< Isaya 54 >
1 ''Imba, ewe mwanamke tasa, ewe ambaye haujazaa; imba wimbo kwa furaha na lia kwa nguvu ewe ambaye hujapata uchungu wa kuzaa. Maana watoto walio katika ukiwa ni wengi kuliko watoto wa wanawake waliolewa,'' asema Yahwe.
“Imba, ewe mwanamke tasa, wewe ambaye kamwe hukuzaa mtoto; paza sauti kwa kuimba, piga kelele kwa furaha, wewe ambaye kamwe hukupata utungu; kwa sababu watoto wa mwanamke aliyeachwa ukiwa ni wengi kuliko wa mwanamke mwenye mume,” asema Bwana.
2 Fanya hema lako kuwa kubwa na tawanya mapazia mbali, sio kidogo; nyoosha kamba zako na imarisha vigingi vyako.
“Panua mahali pa hema lako, tandaza mapazia ya hema lako uyaeneze mbali, wala usiyazuie; ongeza urefu wa kamba zako, imarisha vigingi vyako.
3 Maana utawanjwa katika mkono wa kulia na wa kushoto, na ukoo wako utashinda mataifa na kuwapatia miji iliyo na ukiwa.
Kwa maana utaenea upande wa kuume na upande wa kushoto; wazao wako watayamiliki mataifa na kukaa katika miji yao iliyoachwa ukiwa.
4 Usiogope maana hautahaibika, wala kukatishwa tamaa maana hautapatwa na aibu; hutasahau aibu ya ujana wako na aibu ya kutelekezwa.
“Usiogope, wewe hutaaibika. Usiogope aibu, wewe hutaaibishwa. Wewe utasahau aibu ya ujana wako, wala hutakumbuka tena mashutumu ya ujane wako.
5 Maana Muumba ni mume wako; Yahwe wa majeshi ndilo jina lake. Mtakatifu wa Israeli yeye ni mkombozi wenu; anaitwa Mungu wa nchi yote.
Kwa maana Muumba wako ndiye mume wako, Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli ni Mkombozi wako, yeye anaitwa Mungu wa dunia yote.
6 Yahwe anakuita wew urudi kama mwanamke aliyetelekezwa na mwenye roho ya huzuni, kama mwanamke mdogo aliyeolewa na kukataliwa, asema Mungu.
Bwana atakuita urudi kana kwamba ulikuwa mke aliyeachwa na kuhuzunishwa rohoni; kama mke aliyeolewa bado angali kijana na kukataliwa,” asema Mungu wako.
7 ''Kwa kipindi kifupi nimewatelekeza ninyi, lakini kwa huruma kubwa nitawakusanya ninyi.
“Kwa kitambo kidogo nilikuacha, lakini kwa huruma nyingi nitakurudisha.
8 Katika gharikia ya hasira nimeuficha uso wangu kwa muda. lakini kwa agano la milele la kuaminika nitakuwa na huruma na ninyi- amesema Yahwe, aliyewakomboa ninyi.
Katika ukali wa hasira nilikuficha uso wangu kwa kitambo, lakini kwa fadhili za milele nitakuwa na huruma juu yako,” asema Bwana Mkombozi wako.
9 Maana haya ni kama Nuhu kwangu: kama nilivyoapa maji ya Nuhu hayuatapita tena katika nchi, Hivyo nimeapa kwama sitapatwa na hasira na ninyi wala kuwakemea ninji.
“Kwangu mimi jambo hili ni kama siku za Noa, nilipoapa kuwa maji ya Noa kamwe hayatafunika tena dunia. Hivyo sasa nimeapa sitawakasirikia ninyi, kamwe sitawakemea tena.
10 Japo milima yaweza kuanguka na vilima vyaweza kutikiswa, japo uimara wa pendo langu hautageuka nyuma kutoka kwenu, wala agano langu la amani kutikiswa- asema Yahwe, Yeye mwenye huruma juu yenu.
Ijapotikisika milima, na vilima viondolewe, hata hivyo upendo wangu usiokoma kwenu hautatikisika, wala agano langu la amani halitaondolewa,” asema Bwana, mwenye huruma juu yenu.
11 Wanaotaabika, wanaopitia dhoruba na wasio na faraja, tazama, nitaweka lami kwa rangi nzuri, na kuweka misingi kwa yakuti.
“Ewe mji uliyeteswa, uliyepigwa kwa dhoruba na usiyetulizwa, nitakujenga kwa almasi, nitaweka misingi yako kwa yakuti samawi.
12 Nitaufanya mnara wa akiki na lango yake ya almasi na kuta zake za nje ni za mawe mazuri.
Nitafanya minara yako ya akiki, malango yako kwa vito vingʼaavyo, nazo kuta zako zote za vito vya thamani.
13 Na watoto wako wote watafundishwa na Yahwe; na amani ya watoto wako itakuwakubwa.
Watoto wako wote watafundishwa na Bwana, nayo amani ya watoto wako itakuwa kuu.
14 Katika haki nitakuanzisha tena. Hautaona dhiki tena, maana hautaogopa, na hakuna kitu cha kutisha kitakachokuja karibu yako.
Kwa haki utathibitika: Kuonewa kutakuwa mbali nawe; hutaogopa chochote. Hofu itakuwa mbali nawe; haitakukaribia wewe.
15 Tazama, ikiwa yeyote atakaye koroga matatizo, hayatako kwangu; yeyote atakaye changanya matatizo pamaoja na wewe ataanguka kwa kishindo.
Kama mtu yeyote akikushambulia, haitakuwa kwa ruhusa yangu; yeyote akushambuliaye atajisalimisha kwako.
16 Tazama, nimemumba fundi, anayepuliza makaa yanayoungua na na kuanda a silsha kama kazi yake, na nimemumba mharibifu ili awaharibu.
“Tazama, ni mimi niliyemuumba mhunzi, yeye afukutaye makaa kuwa moto, na kutengeneza silaha inayofaa kwa kazi yake. Tena ni mimi niliyemwambia mharabu kufanya uharibifu mwingi.
17 Hakuna silaha iliyotengenezwa dhidi yako ikafanikiwa; na utamlaani kila mmjoa anayekutusi wewe. Huu ndio urithi wa watumishi wa Yahwe, na uthibitisho wake kutoka kwangu- Hili ndilo tamko la Yahwe.''
Hakuna silaha itakayofanyizwa dhidi yako itakayofanikiwa, nawe utauthibitisha kuwa mwongo kila ulimi utakaokushtaki. Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana na hii ndiyo haki yao itokayo kwangu,” asema Bwana.