< Isaya 36 >

1 Katika mwaka wa kumi na nne wa mfalme Hezekia, Senacherebi, mfalme wa Asiria, alivamia miji yote ya Yuda na kuwakamata.
Katika mwaka wa kumi na nne wa utawala wa Mfalme Hezekia, Senakeribu mfalme wa Ashuru akaishambulia miji yote ya Yuda yenye ngome na kuiteka.
2 Halafu mfalme wa Asiria akamtuma kamanda mkuu na jeshi kubwa kutoka Lachishi mpaka Yerusalemu kwa mfalme Hezekia. Alipofika kwenye mfereji katika kisima cha juu, katika njia kuu na katika shamba la dobi na akasimama pale.
Kisha mfalme wa Ashuru akamtuma jemadari wa jeshi pamoja na jeshi kubwa kutoka Lakishi hadi kwa Mfalme Hezekia huko Yerusalemu. Jemadari wa jeshi akasimama kwenye mfereji wa Bwawa la Juu, lililojengwa katika barabara iendayo kwenye Uwanja wa Dobi.
3 Maofisa wa Israeli waliotumwa kuzungumza nao walikuwa ni Eliakimu mtoto wa Hilkia, kiongozi wa jumba, Shebna katibu wa mfalme, na Joa mtoto wa Asapha, anayeandika makubaliano ya serekali.
Eliakimu mwana wa Hilkia aliyekuwa msimamizi wa jumba la kifalme, Shebna aliyekuwa katibu, na Yoa mwana wa Asafu mwandishi wakamwendea.
4 Kamanda mkuu wa jeshi akawaambia wao, ''Mwambieni Hezekia kwamba mfalme mkuu, mfalme Asiria, asema, 'Nini chanzo cha ujasiri wako?
Jemadari wa jeshi akawaambia, “Mwambieni Hezekia, “‘Hili ndilo asemalo mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru: Ni wapi unapoweka hili tumaini lako?
5 Unaongea maneno yasiyo na maana tu, nasema kama kuna shauri na nguvu za vita. Sasa ni nani unayemuamini? na ni nani aliyekupa ujasiri wa kuniasi mimi.
Unasema mnayo mikakati na nguvu za kijeshi, lakini unasema maneno matupu tu. Je, wewe unamtegemea nani, hata ukaniasi mimi?
6 Tazama, umeweka imani yako Misri, maana banzi la mwanzi unalolitumia kama fimbo ya kutembelea, ikiwa mtu ataiegemea na kuishika kwenye mkono wake itamchoma. Hivyo ndovyo jinsi Farao mfalme wa Misri alivyo kwa yeyote anayemuamini.
Tazama sasa, unaitegemea Misri, fimbo ile ya mwanzi uliopasuka, ambayo huuchoma na kuujeruhi mkono wa mtu akiiegemea! Hivyo ndivyo alivyo Farao mfalme wa Misri, kwa wote wanaomtegemea.
7 Lakini ikiwa utasema nami, ''Tunamwamini Yahwe Mungu wetu,''Je sio yeye ambaye Hezekia ameondosha mahali palipoinuka na madhebau, asema kwa Yuda na Yerusalemu, ''Lazima tuabudu mbele ya madhebau hii katika Yerusalemu''?
Nawe kama ukiniambia, “Tunamtumainia Bwana Mungu wetu”: je, siyo yeye ambaye Hezekia aliondoa mahali pake pa juu pa kuabudia miungu na madhabahu zake, akiwaambia Yuda na Yerusalemu, “Ni lazima mwabudu mbele ya madhabahu haya”?
8 Hivyo sasa, nataka kukufanya wewe kuwa zawadi nzuri kwa Bwana mfalme Asiria. Nitakupa farasi elfu mbili, kama utaweza kuwatafutia dereva.
“‘Njooni sasa, fanyeni mapatano na bwana wangu, mfalme wa Ashuru: Nitakupa farasi elfu mbili, kama unaweza kuwapandisha waendesha farasi juu yao!
9 Ni kwa jinsi gani unaweza kumpinga moja kati ya nahodha aliye mdogo katika watumishi wa Bwana wangu? Mmeweka imani yenu Misri katika gari na farasi!
Utawezaje kumzuia hata afisa mmoja aliye mdogo kati ya maafisa wa bwana wangu, ijapo unategemea Misri kwa magari ya vita na wapanda farasi?
10 Halafu sasa, Je nimewezaje kusafiri mpaka hapa pasipo Yahwe kupigana dhidi ya nchi hii na kuhiaribu? Yahwe asema nami, Vamia nchi hii na uhiharibu.
Zaidi ya hayo, je, nimekuja kushambulia na kuangamiza nchi hii bila Bwana? Bwana mwenyewe ndiye aliniambia niishambulie nchi hii na kuiangamiza.’”
11 Halafu Eliakimu mtoto wa Hilkia, na Shebna na Joa asema kwa kamanda mkuu, Tafadhali zungumza na watu wako kwa lugha ya kiashuru, maana kiashuru tunakielewa. Usiongee na sisi kwa lugha kiyahudi katika masikio ya watu ambao wako ukutani.''
