< Hosea 7 >
1 Wakati wowote ninapotaka kuponya Israeli, dhambi ya Efraimu inafunuliwa, pamoja na matendo maovu ya Samaria, kwa sababu wanafanya udanganyifu; mwizi huingia, na kundi la wanyang'anyi hushambulia mitaani.
kila mara nilipotaka kumponya Israeli, dhambi za Efraimu zinafichuliwa na maovu ya Samaria yanafunuliwa. Wanafanya udanganyifu, wevi huvunja nyumba, maharamia hunyangʼanya barabarani,
2 Hawatambui mioyoni mwao kwamba ninakumbuka matendo yao mabaya. Sasa matendo yao huwazunguka; yapo mbele ya uso wangu.
lakini hawafahamu kwamba ninakumbuka matendo yao yote mabaya. Dhambi zao zimewameza, ziko mbele zangu siku zote.
3 Kwa sababu ya uovu wao wamemfanya mfalme awe na furaha, na maofisa wao kwa uongo wao.
“Wanamfurahisha sana mfalme kwa maovu yao, wakuu wao kwa uongo wao.
4 Wote ni wazinzi, kama tanuru iliyochomwa na mwokaji, ambaye huacha kuuchochea moto tangu kukanda unga mpaka kuwa chachu.
Wote ni wazinzi, wanawaka kama tanuru ambayo moto wake mwokaji hana haja ya kuuchochea kuanzia kukanda unga hadi umekwisha kuumuka.
5 Siku ya mfalme wetu, viongozi walijifanya wagonjwa na ukali wa divai. Alinyoosha mkono wake kwa wale waliokuwa wakidhihaki.
Katika sikukuu ya mfalme wetu wakuu wanawaka kwa mvinyo, naye anawaunga mkono wenye mizaha.
6 kwa mioyo kama tanuri, wao hupanga mipango yao ya udanganyifu. Hasira zao hulala usiku wote; asubuhi huwaka juu kama moto.
Mioyo yao ni kama tanuru, wanamwendea kwa hila. Hasira yao inafoka moshi usiku kucha, wakati wa asubuhi inalipuka kama miali ya moto.
7 Wote wamepata moto kama tanuru, na huwaangamiza wale wanaowatawala. Wafalme wao wote wameanguka; hakuna hata mmoja wao ananiita.
Wote ni moto kama tanuru; wanawaangamiza watawala wao. Wafalme wake wote wanaanguka, wala hakuna yeyote kati yao aniitaye mimi.
8 Efraimu anajichanganya mwenyewe kati ya watu. Efraimu ni mkate ambayo haujawahi kugeuzwa.
“Efraimu anajichanganya na mataifa; Efraimu ni mkate ambao haukuiva.
9 Wageni wamekula nguvu zake, lakini hajui. Nywele za mvi hunyunyiza juu yake, lakini hajui.
Wageni wananyonya nguvu zake, lakini hafahamu hilo. Nywele zake zina mvi hapa na pale, lakini hana habari.
10 Kiburi cha Israeli kinawashuhudia; hata hivyo, hawajarudi kwa Bwana, Mungu wao, wala hawakumtafuta licha ya hayo yote.
Kiburi cha Israeli kinashuhudia dhidi yake, lakini pamoja na haya yote harudi kwa Bwana Mungu wake wala kumtafuta.
11 Efraimu ni kama njiwa, baradhuli na asiye na busara, humwita kwenda Misri, kisha huruka kwenda Ashuru.
“Efraimu ni kama hua, hudanganywa kwa urahisi na hana akili: mara anaita Misri, mara anageukia Ashuru.
12 Wakienda, nitasambaza wavu wangu juu yao, nami nitawaangusha kama ndege wa angani. Nitawaadhibu katika kusonga kwao pamoja.
Wakati watakapokwenda, nitatupa wavu wangu juu yao; nitawavuta chini waanguke kama ndege wa angani. Nitakaposikia wakikusanyika pamoja, nitawanasa.
13 Ole wao! Kwa maana wamepotea kutoka kwangu. Uharibifu unawajia! Wao wameasi dhidi yangu! Napenda kuwaokoa, lakini waliongea uongo dhidi yangu.
Ole wao, kwa sababu wamepotoka kutoka kwangu! Maangamizi ni yao kwa sababu wameniasi! Ninatamani kuwakomboa, lakini wanasema uongo dhidi yangu.
14 Wala hawakunililia kwa moyo wao wote, lakini wanaomboleza kwenye vitanda vyao. Wanakusanyika kwa ajili ya nafaka na divai mpya, nao wananiasi mimi.
Hawanililii mimi kutoka mioyoni mwao, bali wanaomboleza vitandani mwao. Hukusanyika pamoja kwa ajili ya nafaka na divai mpya, lakini hugeukia mbali nami.
15 Ingawa niliwafundisha na kuimarisha mikono yao, sasa wanapanga mabaya dhidi yangu.
Niliwafundisha na kuwatia nguvu, lakini wanapanga mabaya dhidi yangu.
16 Wanarudi, lakini harudi kwangu, Niliye Juu. Wao ni kama upinde usiotumainika. Maofisa wao wataanguka kwa upanga kwa sababu ya udhalimu wa vinywa. Hii itakuwa ni aibu yao katika nchi ya Misri.
Hawamgeukii Yeye Aliye Juu Sana, wako kama upinde wenye kasoro. Viongozi wao wataanguka kwa upanga kwa sababu ya maneno yao ya jeuri. Kwa ajili ya hili watadhihakiwa katika nchi ya Misri.