< Isaya 14 >

1 Yahwe atakuwa na huruma juu ya Yakobo; atamchagua tena Israeli na kumrudisha tena kwenye nchi yake. Wageni wataungana nao na wataambatana wenyewe na nyumba ya Yakobo.
Bwana atamhurumia Yakobo, atamchagua Israeli tena, na kuwakalisha katika nchi yao wenyewe. Wageni wataungana nao na kujiunga na nyumba ya Yakobo.
2 Mataifa yataletwa katika maeneo yao wenyewe. Ndipo nyumba ya Israeli itawachukwa katika nchi ya Yahwe kwa watumishi wa kiume na wakike. Watachukuwa wafungwa wale waliokamatwa, na watawaongoza wale waliokuwa wanawanyanyasa.
Mataifa watawachukua na kuwaleta mahali pao wenyewe. Nayo nyumba ya Israeli itamiliki mataifa kama watumishi na wajakazi katika nchi ya Bwana. Watawafanya watekaji wao kuwa mateka, na kutawala juu ya wale waliowaonea.
3 Siku hiyo Yahwe atatoa pumziko kutoka kwenye mateso na maumivu, na kutoka kwenye kazi ngumu ambayo waliitajika kuzifanya,
Katika siku Bwana atakapokuondolea mateso, udhia na utumwa wa kikatili,
4 mtaimba hii kauli wimbo juu ya mfalme wa Babeli, ''Ni kwa jinsi gani wayanyasaji wamefika mwisho, kiburi cha hasira kimekwisha!
utaichukua dhihaka hii dhidi ya mfalme wa Babeli: Tazama jinsi mtesi alivyofikia mwisho! Tazama jinsi ghadhabu yake kali ilivyokoma!
5 Yahwe amevunja wafanyakazi waovu, fimbo ya hao viongozi,
Bwana amevunja fimbo ya mwovu, fimbo ya utawala ya watawala,
6 inayowapeleka watu kwenye laana na mapigo yasiyopimika, wanoongoza taifa kwa hasira,
ambayo kwa hasira waliyapiga mataifa kwa mapigo yasiyo na kikomo, nao kwa ghadhabu kali waliwatiisha mataifa kwa jeuri pasipo huruma.
7 yote iko katika punziko na utulivu; wmeanza kusherekea kwa kiimba.
Nchi zote ziko kwenye mapumziko na kwenye amani, wanabubujika kwa kuimba.
8 Hata mti wa mseprasi inafuhaia pamoja mierezi ya Lebanoni; inasema, Tangu ulipoweka chini, hakuna mkata kuni aliyekuja kutungusha sisi,
Hata misunobari na mierezi ya Lebanoni inashangilia mbele yako na kusema, “Basi kwa sababu umeangushwa chini, hakuna mkata miti atakayekuja kutukata.”
9 Kuzimu haina hamu kwa ajili yako unaye enda pale. Watafufuka waliokufa kwa ajili yako, wafalme wote wa dunia, wafanje watoke katika viti vyao vya enzi, wafalme wote wa mataifa. (Sheol h7585)
Kuzimu kote kumetaharuki kukulaki unapokuja, kunaamsha roho za waliokufa ili kukupokea, wote waliokuwa viongozi katika ulimwengu, kunawafanya wainuke kwenye viti vyao vya kifalme: wale wote waliokuwa wafalme juu ya mataifa. (Sheol h7585)
10 Watazungumza na kukuambia wewe, 'umekuwa dhaifu kama sisi.
Wote wataitikia, watakuambia, “Wewe pia umekuwa dhaifu, kama sisi tulivyo; wewe umekuwa kama sisi.”
11 Kiburi chako kimeshushwa kuzimu na sauti kifaa cha kamba yako. Buu wameongezeka chini yako na vijidudu vinakufunika wewe.' (Sheol h7585)
Majivuno yako yote yameshushwa mpaka kuzimu, pamoja na kelele ya vinubi vyako, mafunza yametanda chini yako, na minyoo imekufunika. (Sheol h7585)
12 Kwa jinsi gani ulivyoanguka kutoka mbinguni, nyota ya siku, jua la asubuhi! ni kwa jinsi gani mlivyoshushwa chini, umeyashinda mataifa!
