< Isaya 32 >

1 Tazama, mfalme atatawala kwa haki, wakuu wataongoza kwa haki.
看哪,必有一王凭公义行政; 必有首领借公平掌权。
2 Kila mmoja atakuwa kama makazi kutoka kwenye upepo na kimbilio kutoka kwenye dhoruba, kama mifereji kwenye sehemu kavu, kama kivuli kwenye mwamba mkubwa katika nchi iliyochoka.
必有一人像避风所和避暴雨的隐密处, 又像河流在干旱之地, 像大磐石的影子在疲乏之地。
3 Halafu macho ya waie wanaoona hayataona giza, na masikio ya wale wanosikia yatasikia vizuri.
那能看的人,眼不再昏迷; 能听的人,耳必得听闻。
4 Wenye upele watafikiria kwa makini kwa uelewa wao, na wenye kigugumizi watazungumza dhahiri na kwa urahisi.
冒失人的心必明白知识; 结巴人的舌必说话通快。
5 Mjinga hataitwa tena muheshimiwa, wala muongo hataitwa mkuu.
愚顽人不再称为高明; 吝啬人不再称为大方。
6 Maana mjinga anazungumza ujinga, na moyo wake unapanga maovu na matendo ya wasiomcha Mungu, na anaongea mambo mabaya kuhusu Yahwe. Na anawafanya wenye njaa kuwa tupu na wenye kiu kukosa maji
因为愚顽人必说愚顽话, 心里想作罪孽, 惯行亵渎的事, 说错谬的话攻击耶和华, 使饥饿的人无食可吃, 使口渴的人无水可喝。
7 Njia ya muongo ni maovu. Anajua kubuni mipango mibaya ya kuwalagai masikini kwa uongo, na hata kama masikini atazungumza ukweli.
吝啬人所用的法子是恶的; 他图谋恶计, 用谎言毁灭谦卑人; 穷乏人讲公理的时候, 他也是这样行。
8 Lakini watu wa heshima wanapanga mipango ya kuheshimika; na kwa sabaubau ya matendo ya wenye heshima tuatasimama.
高明人却谋高明事, 在高明事上也必永存。
9 Nyanyukeni juu, enyi wanawake mlio wepesi, na sikilizeni sauti yangu; enyi mabinti msiowangalifu, nisikilizeni mimi.
安逸的妇女啊,起来听我的声音! 无虑的女子啊,侧耳听我的言语!
10 Maana kwa mda mfupi zaidi ya mwaka ujasiri wenu utavunjika, nyie wanawake msiojali, maana mavuno ya zabibu yatakwama, mavuno hayatakuwepo.
无虑的女子啊,再过一年多,必受骚扰; 因为无葡萄可摘, 无果子可收。
11 Tetemekeni, enyi wanawake, mliowadhaifu; taabikeni enyi msikuwa wangalifu; ondoeni nguo zenu nzuri mbaki wazi;
安逸的妇女啊,要战兢; 无虑的女子啊,要受骚扰。 脱去衣服,赤着身体, 腰束麻布。
12 Vaeni nguo za magunia katika viuno vyenu. Ole watakaojichukulia mashamba mazuri, kwa mzabibu ulio zaa sana.
她们必为美好的田地 和多结果的葡萄树,捶胸哀哭。
13 Kwenye aridhi ya watu wangu kutamea miiba na mbigiri, hata juu ya nyumba za furaha na mji ulio na shangwe.
荆棘蒺藜必长在我百姓的地上, 又长在欢乐的城中和一切快乐的房屋上。
14 Maana jumba litaachwa, mji uliosongamana utakuwa faragha; kilima na mnara vitakuwa mapango daima, furaha ya punda, malisho ya mifugo;
因为宫殿必被撇下, 多民的城必被离弃; 山冈望楼永为洞穴, 作野驴所喜乐的, 为羊群的草场。
15 mpaka roho itushukie sisi kutoka juu, na jangwa litakuwa shamba linalozaa, na shamba linalozaa litachukuliwa kama msitu.
等到圣灵从上浇灌我们, 旷野就变为肥田, 肥田看如树林。
16 Wenye haki wataishi jangwani; na wenye haki wataishi katika shamba linalozaa matunda.
那时,公平要居在旷野; 公义要居在肥田。
17 Kazi ya mwenye haki itakuwa ni ya amani; na matokeo ya wenye haki, ni utulivu na kujiamini daima.
公义的果效必是平安; 公义的效验必是平稳,直到永远。
18 Watu wangu wataishi katika makao ya amani, na katika nyumba salama na mahali tulivu pa kupumzikia.
我的百姓必住在平安的居所, 安稳的住处,平静的安歇所。
19 Lakini hata kama ni mvua ya mawe na msitu umeharibiwa, na mji umeteketezwa,
(但要降冰雹打倒树林; 城必全然拆平。)
20 yule ambae anaye panda pembezoni mwa mifereji atabarikiwa, na yule atakaye wapeleka ng'ombe na punda kuchunga.
你们在各水边撒种、 牧放牛驴的有福了!

< Isaya 32 >