< Isaya 28 >

1 Ole kwa taji la kiburi ambalo huvaliwa na kila mlevi wa Efraimu, na ua linalofifia la utukufu wa uzuri wake, ua lililowekwa kichwani mwa bonde linalostawi na hao wanoshindwa na nvinyo!
Ole kwa lile taji la maua, kiburi cha walevi wa Efraimu, kwa ua linalosinyaa, uzuri wa utukufu wake, uliowekwa kwenye kichwa cha bonde lenye rutuba: kwa ule mji, kiburi cha wale walioshushwa na mvinyo!
2 Tazama Bwana anamtuma aliye hodari na nguvu; kama dhoruba ya mvua ya mawe na upepo mkali unaoharibu, na atatupa kila taji la ua chini kwenye aridhi.
Tazama, Bwana anaye mmoja aliye na uwezo na nguvu. Kama dhoruba ya mvua ya mawe na upepo uharibuo, kama mvua inyeshayo kwa nguvu na mafuriko yashukayo, atakiangusha chini kwa nguvu.
3 Taji ya kiburi ya walevi wa Efraimu lililoko chini ya paa.
Lile taji la maua, kiburi cha walevi cha Efraimu, kitakanyagwa chini ya nyayo.
4 Ua lililofifia la utukufu wa uzuri wake, juu ya kichwa cha bonde la utajiri, itakuwa kama tunda lililoiva mtini kabla ya maji yake, kwamba, wakati mtu anapoliona tunda, wakati likiwa bado mikononi mwake, analigugumia chini.
Lile ua linalosinyaa, uzuri wa utukufu wake, uliowekwa kwenye kichwa cha bonde lenye rutuba, litakuwa kama tini iliyoiva kabla ya mavuno: mara mtu aionapo, huichuma na kuila.
5 Katika siku hiyo Yahwe wa majeshi atakuwa taji nzuri na taji ya uzuri kwa watu wake waliobakia,
Katika siku ile, Bwana Mwenye Nguvu Zote atakuwa taji la utukufu, taji zuri la maua kwa mabaki ya watu wake.
6 roho ya haki kwa yeye aliyekaa katika hukumu, nguvu kwa wale waliobadilisha adui zao katika malango yao.
Atakuwa roho ya haki kwa yeye aketiye katika kiti cha hukumu, chanzo cha nguvu kwa wale wazuiao vita langoni.
7 Lakini wale wanaoyumbayumba kwa ajili ya mvinyo, na wanojikongoja kwa ajili ya pombe kali. Kuhani na nabii watayumbayuma kwa ajili ya pombe kali, na watamezwa na mvinjo. Watajikongoja kwa ajili ya pombe kali, Kujikongoja katika maono na kuyumbayuma katika maamuzi.
Hawa pia wanapepesuka kwa sababu ya mvinyo, wanayumbayumba kwa sababu ya kileo: Makuhani na manabii wanapepesuka kwa sababu ya kileo, wanachanganyikiwa kwa sababu ya mvinyo; wanapepesuka wanapoona maono, wanajikwaa wanapotoa maamuzi.
8 Hakika, meza zote zimejaa matapishi. Hivyo basi hakuna sehemu iliyosafi.
Meza zote zimejawa na matapishi wala hakuna sehemu hata ndogo isiyokuwa na uchafu.
9 Ni nani atakaye tufundisha maarifa, na nani atayetuelezea ujumbe? Kwa walioachishwa maziwa au kwa wanonyonya?
“Yeye anajaribu kumfundisha nani? Yeye anamwelezea nani ujumbe wake? Je, ni kwa watoto walioachishwa kunyonya? Je, ni wale ambao ndipo tu wametolewa matitini?
10 Maana ni amri juu ya amri, utawala juu ya utawala; na hapa kidogo na pale kidogo.
Kwa maana ni: Amri juu ya amri, amri juu ya amri, kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; hapa kidogo, kule kidogo.”
11 Kweli, kwa mdomo wa dharau na lugha za kigeni atazungumza na watu wake.
Sawa kabisa, kwa midomo migeni na kwa lugha ngeni, Mungu atasema na watu hawa,
12 Wakati uliopita aliwambia, '''Hawa ni wengine, wape punziko walio choka; maana huku ni kujifurahisha,'' lakini hawakusikiliza.
wale ambao aliwaambia, “Hapa ni mahali pa kupumzika, waliochoka na wapumzike,” na, “Hapa ni mahali pa mapumziko,” lakini hawakutaka kusikiliza.
13 Hivyo basi neno la Yahwe litakuwa kwao amri juu ya amri, amri juu ya amri, utawala juu ya utawala; na kidogo hapa na kidogo pale, ili waende na kuanguka nyuma, na kuvunjwa, kutegwa, na kukamatwa.
Hivyo basi, neno la Bwana kwao litakuwa: Amri juu ya amri, amri juu ya amri, kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni, hapa kidogo, kule kidogo: ili waende na kuanguka chali, wakijeruhiwa, wakinaswa na kukamatwa.
14 Hivyo basi sikiliza neno la Yahwe, yeyote afaanyae maskhara, wewe unaowaongoza watu hawa ambao wako Yerusalemu.
Kwa hiyo sikieni neno la Bwana, enyi watu wenye dharau mnaotawala watu hawa wa Yerusalemu.
