< Hosea 4 >
1 Sikilizeni neno la Bwana, enyi watu wa Israeli. Bwana ana mashtaka dhidi ya wenyeji wa nchi, kwa sababu hakuna ukweli au uaminifu wa agano, hakuna ujuzi wa Mungu katika nchi.
[後編:以色列的罪惡和懲罰]四:以色列子民,請聽上主的話! 因為上主譴責此地的居民:因為此地沒有誠實,沒有仁愛,沒有人認識天主;
2 Kuna laana, uongo, mauaji, wizi na uzinzi. Watu wamevunja mipaka yote, na damu inakuja baada ya damu.
只有詛咒、謊言、殺戳、偷竊、姦淫、強暴和纍纍的血案。
3 Kwa hiyo nchi inakauka, na kila mtu aliyeishi ndani yake anaangamia; wanyama katika mashamba na ndege angani, hata samaki katika bahari, wanaondolewa.
因此,此地必要荒廢;凡住在這地上的,甚至田間的野獸和天空的飛鳥都要絕跡,連海中的魚類也要消滅。
4 Lakini usiruhusu mtu yeyote kuleta mashtaka; msiruhusu mtu yeyote ahukumu mtu mwingine. Kwa maana ninyi ndio makuhani, ninaowashtaki.
但是沒有人爭辯,也沒有人譴責! 司祭啊,我要與你爭辯!
5 Ninyi makuhani mtajikwaa wakati wa mchana; manabii pia watajikwaa pamoja nanyi usiku, nami nitamwangamiza mama yako.
你白天黑夜跌倒,先知也同你一齊跌倒,你竟然使你的人民喪亡。
6 Watu wangu wanaharibiwa kwa sababu ya ukosefu wa maarifa. Kwa sababu makuhani wamekataa maarifa, nami nitawakataa msiwe makuhani kwangu. Kwa sababu umesahau sheria yangu, ingawa mimi ni Mungu wako, nami pia nitasahau watoto wako.
我的百姓因缺乏知識而滅亡;因為你拋棄了知識,我也要拋棄你,不讓你充當我的司祭;你既然忘卻了你的天主的法律,我也要忘記你的子孫。
7 Makuhani wengi waliongezeka, zaidi walifanya dhambi dhidi yangu. Walibadilisha heshima zao kwa aibu.
司祭越增多,也越得罪我,竟以羞辱作為他們的光榮。
8 Wanajilisha dhambi ya watu wangu; wao ni wenye tamaa zaidi ya uovu wao.
他們賴我百姓的罪惡自肥,一心渴望他們的過犯。
9 Itakuwa sawa kwa watu kama kwa makuhani: nitawaadhibu wote kwa matendo yao; Nitawalipa kwa matendo yao.
由此百姓和司祭,一律看待:我將按他的行徑懲治他,對他的行為予以報復,
10 Watakula lakini hawatashiba; watafanya uzinzi lakini hawataongezeka, kwa sababu wamekwenda mbali na Bwana.
好使他們吃,卻吃不飽,行淫而不能繁殖;因為他們捨棄了上主,縱慾,
11 Wanapenda uasherati, divai, na divai mpya, ambayo imechukua uelewa wao.
行淫:老酒新酒叫人失去良知。
12 Watu wangu hutaka shauri kwa sanamu zao za mbao, na fimbo zao za kutembelea huwapa unabii. Kwa maana mawazo ya uasherati yamewadanganya, na wamefanya kama makahaba badala ya kuwa mwaminifu kwa Mungu wao.
我的人民求教於木偶,讓木杖啟示他;因為淫心迷往了他們,使他們行淫,遠開了他們的天主。
13 Wanatoa sadaka juu ya milima na kuteketeza uvumba kwenye milima, chini ya mialoni, milibua na miela, kwa sababu kivuli ni nzuri. Basi binti zenu hufanya uasherati, na binti zenu wanazini.
在山頂上獻祭,在丘陵上、在橡樹、楊樹和篤耨香下焚香,在濃蔭下多麼愉快;因此你們的女兒行淫,你的兒媳犯姦。
14 Mimi siwaadhibu binti zako wakati wanachagua kutenda uasherati, wala binti zako wakati wazini. Kwa maana wanaume pia wanajitoa kwa makahaba, na hutoa dhabihu ili waweze kufanya vitendo vya uasherati na makahaba. Hivyo watu wasiofahamu wataangamizwa.
但我卻不因你們的女兒行了淫,而懲罰她們,也不因你們的兒息媳犯了姦,而處罰她們;因為她們同蕩婦走往偏僻之處,又同廟妓一同獻祭:但無知的百姓卻因此而墮落!
15 Ingawa wewe, Israeli, umefanya uzinzi, lakini Yuda asiwe na hatia. Ninyi msiende Gilgali; msiende hadi Beth Aven. Wala msiape, “Aishivyo Bwana.”
以色列,如果你行了淫,但願猶大不要陷於罪惡! 你們不要到基耳加耳去,不要上貝特阿文,也不要起誓願 2上主永在! 」
16 Kwa maana Israeli amefanya ukaidi, kama ndama mkaidi. Je! Bwana anaweza kuwaleta kwenye malisho kama kondoo mahali penye nafasi?
的確,以色列倔強,有如一頭倔強的母牛,那麼上主那能牧放他們,有如在廣闊的草場牧放羔羊﹖
17 Efraimu alijiunga na sanamu; mwache peke yake.
厄弗辣因與偶像結了不解之緣:任憑他們吧!
18 Hata wakati kileo chao kimeondoka wakaendelea kufanya uzinzi; watawala wake hupenda sana aibu yao.
他們與醉客為伍,任意荒淫,喜愛羞恥勝於上主的光榮。
19 Upepo utamfunga kwa mabawa yake; nao wataona aibu kwa sababu ya dhabihu zao.
暴風要伸展羽翼將他們捲去,他們必因自己的祭壇蒙受恥辱。