< Isaya 43 >

1 Lakini sasa haya ndio Yahwe asemayo, yeye aliyekuumba ewe, Yakobo, na yeye aliyekuumba ewe, Israeli: ''Usiogope, kwa maana nimekukomboa wewe; nmeikuita kwa jina lako, wewe ni wangu.
ועתה כה אמר יהוה בראך יעקב ויצרך ישראל אל תירא כי גאלתיך קראתי בשמך לי אתה׃
2 Utakapopita katika maji, Nitakuwa pamoja na wewe; na katika mito, hayatakuzuru wewe. Utakapotembea katika moto hautaungua, na moto hautakuharibu wewe.
כי תעבר במים אתך אני ובנהרות לא ישטפוך כי תלך במו אש לא תכוה ולהבה לא תבער בך׃
3 Maana mimi Yahwe Mungu wako, Mtakatifu wa Israeli Mkombozi wenu. Nimewapa Misri kama fidia yenu, Ethiopia na Seba watabadilishana kwako.
כי אני יהוה אלהיך קדוש ישראל מושיעך נתתי כפרך מצרים כוש וסבא תחתיך׃
4 Kwa maana ulikuwa wa thamani na maalumu katika macho yangu, Ninakupenda; kwa sababu hiyo Nitatoa watu kwa ajili yako, na watu wengine kwa ajili ya maisha yako.
מאשר יקרת בעיני נכבדת ואני אהבתיך ואתן אדם תחתיך ולאמים תחת נפשך׃
5 Usiogope, maana Mimi niko pamoja na wewe; Nitawarudisha watoto wako kutoka mashariki, na kuwakusanya nyie kutoka magharibi.
אל תירא כי אתך אני ממזרח אביא זרעך וממערב אקבצך׃
6 Nitasema na kaskazini, 'Wakabidhini wao; na kwa kusini, Usiangalie ya nyuma; Leteni vijana wangu kutoka mbali na binti zangu kutoka vijiji vya mikoani katika nchi,
אמר לצפון תני ולתימן אל תכלאי הביאי בני מרחוק ובנותי מקצה הארץ׃
7 yeyote aitwe kw jina langu, niliyemuumba kwa utukufu wangu mwenyewe, Niliyemuumba, ndio, Mimi niliyemfanya.
כל הנקרא בשמי ולכבודי בראתיו יצרתיו אף עשיתיו׃
8 Waleteni nje watu ambao ni vipofu, hata kama wana macho, na viziwi, hata kama wana masikio.
הוציא עם עור ועינים יש וחרשים ואזנים למו׃
9 Mataifa yote yatakusanyika kwa pamoja na watu watakusanyika. Ni nani miongoni mwenu atakaye tamka na kutangaza kutumia mambo ya mwanzo? Waache walete mashahidi kuwashuhudia wao kama wako sahihi, waache wasikilize na kuthibitisha, 'kama ni kweli'.
כל הגוים נקבצו יחדו ויאספו לאמים מי בהם יגיד זאת וראשנות ישמיענו יתנו עדיהם ויצדקו וישמעו ויאמרו אמת׃
10 Ninyi ni mashahidi wangu, ametangaza Yahwe, ''na watumishi wangu niliowachagua, ili uweze kujua na kuniamini mimi, na kuelewa kwamba mimi ndiye. Kabla yangu hapana mungu mwingine aliyeumbwa, na wala hatatoke baada yangu.
אתם עדי נאם יהוה ועבדי אשר בחרתי למען תדעו ותאמינו לי ותבינו כי אני הוא לפני לא נוצר אל ואחרי לא יהיה׃
11 Mimi, Mimi Yahwe, na hakuna Mkombozi zaidi yangu.
אנכי אנכי יהוה ואין מבלעדי מושיע׃
12 Nimetangaza, nimeokoa, na kutangaza, na hakuna Mungu mwingine miongoni mwenu, Ninyi ni mashahidi wangu asema Yahwe, ''Mimi ni Mungu.
אנכי הגדתי והושעתי והשמעתי ואין בכם זר ואתם עדי נאם יהוה ואני אל׃
13 Kuanzia leo na kuendelea mimi ndiye, na hakuna hata mmoja atakayewakomboa kwenye mkono wangu. Nitafanya, na nani awezae kunizuia?''
