< Hosea 13 >

1 Efraimu alipozungumza, kulikuwa na tetemeko. Alijikuza katika Israeli, lakini akawa na hatia kwa sababu ya ibada ya Baali, naye akafa.
כדבר אפרים רתת נשא הוא בישראל ויאשם בבעל וימת
2 Sasa wanafanya dhambi zaidi na zaidi. Wanatengeneza sanamu za chuma kutoka kwenye fedha zao, sanamu kwa kadiri ya ufanisi wao, zote ni kazi ya mafundi. Watu wanasema juu yao, 'Watu hawa watoao dhabihu na kumbusu ndama.'
ועתה יוספו לחטא ויעשו להם מסכה מכספם כתבונם עצבים מעשה חרשים כלה להם הם אמרים זבחי אדם עגלים ישקון
3 Kwa hiyo watakuwa kama mawingu ya asubuhi, kama umande unaoondoka mapema, kama makapi yanayotokana na upepo kutoka kwenye sakafu, na kama moshi utokao kwenye bomba.
לכן יהיו כענן בקר וכטל משכים הלך כמץ יסער מגרן וכעשן מארבה
4 Lakini mimi ndimi Bwana, Mungu weko, tangu nchi ya Misri. Hutamjua Mungu mwingine bali mimi; wala zaidi yangu, hakuna mkombozi mwingine.
ואנכי יהוה אלהיך מארץ מצרים ואלהים זולתי לא תדע ומושיע אין בלתי
5 Nilikujua jangwani, katika nchi yenye kame.
אני ידעתיך במדבר--בארץ תלאבות
6 Wakati ulipokuwa na malisho, ulishiba; na wakati uliposhiba, moyo wako ukainuliwa. Kwa sababu hiyo umenisahau.
כמרעיתם וישבעו--שבעו וירם לבם על כן שכחוני
7 Nitakuwa kama simba; kama chui nitaangalia kando ya njia.
ואהי להם כמו שחל--כנמר על דרך אשור
8 Nitawaangamiza kama dubu aliyenyang'anywa watoto wake. Nami nitararua vifua vyao, na huko nitawaangamiza kama simba, kama vile mnyama wa mwitu atakayerarua vipande vipande.
אפגשם כדב שכול ואקרע סגור לבם ואכלם שם כלביא חית השדה תבקעם
9 Nitawaangamiza, Israeli; nani atakayekusaidia?
שחתך ישראל כי בי בעזרך
10 Mfalme wako yuko wapi, ili akuokoe katika miji yako yote? Wako wapi wakuu, ambao kwao umeniambia hivi, 'Nipe mfalme na wakuu'?
אהי מלכך אפוא ויושיעך בכל עריך ושפטיך--אשר אמרת תנה לי מלך ושרים
11 Nimekupa mfalme kwa hasira yangu, nikamchukua kwa ghadhabu yangu.
אתן לך מלך באפי ואקח בעברתי
12 Uovu wa Efraimu umehifadhiwa; hatia yake imehifadhiwa.
צרור עון אפרים צפונה חטאתו
13 Atakuwa na uchungu wa kujifungua, lakini ni mwana mjinga, kwa maana wakati wa kuzaliwa, hatatoka tumboni.
חבלי יולדה יבאו לו הוא בן לא חכם כי עת לא יעמד במשבר בנים
14 Je, nitawaokoa na mkono wa kaburi? Je, nitawaokoa na kifo? Ewe Mauti yako wapi mapigo yako? Ewe kaburi kuko wapi kuharibu kwako? Huruma itafichwa na macho yangu. (Sheol h7585)
מיד שאול אפדם ממות אגאלם אהי דבריך מות אהי קטבך שאול--נחם יסתר מעיני (Sheol h7585)
15 Ingawa Efraimu anafanikiwa kati ya ndugu zake, upepo wa mashariki utakuja; upepo wa Bwana utapiga kutoka jangwani. Kijito cha maji cha Efraimu kitauka, na kisima chake hakitakuwa na maji. Adui yake atapora ghala lake la kila kitu cha thamani.
כי הוא בין אחים יפריא יבוא קדים רוח יהוה ממדבר עלה ויבוש מקורו ויחרב מעינו--הוא ישסה אוצר כל כלי חמדה
16 Samaria itakuwa na hatia, kwa sababu amemuasi dhidi ya Mungu wake. Wataanguka kwa upanga; watoto wao wadogo watavunjwa, na wanawake wao wajawazito watatambuliwa wazi.
תאשם שמרון כי מרתה באלהיה בחרב יפלו--עלליהם ירטשו והריותיו יבקעו

< Hosea 13 >