< Isaya 52 >
1 Amka, amka, vaa nguvu zako, Sayuni; vaa vazi lako zuri, mji mtakatifu; maana hakuna tena kutotahiriwa wala wasio safi kuingia kwako.
Amka, amka, ee Sayuni, jivike nguvu. Vaa mavazi yako ya fahari, ee Yerusalemu, mji mtakatifu. Asiyetahiriwa na aliye najisi hataingia kwako tena.
2 Jikung'ute mwenyewe kutoka mavumbini; nyanyuka na ukae, ewe Yerusalemu; ondoa shanga katika shingo yako, wafungwa, binti ya Sayuni.
Jikungʼute mavumbi yako, inuka, uketi kwenye kiti cha enzi, ee Yerusalemu. Jifungue minyororo iliyo shingoni mwako, ee Binti Sayuni uliye mateka.
3 Maana Yahwe asema hivi, umeuzwa bure, na utakombolewa pasipo pesa.''
Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana: “Mliuzwa pasipo malipo, nanyi mtakombolewa bila fedha.”
4 Maana Bwana Yahwe asema hivi, ''Hapo mwanzo watu wangu walishuka chini Misri kuishi kwa muda mfupi; Waasiria waliwanyanyasa wao hivi karibuni.
Kwa maana hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi: “Hapo kwanza watu wangu walishuka Misri kuishi, hatimaye, Ashuru wakawaonea.
5 Sasa ni kitu gani nilicho nacho hapa- Hili ni tamko Yahwe- aonae kwamba watu wake wanachukuliwa bure tu? Wale wanowaongoza wao wanafanya mzaha-Hili ni tamko la Yahwe- jina langu linakashifiwa mchan kutwa.
“Basi sasa nina nini hapa?” asema Bwana. “Kwa kuwa watu wangu wamechukuliwa pasipo malipo, nao wale wanaowatawala wanawadhihaki,” asema Bwana. “Mchana kutwa jina langu limetukanwa bila kikomo.
6 Hivyo basi watu wangu watalijua jina langu; watajua kwamba siku hiyo kwamba mimi ndiye ninayesema ''Ndiyo, Ni Mimi!''
Kwa hiyo watu wangu watalijua Jina langu; kwa hiyo katika siku ile watajua kwamba ndimi niliyetangulia kulisema. Naam, ni mimi.”
7 Ni kwa uzuri gani juu miliima ni miguu ya mjumbe aliyeleta habari njema, atangazae amani, aliyebeba uzuri wa ukuu, aliyetangaza wokovu, anayesema kwa Sayuni, ''Mungu wako anatawala!''
Tazama jinsi miguu ya wale waletao habari njema ilivyo mizuri juu ya milima, wale wanaotangaza amani, wanaoleta habari njema, wanaotangaza wokovu, wauambiao Sayuni, “Mungu wako anatawala!”
8 Sikiliza enyi walinzi nyanyueni sauti zenu, kwa pamoja pigeni kelele kwa furaha, maana mtamuona, kwa kila jicho lenu, kurejea kwa Yahwe Sayuni.
Sikiliza! Walinzi wako wanapaza sauti zao, pamoja wanapaza sauti zao kwa furaha. Wakati Bwana atakaporejea Sayuni, wataliona kwa macho yao wenyewe.
9 Pazeni sauti kwa kuimba kwa furaha, enyi mateka wa Yerusalemu; maana Yahwe amefariji watu wake; ameikomboa Yerusalemu.
Pazeni sauti ya nyimbo za furaha pamoja, enyi magofu ya Yerusalemu, kwa maana Bwana amewafariji watu wake, ameikomboa Yerusalemu.
10 Yahwe amewaonyesha kwamba mkono wake mtakatifu katika macho ya mataifa yote; nchi yote itauona wokovu wa Mungu wetu.
Mkono mtakatifu wa Bwana umefunuliwa machoni pa mataifa yote, nayo miisho yote ya dunia itaona wokovu wa Mungu wetu.
11 Ondokeni, ondokeni, enendeni mbali na hapa; msiguse kitu chochote ambacho ni najisi; au kuishi katikati yake; jitakase mwenyewe, enyi mliobeba vyombo vya Yahwe.
Ondokeni, ondokeni, tokeni huko! Msiguse kitu chochote kilicho najisi! Tokeni kati yake mwe safi, ninyi mchukuao vyombo vya Bwana.
12 Maana hautakwenda nje kwa kukimbia, wala hautaondoka kwa hofu; Maana Yahwe atakuwa mbele yako; na Mungu wa Israeli atakuwa mlinzi wako nyuma.
Lakini hamtaondoka kwa haraka, wala hamtakwenda kwa kukimbia; kwa maana Bwana atatangulia mbele yenu, Mungu wa Israeli atakuwa mlinzi nyuma yenu.
13 Tazameni, mtumishi wangu atafanya hekima; atakuwa juu na atanyanyuliwa juu, na atapandishwa juu.
Tazama, mtumishi wangu atatenda kwa hekima; atatukuzwa, na kuinuliwa juu, na kukwezwa sana.
14 Na wengi watamstajabia yeye- muonekano wake umekunjamana nje ya muonekano wa mwanadamu, hivyo basi upande wake ulikuwa mbali na kitu chochote ambacho ni binadamu-
Kama walivyokuwa wengi walioshangazwa naye, kwani uso wake ulikuwa umeharibiwa sana zaidi ya mtu yeyote na umbo lake kuharibiwa zaidi ya mfano wa mwanadamu:
15 Na hivyo, mtumishi wangu atanyunyizia mataifa mengi na wafme watafunga midomo yao kwa sababu yake. Kana kwamba hawajawahi kuambiwa, wataona, kana kwamba hawakusikia, wataelewa.
hivyo atayashangaza mataifa mengi, nao wafalme watafunga vinywa vyao kwa sababu yake. Kwa kuwa yale ambayo hawakuambiwa, watayaona, nayo yale wasiyoyasikia, watayafahamu.