< Isaya 55 >
1 ''Njooni, kila aliye na kiu, njooni kwenye maji! na ewe usio na pesa, njoo, ununua na ule! Njoo, nunua mvinyo na maziwa pasipo pesa na pasipo gharama.
“Come, all you who are thirsty, come to the waters; and you without money, come, buy, and eat! Come, buy wine and milk without money and without cost!
2 Kwa nini tunapima fedha kwa kitu ambacho sio mkate? na kufanya kazi isiyoridhisha? Nisikilizeni mimi kwa makini na ule kilicho kizuri, na kujifurahisha mwenyewe kwa unono.
Why spend money on that which is not bread, and your labor on that which does not satisfy? Listen carefully to Me, and eat what is good, and your soul will delight in the richest of foods.
3 Jeuzeni masikio yenu, na mje kwangu! Sikiliza, iliuweze kuishi! Nitafanya agano ya milele na ninyi; pendo langu la kuaminika nililomuhaidi Daudi.
Incline your ear and come to Me; listen, so that your soul may live. I will make with you an everlasting covenant— My loving devotion promised to David.
4 Tazama, nimwemuweka yeye kama shahidi kwa mataifa, kama kiiongozi na kamanda wa watu.
Behold, I have made him a witness to the nations, a leader and commander of the peoples.
5 Tazama, utaliita taifa ambalo haulijui; na taifa ambalo halikujui wewe litakukimbilia wewe kwa sababu wewe ni Yahwe Mungu wao, Mtakatifu wa Israeli, yeye aliyekutukuza wewe.
Surely you will summon a nation you do not know, and nations who do not know you will run to you. For the LORD your God, the Holy One of Israel, has bestowed glory on you.”
6 Mtafuteni Yahwe maana anapatikana; muiteni yeye maana yu karibu.
Seek the LORD while He may be found; call on Him while He is near.
7 Tuwaache waovu waziache njia zao, na mtu mwenye dhambi mawazo yake. Muache yeye arudi kwa Yahwe, na atamuhurumia yeye, na kwa Mungu wetu, yeye ambaye atamsamehe huyo kwa wingi.
Let the wicked man forsake his own way and the unrighteous man his own thoughts; let him return to the LORD, that He may have compassion, and to our God, for He will freely pardon.
8 Maana mawazo yangu sio mawazo yenu, wala njia zangu sio njia zenu- Hili ni tamko la Yahwe-
“For My thoughts are not your thoughts, neither are your ways My ways,”
9 maana kama vile mbingu zilivyo juu kuliko nchi, hivyo ndivyo njia zangu zilivyo juu kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.
“For as the heavens are higher than the earth, so My ways are higher than your ways and My thoughts than your thoughts.
10 Maana kama mvua na theluji zishukavyo chini kutoka mbinguni na hazirudi tena pale isipokuwa kueneza nchi na kufanya uzalishaji na chipukizi na kutoa mbegu kwa wakulima waliopanda na mkate kwa walaji,
For just as rain and snow fall from heaven and do not return without watering the earth, making it bud and sprout, and providing seed to sow and food to eat,
11 hivyo neno langu litakuwa linalotoka kwenye mdomo wangu: halitanirudia tena mimi bure, Lakini itatimiza lilie nililokusudia, na litatimiza lile nililolituma.
so My word that proceeds from My mouth will not return to Me empty, but it will accomplish what I please, and it will prosper where I send it.
12 Maana utakwenda nje katika furaha na utaongozwa kwa amani; Milima na vilima vitapaza sauti kwa furaha mbele yako, na miti yote shambani itapiga makofi.
You will indeed go out with joy and be led forth in peace; the mountains and hills will burst into song before you, and all the trees of the field will clap their hands.
13 Badala ya miiba ya porini, misonobari itakuwa; na badala ya mbigiri, mihadasi inaota, na itakuwa kwa Yahwe, maana jina lake, ni kama alama ya milele ambayo haiwezi kuondolewa.''
Instead of the thornbush, a cypress will grow, and instead of the brier, a myrtle will spring up; they will make a name for the LORD, an everlasting sign, never to be destroyed.”