Ndipo Eliakimu, Shebna na Yoa wakamwambia yule jemadari wa jeshi, “Tafadhali zungumza na watumishi wako kwa lugha ya Kiaramu, kwa kuwa tunaifahamu. Usiseme nasi kwa Kiebrania watu walioko juu ya ukuta wakiwa wanasikia.”
12 Lakini kamanda mkuu akasema, ''Je bwana wenu ametuma kwa bwana wako na kuzungumza haya maneno? Je hajanituma kwa watu walio kaa kwenye ukuta, ili wale kinyesi chaao mwenyewe na kunywa mkojo waomwenyewe?
Lakini yule jemadari wa jeshi akajibu, “Je, bwana wangu amenituma kutoa ujumbe huu kwa bwana wenu na kwenu tu? Je, hakunituma pia kwa watu walioketi ukutani, ambao, kama ninyi, itawabidi kula mavi yao na kunywa mikojo yao wenyewe?”
13 Halafu kamanda mkuu akasimama na kupiga kelele kwa sauti kubwa kwa lugha ya kiyahudi, na akisema,
Kisha yule jemadari wa jeshi akasimama na kuita kwa lugha ya Kiebrania, akasema: “Sikieni maneno ya mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru!
14 ''Mfalme asema, ' Msimruhusu Hezekia awadanganye ninyi, maana hataweza kuwaokoa ninyi.
Hili ndilo asemalo mfalme: Msikubali Hezekia awadanganye. Hawezi kuwaokoa!
15 Msimruhusu Hezekia awafanye muumuamini Yahwe, Nawambieni Hakika Yahwe atatukomboa sisi; mjii huu hautachukuliwa na mfalme wa Asiria.''
Msikubali Hezekia awashawishi kumtumaini Bwana kwa kuwaambia, ‘Hakika Bwana atatuokoa. Mji huu hautaangukia mikononi mwa mfalme wa Ashuru.’
16 Msimsikilize Hezekia, maana hivi ndivyo mfalme wa Asiria anavyosema: 'Fanyeni amani na mimi na mje kwangu. Halafu kila mmoja wenu atakula kwenye mzabibu wake mwenyewe na tunda la mti wake mwenyewe, na kunjwa maji ya kisima chake mwenyewe.
“Msimsikilize Hezekia. Hili ndilo mfalme wa Ashuru asemalo: Fanyeni amani nami na mje kwangu. Kisha kila mmoja wenu atakula kutoka kwa mzabibu wake na mtini wake mwenyewe, na kunywa maji kutoka kisima chake mwenyewe,
17 Mtafanya hivi mpaka nije kuwachukua na kuwapeleka kwenye nchi kama ya kwenu. nchi ya mavuno na mvinyo mpya, nchi ya mkate na shamba.
mpaka nije nikawapeleke katika nchi iliyo kama nchi yenu wenyewe, nchi ya nafaka na divai mpya, nchi ya mkate na ya mashamba ya mizabibu.
18 Msimruhusu Hezekia awapotoshe nyie, akisema, Yahwe atatuokoa nyie; Je kuna miungu ya aina yeyote ya watu iliyowakomboa kutoka mikononi mwa mfalme wa Asiria?
“Msikubali Hezekia awapotoshe asemapo, ‘Bwana atatuokoa.’ Je, yuko mungu wa taifa lolote aliyewahi kuokoa nchi yake kutoka mkononi mwa mfalme wa Ashuru?
19 Wako wapi miungu wa Hamathi na Arpadi? Iko wapi miungu ya Sefarvaimu? Je wameikomboa Samaria kutoka kwenye nguvu zangu?
Iko wapi miungu ya Hamathi na ya Arpadi? Iko wapi miungu ya Sefarvaimu? Je, imeokoa Samaria kutoka mkononi mwangu?
20 Miongoni mwa miungu yote ya nchi hii, Je kuna miungu ya aina yeyote iliyoikomboa nchi yao kutoka kwenye nguvu yangu, ni kama Yahwe anaweza kuawokoa Yerusalemu kutoka kwenye nguvu yangu?''
Ni yupi miongoni mwa miungu yote ya nchi hizi ameweza kuokoa nchi yake mkononi mwangu? Inawezekanaje basi Bwana aiokoe Yerusalemu mkononi mwangu?”
21 Lakini watu wanabaki kimya na hawataki kujibu, maana amri ya mfalme ilikuwa, ''Msimjibu''.
Lakini wale watu wakakaa kimya, wala hawakujibu lolote, kwa kuwa mfalme alikuwa amewaamuru, “Msimjibu lolote.”
22 Halafu Eliakimu mtoto wa Hilkia, yeye aliye juu ya kaya, Shebna mwandishi, na Joa mtoto wa Asafu, na mtunza kumbukumbu, walikuja kwa Hezekia na nguo zilizotoboka na wakapeleka maneno ya kamanda mkuu.
Kisha Eliakimu mwana wa Hilkia msimamizi wa jumba la kifalme, Shebna katibu, na Yoa mwana wa Asafu, mwandishi wakamwendea Hezekia, nguo zao zikiwa zimeraruliwa, na kumwambia yale jemadari wa jeshi aliyoyasema.

< Isaya 36 >