Tazama jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, ewe nyota ya asubuhi, mwana wa mapambazuko! Umetupwa chini duniani, wewe uliyepata kuangusha mataifa!
13 Unasema katika moyo wako, ' Nitapaa kutoka juu mbinguni, nitanyanyua enzi yangu juu ya nyota za Mungu, na nitakaa kwenye mlima wa kukusanyikia, kwa mbali kufika kaskazini.
Ulisema moyoni mwako, “Nitapanda juu hadi mbinguni, nitakiinua kiti changu cha enzi juu ya nyota za Mungu, nitaketi nimetawazwa juu ya mlima wa kusanyiko, kwenye vimo vya juu sana vya Mlima Mtakatifu.
14 Nitapaa juu umbali wa mawingu; Nitalifanya mimi mwenyewe kama Mungu aliye juu zaidi.'
Nitapaa juu kupita mawingu, nitajifanya kama Yeye Aliye Juu Sana.”
15 Lakini kwa sasa umeshushwa chini kuzimu, kwenye kina cha shimo. (Sheol h7585)
Lakini umeshushwa chini hadi kuzimu, hadi kwenye vina vya shimo. (Sheol h7585)
16 Wale wanaokuona watakuangalia wewe, watakuangalia sana. Watasema, Je ni huyu mtu aliyefanya dunia itetemeke, nani aliyetingisha falme,
Wale wanaokuona wanakukazia macho, wanatafakari hatima yako: “Je, huyu ndiye yule aliyetikisa dunia na kufanya falme zitetemeke,
17 ni nani aliyefanya dunia kama jangwa, ni nani aliyeharibu miji yake, na hataki kuwachia wafungwa waende nyumbani?'
yule aliyeifanya dunia kuwa jangwa, aliyeipindua miji yake, na ambaye hakuwaachia mateka wake waende nyumbani?”
18 Wafalme wote wamataifa, wote kwa pamoja wamelala chini kwa heshima, kila mtu kwa kaburi lake.
Wafalme wote wa mataifa wamelala kwa heshima kila mmoja katika kaburi lake.
19 Lakini umetupwa nje ya kaburi lako kama tawi lilivyotupwa mbali. Maiti imekufunika kama vazi, na wale wanaochomwa kwa upanga, nani wale washukao mpaka misingi ya shimo.
Lakini wewe umetupwa nje ya kaburi lako kama tawi lililokataliwa, umefunikwa na waliouawa pamoja na wale waliochomwa kwa upanga, wale washukao mpaka kwenye mawe ya shimo. Kama mzoga uliokanyagwa chini ya nyayo,
20 Hautaunganishwa pamoja katika mazishi, kwa sababu umeiharibu nchi yako na kuuwa watu wako. Watoto wa watenda maovu hawatatajwa tena.''
Hutajumuika nao kwenye mazishi, kwa kuwa umeharibu nchi yako na kuwaua watu wako. Mzao wa mwovu hatatajwa tena kamwe.
21 Anda machinjio kwa ajili ya watoto wake, kwa sababu ya uovu wa mababu zao, hivyo basi hawatanyanyuka juu na na kuimiliki aridhi ya nchi iliyojaa miji ya dunia yote.''
Andaa mahali pa kuwachinjia wanawe kwa ajili ya dhambi za baba zao, wasije wakainuka ili kuirithi nchi na kuijaza dunia kwa miji yao.
22 Nitapanda juu yao''- hili ni tamko la Yahwe wa majeshi. Nitang'oa jina katika Babeli, uzao, na ukoo''- hili ndilo tamko la Yahwe.