גם מיום אני הוא ואין מידי מציל אפעל ומי ישיבנה׃
14 Yahwe asema hivi, Mkombozi wenu, yeye Mtakatifu wa Israeli: ''Kwa niaba yenu nimemtuma mjumbe kwenda Babeli na kuwaongoza wao wote chini kama watuhumiwa, kubadilisha kelele za furaha za watu wa Babeli' kuwa wimbo wa maombolezo.
כה אמר יהוה גאלכם קדוש ישראל למענכם שלחתי בבלה והורדתי בריחים כלם וכשדים באניות רנתם׃
15 Mimi ni Yahwe, niliye Mtakatifu, Muumbaji wa Israeli, Mfalme wenu.
אני יהוה קדושכם בורא ישראל מלככם׃
16 Yahwe asema hivi, Ni nani aliyefungua njia katika bahari, na njia katika maji yenye nguvu,
כה אמר יהוה הנותן בים דרך ובמים עזים נתיבה׃
17 ni nani anayeongoza gari na farasi, majeshi na jeshi kuu. Walianguka chini kwa pamoja; hawakunyanyuka tena; wamezimwa, kama utambi unaoungua.
המוציא רכב וסוס חיל ועזוז יחדו ישכבו בל יקומו דעכו כפשתה כבו׃
18 Msifikirie hayo mambo yaliyopita, wala kuyafikiria mambo ya zamani.
אל תזכרו ראשנות וקדמניות אל תתבננו׃
19 Tazama ninakaribia kufanya mambo mapya; sasa yanakaribia kutokea; Je humyajui haya? Nitafanya njia jangani na na mikondo ya maji katika jangwa
הנני עשה חדשה עתה תצמח הלוא תדעוה אף אשים במדבר דרך בישמון נהרות׃
20 Wanyama pori wa shambani wataniheshimu mimi, Mbweha na mbuni, kwa sababu ninatoa maji jangwani, na mito jangwani, ili watu wangu niliowachuga wapate kunjwa,
תכבדני חית השדה תנים ובנות יענה כי נתתי במדבר מים נהרות בישימן להשקות עמי בחירי׃
21 Watu hawa niliowaumba mwenyewe, kwamba wahesabu tena sifa zangu.
עם זו יצרתי לי תהלתי יספרו׃
22 Lakini hamjanita mimi, Yakobo; umechoka na mimi, Israeli.
ולא אתי קראת יעקב כי יגעת בי ישראל׃
23 Haujaniletea hata kondoo wako kama sadaka ya kuteketeza; na wala haujaniheshimu mimi kwa sadaka yako Sijakutumisha wewe kwa sadaka ya mazao, wala sijawachosha kwa sadaka yenu ya ubani.
לא הביאת לי שה עלתיך וזבחיך לא כבדתני לא העבדתיך במנחה ולא הוגעתיך בלבונה׃
24 Hamkuninunulia mimi manukato mazuri kwa fedha, hakumwagia mimi mafuta ya sadaka zenu; Lakini mnanichosha mimi na dhambi zenu na mnanichosha mimi kwa matendo yenu mabaya.
לא קנית לי בכסף קנה וחלב זבחיך לא הרויתני אך העבדתני בחטאותיך הוגעתני בעונתיך׃
25 Mimi, ndio, Mimi, ndiye niliyafaye maovu yenu kwa niaba yangu mmi mwenyewe; na Sitawaita na kuwakumbusha dhambi zenu tena.
אנכי אנכי הוא מחה פשעיך למעני וחטאתיך לא אזכר׃
26 Nikumbusheni mimi kilichotokea. Njooni tusemezane pamoja; leta hoja zako, ili kusudi uthibitishe kuwa hauna hatia.
הזכירני נשפטה יחד ספר אתה למען תצדק׃
27 Baba yako wa kwanza alitenda dhambi, na viongozi wenu walitenda dhambi dhidi yangu.
אביך הראשון חטא ומליציך פשעו בי׃
28 Hivyo basi Nitawatia unajisi viongozi watakatifu; Nitamkabidhi Yakobo kuwaharibu kabisa, na Israeli kulaani udhalilishaji.
ואחלל שרי קדש ואתנה לחרם יעקב וישראל לגדופים׃

< Isaya 43 >