< Hosea 8 >
1 “Weka tarumbeta katika midomo yako! Tai anakuja juu ya nyumba ya Bwana kwa sababu watu wamevunja agano langu na waliasi dhidi ya sheria yangu.
ラッパをあなたの口にあてよ、はげたかは主の家に臨む。彼らがわたしの契約を破り、わたしの律法を犯したからだ。
2 Wananililia,'Mungu wangu, sisi katika Israeli tunakujua.'
彼らはわたしに向かって叫ぶ、「わが神よ、われわれイスラエルはあなたを知る」と。
3 Lakini Israeli amekataa mema, na adui atamfuata.
イスラエルは善はしりぞけた。敵はこれを追うであろう。
4 Wameweka wafalme, lakini sio kwa shauri langu. Wamewafanya wakuu, lakini sikuwa na habari. Kwa fedha zao na dhahabu wamejifanyia sanamu wenyewe, ili wakatiliwe mbali.”
彼らは王を立てた、しかし、わたしによって立てたのではない。彼らは君を立てた、しかし、わたしはこれを知らない。彼らは銀と金をもって、自分たちの滅びのために偶像を造った。
5 “Ndama yako imekataliwa, Samaria. Hasira yangu inawaka juu ya watu hawa. Kwa muda gani watakuwa na hatia?
サマリヤよ、わたしはあなたの子牛を忌みきらう。わたしの怒りは彼らに向かって燃える。彼らはいつになればイスラエルで罪なき者となるであろうか。
6 Kwa maana sanamu hii ilitoka Israeli; fundi aliifanya; si Mungu! Ndama ya Samaria itavunjwa vipande vipande.
これは工人の作ったもので、神ではない。サマリヤの子牛は砕けて粉となる。
7 Kwa maana watu hupanda upepo na kuvuna kimbunga. Mbegu zilizosimama hazina vichwa; haitoi unga. Ikiwa itakomaa, wageni watakula.
彼らは風をまいて、つむじ風を刈り取る。立っている穀物は穂を持たず、また実らない。たとい実っても、他国人がこれを食い尽す。
8 Israeli imemezwa; sasa wanalala kati ya mataifa kama kitu kisicho na maana.
イスラエルはのまれた。彼らは諸国民の間にあって、すでに無用な器のようになった。
9 Kwa maana walikwenda Ashuru kama punda wa mwitu pekee. Efraimu ameajiri wapenzi kwa ajili yake mwenyewe.
彼らはひとりさまよう野のろばのように、アッスリヤにのぼって行った。エフライムは物を贈って恋人を得た。
10 Hata ingawa wameajiri wapenzi kati ya mataifa, sasa nitawakusanya pamoja. Wao wataanza kupotea kwa sababu ya unyanyasaji wa mfalme wa wakuu.
たとい彼らが国々に物を贈って同盟者を得ても、わたしはまもなく彼らを集める。彼らはしばらくにして、王や君たちに油をそそぐことをやめる。
11 Kwa maana Efraimu imeongeza madhabahu kwa sadaka za dhambi, lakini zimekuwa madhabahu kwa kufanya dhambi.
エフライムは多くの祭壇を造って罪を犯したゆえ、これは彼には罪を犯すための祭壇となった。
12 Niliweza kuandika sheria yangu kwao mara elfu kumi, lakini wangeiona kama kitu cha ajabu kwao.
わたしは彼のために、あまたの律法を書きしるしたが、これはかえって怪しい物のように思われた。
13 Kwa ajili ya dhabihu za sadaka zangu, hutoa nyama na kuila, lakini mimi, Bwana, siwakubali. Sasa nitafikiri juu ya uovu wao na kuadhibu dhambi zao. Watarudi Misri.
彼らは犠牲を好み、肉をささげてこれを食べる。しかし主はこれを喜ばれない。今、彼らの不義を覚え、彼らの罪を罰せられる。彼らはエジプトに帰る。
14 Israeli amenisahau mimi, Muumba wake, na amejenga majumba. Yuda ameimarisha miji mingi, lakini nitatuma moto juu ya miji yake; itaharibu ngome zake.
イスラエルは自分の造り主を忘れて、もろもろの宮殿を建てた。ユダは堅固な町々を多く増し加えた。しかしわたしは火をその町々に送って、もろもろの城を焼き滅ぼす。