Bwana Mwenye Nguvu Zote asema, “Nitainuka dhidi yao, nitalikatilia mbali jina lake kutoka Babeli pamoja na watu wake walionusurika, watoto wake na wazao wake,” asema Bwana.
23 Tena nitaifanya nchi hiyo kuwa makao ya bundi, dimbwi la maji, nanitawafagia kwa mfagio wa uharibifu''- hili ni tamko la Yahwe wa majeshi.
“Nitaifanya kuwa mahali pa bundi, na kuwa nchi ya matope; nitaifagia kwa ufagio wa maangamizi,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.
24 Yahwe wa majeshi ameapa, ''Hakika, kama nilivyodhamiria, itakuwa kama ilivyo; na kama nilivyo kusudia itakuwa:
Bwana Mwenye Nguvu Zote ameapa, “Hakika, kama vile nilivyopanga, ndivyo itakavyokuwa, nami kama nilivyokusudia, ndivyo itakavyosimama.
25 Nitawavunja Waasiria kwa mikono yangu, na kukanyaga milima kwa miguu yangu mwenyewe. Hivyo nira yake itanyanyuliwa juu yao na mzigo juu ya mabega yao.''
Nitamponda Mwashuru katika nchi yangu, juu ya milima yangu nitawakanyagia chini. Nira yake itaondolewa kutoka kwa watu wangu, nao mzigo wake utaondolewa kutoka mabegani mwao.”
26 Huu ni mpango uliokusudiwa katika nchi yote, na huu ndio mkono ulionyanyuliwa juu ya mataifa.
Huu ndio mpango uliokusudiwa kwa ajili ya ulimwengu wote, huu ni mkono ulionyooshwa juu ya mataifa yote.
27 Kwa maana Yahwe wa majeshi amepanga hivi; ni nani atakayemzia yeye? Mkono wake umenyanyuliwa juu, ni nani atakajemrudisha nyuma?
Kwa kuwa Bwana Mwenye Nguvu Zote amekusudia, ni nani awezaye kumzuia? Mkono wake umenyooshwa, ni nani awezaye kuurudisha?
28 Katika miaka ambayo mfalme Ahazi alipokufa, hili ndio tamko lilokuja:
Neno hili lilikuja mwaka ule Mfalme Ahazi alipofariki:
29 Msishangilie, enyi wafilisti wote, kwamba fimbo ya kukupigia wewe imevunjika. Maana katika njia ya nyoka atatoka fira, na watoto wake watakuwa moto nyoka wanaopaa.
Msifurahi, enyi Wafilisti wote, kwamba fimbo iliyowapiga imevunjika; kutoka mzizi wa huyo nyoka atachipuka nyoka mwenye sumu kali, uzao wake utakuwa joka lirukalo, lenye sumu kali.
30 Na mtoto wa kwanza wa maskini watachunga kondoo wao kwenye malisho yangu, na wahitaji watalala chini salama. Nitaiuwa mizizi yenu kwa njaa ambayo atawauwa wakazi wenu wote.
Maskini kuliko maskini wote watapata malisho, nao wahitaji watalala salama. Lakini mzizi wako nitauangamiza kwa njaa, nayo njaa itawaua walionusurika.
31 Omboleza, ewe lang, lia, ewe mji; ninyi nyote mtayeyukia mbali, Ufilisti. Maana kutoka kaskazini limetoka wingu la moshi, na hakuna hata mmoja atakaye odoka kwenye nafasi yake.
Piga yowe, ee lango! Bweka, ee mji! Yeyukeni, enyi Wafilisti wote! Wingu la moshi linakuja toka kaskazini, wala hakuna atakayechelewa katika safu zake.
32 Ni kivipi mtu mmoja atamjibu mjumbe wa taifa? Kwamba Yahwe ameipata Sayuni, na ndani yake walionewa watatafuta kimbilio.
Ni jibu gani litakalotolewa kwa wajumbe wa taifa hilo? “Bwana ameifanya imara Sayuni, nako ndani yake watu wake walioonewa watapata kimbilio.”

< Isaya 14 >