wote watakuja kukuinamia chini— asema Yahwe.
And it shall be, from new moon to new moon, And from sabbath to sabbath, That all flesh shall come and worship before me, saith Jehovah.
24 Watakwenda nje na kuona miili ya wafu ya watu walioniasi mimi, maana wadudu wawalao wao hatakufa, na moto huwaunguzao hautazimika; na itakuwa ni chuki kwa wale wote wenye mwili.''
Then shall they go forth and see The dead bodies of the men that rebelled against me! For their worm shall not die, And their fire shall not be quenched, And they shall be an abhorrence to all flesh.