< Isaya 39 >

1 Katika mda ule Merodaki mtoto wa Baladani, mfalme wa Babeli, alituma zawadi na barua kwa Hezekia; maana alisikia Hezekia alikuwa anaumwa na amepona.
בעת ההיא שלח מרדך בלאדן בן בלאדן מלך בבל ספרים ומנחה--אל חזקיהו וישמע כי חלה ויחזק
2 Hezekia alifurahishwa na hivi vitu; alimuonyesha mjumbe nyumba ya ghala la vitu vya thamani- vitu kama fedha, dhahabu, viungo, na mafuta ya thamani, ghala la kuwekea silaha zake, na vitu vyote vilivyopatikana kwenye stoo yake. Hapakuwa na kitu katika nyumba yake, wala ufalme wake wote, Hezekia hakuwaonyesha wao.
וישמח עליהם חזקיהו ויראם את בית נכתה את הכסף ואת הזהב ואת הבשמים ואת השמן הטוב ואת כל בית כליו ואת כל אשר נמצא באצרתיו לא היה דבר אשר לא הראם חזקיהו בביתו--ובכל ממשלתו
3 Basi Isaya nabii alikuja kwa mfalme Hezekia na kumuuliza, ''Je watu hawa wamekuambia nini? wametoka wapi?, ''Wamekuja kwangu kutoka mbali nchi ya Babeli.''
ויבא ישעיהו הנביא אל המלך חזקיהו ויאמר אליו מה אמרו האנשים האלה ומאין יבאו אליך ויאמר חזקיהו מארץ רחוקה באו אלי מבבל
4 Isaya akamuuliza je ni vitu gani walivyoviona katika nyumba yako? Hezekia akajibu, ''Wameona kila kitu katika nyumba nyangu. Hakuna kitu miongoni mwa vitu vyangu vya thamani ambavyo sijawaonyesha.''
ויאמר מה ראו בביתך ויאמר חזקיהו את כל אשר בביתי ראו--לא היה דבר אשר לא הראיתים באוצרתי
5 Basi Isaya akamwambia Hezekia, ''Sikiliza neno la Yahwe wa majeshi:
ויאמר ישעיהו אל חזקיהו שמע דבר יהוה צבאות
6 'Tazama siku inakaribia kuja pale kila kitu katika nyumba yako, vitu ambavyo mababu zako wamevihifadhi mbali mpaka mda huu wa sasa Vitapelekwa Babeli. Hakuna kitakachobakizwa, asema Yahwe.
הנה ימים באים ונשא כל אשר בביתך ואשר אצרו אבתיך עד היום הזה בבל לא יותר דבר אמר יהוה
7 Na watoto watazaliwa kutoka kwako, ambao wewe mwenyewe utawazaa- watachukuliwa mbali, na watakuwa matoashi katika jumba la mfalme wa Babeli.''
ומבניך אשר יצאו ממך אשר תוליד--יקחו והיו סריסים בהיכל מלך בבל
8 Basi Hezekia akamwambia Isaya, ''Neno la Yahwe alilolizunumza ni zuri.'' Maana alifikiria, ''Patakuwa na amani na utulivu katika siku zangu.''
ויאמר חזקיהו אל ישעיהו טוב דבר יהוה אשר דברת ויאמר כי יהיה שלום ואמת בימי

< Isaya 39 >