< Isaya 10 >
1 Ole wao watimizao sheria zisizo za haki na waandikao sheria zisizo na haki.
2 Wanawanyima wahitaji haki yao, wanawaibia watu wangu walio masikini haki zao, wajane mateka wao, na kuwafanya waliofiwa na baba zao mawindo yao!
3 Hutafanya nini siku ya hukumu pale siku ya uaribifu itakapokuja kutoka mbali, utakimbilia msaada kwa nani? na utauacha utajiri wako wapi?
4 Hakuna kitakachobaki, utaota miongoni mwa wafungwa au kuanguka miongoni mwa wauwaji. Katika mambo yote haya, hasira yake haijapungua; badala yake mkono wake ameunjoosha hata sasa.
5 Ole kwa watu wa Asiria klabu ya asira yangu, fimbo ya asira yangu!
6 Nimemtuma juu ya taifa lenye kiburi na juu ya watu waliobeba uwingi wa hasira. Ninaamuru chukua nyara, chukua mawindo, na kuwakanyaga wao kama matope mitaani.
7 Lakini hichi sicho alichomaanisha, wala sivyo afikiriavyo. Maana katika moyo wake ni kuharibu na kuondoa mataifa.
8 Maana amesema, '' wakuu wote sio wafalme?
9 Je? kalno si kama Karkemish? Je Hamathi si kama Arpadi? Je Samaria si kama Demeski?
10 Kama mikono yangu imeshinda falme za ibada ya sanamu, ikiwa sanamu zao za kuchonga ni bora kuliko sanamu za Yerusalemu
11 na Kama nilivyofanya kule Samaria na sanamu zake zisizo na maana, je sitaweza kufanya hivyo Yerusalemu na sanamu zake?''
12 Pindi ambapo Bwana alipoimaliza kazi kwenye mlima Sayuni na juu ya Yerusalemu, nitayaadhibu maneno ya moyo wenye kiburi ya mfalme wa Asiria na majivuno yake.
13 Kwa maana amesema, ''Kwa nguvu zangu na kwa hekima yangu niliyoifanya. na Nimeelewa, na nimeondoa mipaka ya watu. nimewaibia akiba yao, ni kama nilioileta chini kwa wenyeji wake.
14 Na mkono wangu umezitoa mali za mataifa kama vile mtu ayakusanyavyo mayai, kama nilivyokusanya dunia yote. Hakuna atakayeperusha mabawa yake au kufungua midomo yake au kulia.''
15 Je shoka lijisifu lenyewe juu ya mtu anayelitumia? Je litajisifia lenyewe zaidi ya yule anaelitumia kukatia? Au fimbo imuinuae yeye ambaye si mti.
16 Hivyo basi Yahwe wa majeshi atatuma wadhaifu miongoni mwa wasomi wa kijeshi; na chini ya utukufu na kuteketea kama kuteketea kwa moto.
17 Mwanga wa Isreli utakuwa moto, na Mtakatifu wake atakuwa ni moto unaoteketeza na kula mbigiri siku moja.
18 Yahwe atauteketeza utukufu wa msitu wake na shamba lake linalostawi, vyote nafsi na mwili; itakuwa kama vile mgonjwa apotezae maisha yake.
19 Mabaka ya miti ya misitu itakuwa michache sana, ambayo mtoto anaweza kuyahesabu.
20 Siku hiyo, mabaki ya Israeli, familia ya Yakobo ambayo imekimbia, hawatategemea kushindwa, lakini watamtegemea Yahwe, Mtakatifu wa Israeli.
21 Mabaki ya Yakobo yatarudi kwa Mungu mwenye nguvu.
22 Kwa kupitia watu wako, Israeli ni kama mchanga kama pwani ya bahari, Mabaki yao tu ndio yatakayorudi. Uaribifu wa amri, na mahitaji ya wingi wa haki.
23 Maana Bwana wa majeshi, anakaribia kuleta uharibifu utachukua nafasi kubwa kitika nchi.
24 Hivyo basi Bwana Yahwe wa majeshi anasema, ''watu wangu mhishio Sayuni, msiwaogope watu wa Asiria. Atawangamiza nyie kwa fimbo na atawanyua wafanyakazi juu yenu, kama ilivyotokea kwa Wamisri.
25 Msimuogope, kwa mda mfupi hasira yangu itakwisha juu yenu, na hasira yangu italeta uharibifu.''
26 Hivyo Yahwe wa majeshi atapiga mjeledi juu yenu kama vile alivyoishinda Midiani karibu na mwamba Orebu. Na atanyanyua fimbo yake juu ya bahari kama alivyofanya kule Misri.
27 Siku hiyo mzigo wake utanyanyuliwa kwenye mabeba yako na nira katika shingo yako, nayo nira itaharibiwa kwa sababu ya unene.
28 Adui amekuja Aiathi na amepitia Migroni; katika Michmashi ameyahifadhi mahitaji yake.
29 Wamevuka juu ya njia na wamepunzika huko Geba. Rama inatetemeka na Gibea ya Sauli imekimbia.
30 Lia kwa sauti, ewe binti wa Galimu! sikiliza, Laishashi! Maskini Anathothi!
31 Madmena ni mkimbizi na mkazi wa Gebuni wamejikusanya wanakimbia kutafuta msada.
32 Siku hizi za leo atasimulia huko Nobi na atatingisha mlima wa binti Sayuni, mlima wa Yerusalemu.
33 Tazama, Bwana Yahwe wa majeshi atapunguza matawi kwa nguvu za kutisha; miti mirefu itakatwa chini, wanaojivuna wataangushwa.
34 Atang'oa vichaka vya msitu kwa shoka, Lebanoni na utukufu wake utaanguka.