< Hosea 6 >

1 “Njoo, turudi kwa Bwana. Kwa maana ametuvunja vipande vipande, lakini atatuponya; ametujeruhi, lakini atatufunga majeraha yetu.
לכו ונשובה אל יהוה כי הוא טרף וירפאנו יך ויחבשנו
2 Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, na tutaishi mbele yake.
יחינו מימים ביום השלישי יקמנו ונחיה לפניו
3 Nasi tumjue Bwana; tukaendelee kumjua Bwana. Kuja kwake ni hakika kama asubuhi; atakuja kwetu kama mvua, kama mvua ya vuli ambayo huinyeshea ardhi.”
ונדעה נרדפה לדעת את יהוה כשחר נכון מצאו ויבוא כגשם לנו כמלקוש יורה ארץ
4 Efuraimu, nikufanyie nini? Yuda, nikufanyie nini? Uaminifu wako ni kama wingu la asubuhi, kama umande unaoondoka mapema.
מה אעשה לך אפרים מה אעשה לך יהודה וחסדכם כענן בקר וכטל משכים הלך
5 Kwa hiyo nimewavunja vipande vipande kwa vinywa vya manabii, nimewaua kwa maneno ya kinywa changu. Maagizo yako ni kama nuru inayoangaza.
על כן חצבתי בנביאים--הרגתים באמרי פי ומשפטיך אור יצא
6 Kwa maana natamani uaminifu wala si dhabihu, na kumjua Mungu kuliko sadaka za kuteketezwa.
כי חסד חפצתי ולא זבח ודעת אלהים מעלות
7 Kama Adamu wamevunja agano; hawakuwa waaminifu kwangu.
והמה כאדם עברו ברית שם בגדו בי
8 Gileadi ni jiji la wahalifu wenye miguu ya damu.
גלעד קרית פעלי און--עקבה מדם
9 Kama makundi ya wanyang'anyi wanaomngojea mtu, hivyo makuhani hujiunga pamoja kufanya mauaji kwa njia ya Shekemu; wamefanya uhalifu wa aibu.
וכחכי איש גדודים חבר כהנים דרך ירצחו שכמה כי זמה עשו
10 Katika nyumba ya Israeli nimeona jambo baya; Uzinzi wa Efraimu ukopale, na Israeli ametiwa unajisi.
בבית ישראל ראיתי שעריריה (שערוריה) שם זנות לאפרים נטמא ישראל
11 Kwa maana wewe, Yuda, mavuno yameteuliwa, nitakaporudisha urithi wa watu wangu.
גם יהודה שת קציר לך בשובי שבות עמי

< Hosea 6 >