< Isaya 2 >

1 Vitu ambavyo Isaya mtoto Amozi alivijua katika maono, kuhusu Yuda na Yerusalemu.
Hili ndilo aliloliona Isaya mwana wa Amozi kuhusu Yuda na Yerusalemu:
2 Na itakuwa katika siku za mwisho, ule mlima wa nyumba ya Yahwe itaanzishwa kama mlima mrefu zaidi, na utanyanyuliwa juu ya vilima, na mataifa yote yatakusanyika pale.
Katika siku za mwisho mlima wa Hekalu la Bwana utaimarishwa kama mlima mkuu miongoni mwa milima yote, utainuliwa juu ya vilima, na mataifa yote yatamiminika huko.
3 Watu wengi watakuja na kusema, ''Njooni, twendeni juu ya mlima wa Yahwe, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo, kwa hiyo anaweza kutufundisha baadhi ya njia zake na tunaweza kutembea katika njia zake.'' Nje ya Sayuni itaenda sheria na neno la Yahwe litatoka Yerualemu.
Mataifa mengi yatakuja na kusema, “Njooni, twendeni mlimani mwa Bwana, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo. Atatufundisha njia zake, ili tuweze kuenenda katika mapito yake.” Sheria itatoka Sayuni, neno la Bwana litatoka Yerusalemu.
4 Atahukumu kati ya mataifa na atatoa maamuzi kwa watu wote; watayapiga nyungo mapanga yao kuwa majembe, na mikiku yao kama ya kukatia ndoano; taifa halitanyanyua upanga juu ya taifa lingine, na wala hawata jiandaa kwa vita tena.
Atahukumu kati ya mataifa na ataamua migogoro ya mataifa mengi. Watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao kuwa miundu ya kukata matawi. Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa jingine, wala hawatajifunza vita tena.
5 Nyumba ya Yakobo, njooni, na tutembee katika mwanga wa Yahwe.
Njooni, enyi nyumba ya Yakobo, tutembeeni katika nuru ya Bwana.
6 Kwa maana mmewatekeleza watu wenu, nyumba ya Yakobo, wamejazwa na desturi kutoka mashariki na dalili kutokea kama mfilisti, na watasalimiana kwa mikono na wana wa wageni.
Umewatelekeza watu wako, nyumba ya Yakobo. Wamejaa ushirikina utokao Mashariki, wanapiga ramli kama Wafilisti na wanashikana mikono na wapagani.
7 Nchi yao imejaa fedha na dhahabu, na hakuna mipaka katika utajiri wao; nchi yao pia imejaa farasi, wala hakuna mipika ya magari.
Nchi yao imejaa fedha na dhahabu, hakuna mwisho wa hazina zao. Nchi yao imejaa farasi, hakuna mwisho wa magari yao.
8 Nchi yao pia imejaa sanamu; wanaabu utengenezaji wa mikono yao wenyewe, vitu aambavyo vidole vyao vimetengeneza.
Nchi yao imejaa sanamu, wanasujudia kazi za mikono yao, vitu vile vidole vyao vimevitengeneza.
9 Watu watainama chini, na kila mmoja atanguka chini; hivyo basi msiwanyanyue juu.
Kwa hiyo mwanadamu atashushwa na binadamu atanyenyekezwa: usiwasamehe.
10 Nendeni maeneo yenye miamba na mjifiche kwenye aridhi kwa hofu ya Yahwe na kwa utukufu wa enzi yake.
Ingieni kwenye miamba, jificheni ardhini kutokana na utisho wa Bwana na utukufu wa enzi yake!
11 Mtu anaye tazama kwa kujivuna atashushw chini, na kiburi cha watu kitashushwa chini, na Yahwe mwenyewe atainuliwa siku hiyo.
Macho ya mtu mwenye majivuno yatanyenyekezwa na kiburi cha wanadamu kitashushwa, Bwana peke yake ndiye atakayetukuzwa siku hiyo.
12 Maana kutakuwa na siku ya Yahwe wa majeshi juu ya yeyote anayejigamba na kujiinua juu, na dhidi ya yeyote mwenye kiburi na atashushwa chini-
Bwana Mwenye Nguvu Zote anayo siku aliyoiweka akiba kwa wote wenye kujivuna na wenye kiburi, kwa wote wanaojikweza (nao watanyenyekezwa),
13 na dhidi ya mierezi ya Lebanoni iliyo juu na kupandishwa juu, na dhidi ya mialoni ya Bashani.
kwa mierezi yote ya Lebanoni iliyo mirefu sana, na mialoni yote ya Bashani,
14 Siku hiyo ya Yahwe wa majeshi itakuwa dhidi ya milima yote mirefu, na dhidi ya vilima vyote vilivyonyanyuliwa juu,
kwa milima yote mirefu na vilima vyote vilivyoinuka,
15 na dhidi ya minara mirefu, na dhidi ya kila ukutaunaojitokeza,
kwa kila mnara ulio mrefu sana na kila ukuta wenye ngome,
16 na dhidi ya merikebu zote za Tarshishi, na dhidi ya vyombo vizuri vya meli.
kwa kila meli ya biashara, na kila chombo cha baharini cha fahari.
17 Kiburi cha mwanaume kitashushwa chini, na kiburi cha wanaume kitaanguka; Yahwe mwenyewe atainuliwa siku hiyo.
Majivuno ya mwanadamu yatashushwa, na kiburi cha wanadamu kitanyenyekezwa, Bwana peke yake ndiye atatukuzwa siku hiyo,
18 Sanamu zote zitaondolewa.
nazo sanamu zitatoweka kabisa.
19 Wanaume wataingia kwenye mapango ya miamba na mashimo ya aridhi, kwa hofu ya Yahwe, na kwa utukufu wa enzi yake, atakapo nyanyuka na kuitisha nchi.
Watu watakimbilia kwenye mapango ndani ya miamba, na kwenye mahandaki ardhini kutokana na utisho wa Bwana na utukufu wa enzi yake, ainukapo kuitikisa dunia.
20 Siku hiyo watu watatupa sanamu zao za fedha na dhahabu ambazo wametengeneza wenyewe kwa ajili ya kuabudia - watazitupa mbali kwa fuko na popo.
Siku ile, watu watawatupia panya na popo sanamu zao za fedha na za dhahabu, walizozitengeneza ili waziabudu.
21 Watu wataingia kwenye miamba kupitia mwanya itakuwa miamba chakavu, kwa hofu ya Yahwe na utukufu wa enzi yake,
Watakimbilia kwenye mapango miambani na kwenye nyufa za miamba kutokana na utisho wa Bwana na utukufu wa enzi yake, ainukapo kuitikisa dunia.
22 usimwaminia mtu, ambae pumzi yake inatokea katika pua yake, ni kwa kiasi gan?
Acheni kumtumainia mwanadamu, ambaye hana kitu ila pumzi katika pua zake. Yeye ana thamani gani?

< Isaya 2 >