15 Hii itatokea kwa sababu umesema, '' Tumefannya magano na kifo; maana kuzimu wameyafikia makubaliano. Hivyo basi hukumu itakapopitishwa kwa wingi, haitatufika sisi, maana tumefanya maneno ya uongo kuwa kimbilio letu, na uongo kuwa makazi yetu. (Sheol h7585)
Ninyi mnajisifu, “Tumefanya agano na mauti, tumefanya mapatano na kuzimu. Wakati pigo lifurikalo litakapopita, haliwezi kutugusa sisi, kwa kuwa tumefanya uongo kuwa kimbilio letu na miungu ya uongo kuwa mahali petu pa kujificha.” (Sheol h7585)
16 Hivyo basi Bwana Yahwe asema hivi, ''Ona: Nitaiwekea Sayuni msingi wa mawe, jiwe la kujaribu, jiwe la pembeni lenye samani, msingi wa uhakika. Na yeyote atayeuamini ataaibika kamwe.
Kwa hiyo hivi ndivyo Bwana Mwenyezi asemavyo: “Tazama, ninaweka jiwe katika Sayuni, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembeni la thamani kwa ajili ya msingi thabiti. Yeye atumainiye kamwe hatatiwa hofu.
17 Nitafanya haki kuwa fimbo ya usawa, na kuwa haki pima maji. Atasafishia mbali kimbilio la waongo, na mafuriko yatajaa balaa katika mahali pa siri.
Nitaifanya haki kuwa kamba ya kupimia na uadilifu kuwa timazi; mvua ya mawe itafagia kimbilio lenu, huo uongo, nayo maji yatafurikia mahali penu pa kujificha.
18 Agano lako na kifo litafutwa, na makubaliano yako na kuzimu hayatasimama. Pindi mafuriko makali yatapta, yatawazomba njie. (Sheol h7585)
Agano lenu na kifo litabatilishwa, patano lenu na kuzimu halitasimama. Wakati pigo lifurikalo litakapowakumba, litawaangusha chini. (Sheol h7585)
19 Maana pindi yatakopita, yatawazomba nyie yatapita asubuhi na asubuhi, na yatapita tena mchana na usiku utafika. Pale ujumbe utakapofika utasababisha hofu.
Kila mara lijapo litawachukua, asubuhi baada ya asubuhi, wakati wa mchana na wakati wa usiku, litawakumba tangu mwanzo hadi mwisho.” Kuuelewa ujumbe huu utaleta hofu tupu.
20 Maana kitanda ni kifupi kwa mtu kunyoosha mkono wake nje, na blangeti ni jembamba kwa yeye kujizungushia ndani''
Kitanda ni kifupi mno kujinyoosha juu yake, nguo ya kujifunikia ni nyembamba mno mtu hawezi kujifunikia.
21 Yahwe atanyanyuka kama mlima Perazimu; Atawahimiza yeye mwenye kufanya kazi yake katika bonde la Gibeoni, kazi ya ajabu, na kufanya matendo ya ajabu.
Bwana atainuka kama alivyofanya kwenye Mlima Perasimu, ataghadhibika kama alivyofanya katika Bonde la Gibeoni: ili kufanya kazi yake, kazi yake ya ajabu, ili kutimiza kazi yake, kazi yake ngeni.
22 Hivyo sasa msifanye maskhara, dhamana yako itakazwa, Nimesikia kutoka kwa Bwana, Yahwe wa majeshi, amri ya kuiharibu nchi.
Sasa acheni dharau zenu, la sivyo minyororo yenu itakuwa mizito zaidi. Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, ameniambia habari za maangamizi yaliyoamriwa dhidi ya nchi yote.
23 Kuwa tayari na sikiliza saut yangu; kuwa makini na sikiliza maneno yangu.
Sikilizeni msikie sauti yangu, tegeni masikio na msikie niyasemayo.
24 Je mkulima anayelima siku zote kwa ajili ya kupanda, analima tu kwenye aridhi? Je anaendelea kulima shamba lake pasipo kupanda?
Wakati mkulima alimapo ili apande, je, hulima siku zote? Je, huendelea kubomoa ardhi na kusawazisha udongo?
25 Pindi anapolindaa shamba lake, Je hatawanji jira ya mbegu, anapanda jira, anaweka ngano katika mstari, shairi katika mahali pake, na yameandikw sehemu mbili?
Akiisha kusawazisha shamba, je, hatapanyi mbegu za bizari na kutawanya jira? Je, hapandi ngano katika sehemu yake, shayiri katika eneo lake, na nafaka nyingine katika shamba lake?
26 Mungu wake amemuelekeza; anamfuundisha yeye kwa busara.
Mungu wake humwelekeza na kumfundisha njia iliyo sahihi.
27 Zaidi ya hayo, jira zile hazipuruliwi kwa chombo kikali; wala gurudumu la kukatia linalozunguka juu ya jira; lakini jira linapigwa kwa fimbo, na jira kwa fimbo.
Iliki haipurwi kwa nyundo, wala gurudumu la gari halivingirishwi juu ya jira; iliki hupurwa kwa fimbo, na jira kwa ufito.
28 Nafaka ni mwanzo mkate lakini ni laini sana, japo gurudumu la gari lake na farasi wamezitawanya, na farasi wake hawajaiponda ponda.
Nafaka lazima isagwe ili kutengeneza mkate, kwa hiyo mtu haendelei kuipura daima. Ingawa huendesha magurudumu ya gari lake la kupuria juu yake, farasi wake hawasagi.
29 Haya yanatoka kwa Yahwe wa majeshi, yeye aliye mshauri wa ajabu na na mwenye ubara wa hekima.
Haya yote pia hutoka kwa Bwana Mwenye Nguvu Zote, mwenye mashauri ya ajabu, na anayepita wote kwa hekima.

< Isaya 28 >