< Isaya 35 >
1 Jangwa na Arabu watafurahia; na jangwa litafurahia na kuchanua. Kama waridi,
Jangwa na nchi kame vitafurahi; nyika itashangilia na kuchanua maua. Kama waridi,
2 Yatachanua kwa wingi na yatashangilia kwa furaha na nyimbo; litapewa utukufu wa Lebanoni, mapambo ya Karmeli na Sharoni; watauona utukufu wa Yahwe, mapambo ya Mungu wetu.
litachanua maua, litashangilia sana na kupaza sauti kwa furaha. Litapewa utukufu wa Lebanoni, fahari ya Karmeli na Sharoni; wataona utukufu wa Bwana, fahari ya Mungu wetu.
3 Itieni nguvu mikono iliyo dhaifu, na badala ya magoti yanayotingishika.
Itieni nguvu mikono iliyo dhaifu, yafanyeni imara magoti yaliyolegea,
4 Waambie wenye moyo wa uwoga, ''Wawe imara, wasiogope! Tazama, Mungu wako anakuja na kisasi, kwa ajili ya malipo ya Mungu. Atakuja na kutuokoa.''
waambieni wale wenye mioyo ya hofu, “Kuweni hodari, msiogope; tazama, Mungu wenu atakuja, pamoja na malipo ya Mungu, atakuja na kuwaokoa ninyi.”
5 Halafu macho ya vipofu yataona, na masikio ya viziwi yatasikia.
Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa na masikio ya viziwi yatazibuliwa.
6 Halafu kilema atarukaruka kama kulungu, na ulimi wa bubu utaimba, maana maji yatabubujika Araba, na mifereji jangwani.
Ndipo kilema atarukaruka kama kulungu, nao ulimi wa aliye bubu utapaza sauti kwa shangwe. Maji yatatiririka kwa kasi katika nyika, na vijito katika jangwa.
7 Mchanga ulioungua utakuwa kisima, na aridhi iliyo na kiu itakua chemchem; katika makazi mbweha, pale waliopokuwa wanaishi, kutakuwa na nyasi pamoja na mianzi.
Mchanga wa moto utakuwa bwawa la maji, ardhi yenye kiu itabubujika chemchemi. Maskani ya mbweha walikolala hapo awali patamea majani, matete na mafunjo.
8 Barabara kuu itaitwa Njia takatifu. Wasio safi hawatasifiri kwa kutumia njia hiyo. Lakini itakuwa kwa ajili ya mtu yeyote anayetembea juu yake. Hakuna mjinga atakayeipitia.
Nako kutakuwa na njia kuu, nayo itaitwa Njia ya Utakatifu. Wasio safi hawatapita juu yake; itakuwa ya wale watembeao katika Njia ile; yeye asafiriye juu yake, ajapokuwa mjinga, hatapotea.
9 Hakuna simba pale, wala mnyama mkali katika barabara hiyo; hawatakuwepo kabisa pale, lakini waliokombolewa watapita pale.
Huko hakutakuwepo na simba, wala mnyama mkali hatapita njia hiyo, wala hawatapatikana humo. Ila waliokombolewa tu ndio watakaopita huko,
10 Fidia ya Yahwe itarudi na itakuja kwa wimbo wa Sayuni, na furaha ya milele itakuwa katika vichwa vyao; furaha na shangwe vitawazidi wao; huzuni na magonjwa yataondoshwa mbali.
waliokombolewa na Bwana watarudi. Wataingia Sayuni wakiimba; furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao. Watapata furaha na shangwe; huzuni na majonzi vitakimbia.