< Wahebrania 7 >
1 Ilikuwa hivi Melkizedeki, mfalme wa Salemu, Kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Abrahamu akirudi kutoka kuwaua wafalme na akambariki.
Porque este Melquisedec, rey de Salén, sacerdote del Dios Altísimo, el cual conoció a Abraham cuando regresaba de la derrota de los reyes, y lo bendijo,
2 Abrahamu alimpa moja ya kumi ya kila kitu alichokuwa amekiteka. Jina lake “Melkizedeki “maana yake” mfalme wa haki” na pia “mflame wa Salemu” ambayo ni “mfalme wa amani.”
al cual Abraham dio los diezmos de todo, cuyo nombre [significa] primero Rey de Justicia, y también Rey de Salén, es decir, Rey de Paz,
3 Hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku wala mwisho wa maisha yake. Badala yake, anabakia kuhani milele, kama mwana wa Mungu.
sin padre, sin madre, sin genealogía, sin principio de días ni fin de vida, sino declarado semejante al Hijo de Dios, permanece sacerdote para siempre.
4 Sasa fikiria jinsi huyu mtu alivyokuwa mkuu. Mzazi wetu Abrahamu alimpa moja ya kumi ya vitu vizuri alivyovichukua vitani.
Consideren, pues, cuán grande era éste, a quien el patriarca Abraham dio [el] diezmo de los despojos.
5 Na hakika, ukoo wa Walawi waliopokea ofisi za kikuhani walikuwa na amri kutoka kwenye sheria kukusanya moja ya kumi kutoka kwa watu, ambayo ni, kutoka kwa Wairaeli wenzao, pamoja na kwamba wao, pia, ni ukoo kutoka kwa Abrahamu.
Ciertamente los hijos de Leví que reciben el sacerdocio tienen mandamiento de tomar los diezmos del pueblo según la Ley, es decir, de sus hermanos, aunque éstos también descendieron de Abraham.
6 Lakini Melkizedeki, ambaye hakuwa wa ukoo kutoka kwa Walawi, alipokea moja ya kumi kutoka kwa Abrahamu, na akambariki, yeye aliyekuwa na ahadi.
Pero el que no descendió de [los levitas] recibió un diezmo de Abraham y bendijo al que tiene las promesas.
7 Hapo haikataliwi kwamba mtu mdogo hubarikiwa na mkubwa.
Fuera de toda discusión, el inferior es bendecido por el superior.
8 Kwa jambo hili mtu apokeaye moja ya kumi atakufa siku moja, lakini kwa jambo jingine mmoja aliyepokea moja ya kumi kwa Abrahamu ikaelezwa kama anayeishi.
Y aquí ciertamente reciben los diezmos de hombres mortales, pero allí, [uno] de quien se da testimonio que vive.
9 Na kwa namna ya kuzungumza, Lawi aliyepokea moja ya kumi, pia alilipa moja ya kumi kwa Abrahamu,
Por decirlo así, por medio de Abraham también Leví, quien recibía el diezmo, pagaba diezmos,
10 kwa sababu Lawi alikuwa katika viuno vya baba yake Abrahamu wakati Melkizedeki alipokutana na Abrahamu.
porque aún Leví estaba en el seno de su antepasado cuando Melquisedec lo conoció.
11 Sasa kama ukamilifu uliwezekana kupitia ukuhani wa Lawi, (hivyo chini yake watu hupokea sheria), kulikuwa na hitaji gani zaidi kwa kuhani mwingine kuinuka baada ya mfumo wa Melkizedeki, na siyo kuitwa baada ya mpangilio wa Haruni?
Así que, si [la] perfección fuera por medio del sacerdocio levítico, porque basado en él, el pueblo recibió [la] Ley, ¿qué necesidad había aún de que se levantara otro sacerdote según el orden de Melquisedec, y que no fuera nombrado según el orden de Aarón?
12 Kwa hiyo ukuhani ukibadilika, hapana budi sheria nayo kubadilika.
Porque al ser cambiado el sacerdocio, es necesario que también haya cambio de ley.
13 Kwa mmoja ambaye mambo haya yalisemwa kuhusu kabila jingine, kutoka kwake hakuna aliyehudumu madhabahuni.
Porque Aquél de Quien se dicen estas cosas, es de otra tribu, de la cual nadie sirvió al altar.
14 Sasa ni wazi kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila ambalo Musa hakutaja kuhusu makuhani.
Pues es evidente que nuestro Señor descendió de la tribu de Judá, en cuanto a la cual Moisés nada dijo con respecto a sacerdotes.
15 Na haya tusemayo ni wazi hasa ikiwa kuhani mwingine atatokea kwa mfano wa Melkizedeki.
Es aún más evidente, si se levanta otro sacerdote a semejanza de Melquisedec,
16 Kuhani huyu mpya siyo mmoja ambaye amekuwa kuhani juu ya msingi wa sheria zinazohusiana na uzao wa mtu, lakini katika msingi wa nguvu ya maisha yasiyoweza kuharibika.
constituido no según [la] ley sobre la descendencia humana, sino según el poder de una vida indestructible.
17 Hivyo maandiko yanashuhudia kuhusu yeye: “Wewe ni kuhani milele baada ya mfumo wa Melkizedeki.” (aiōn )
Pues se da testimonio: Tú eres Sacerdote para siempre Según el orden de Melquisedec. (aiōn )
18 Kwa kuwa amri iliyotangulia iliwekwa pembeni kwa sababu ilikuwa dhaifu na haifai.
Porque ciertamente se abroga el mandamiento anterior por causa de su debilidad e ineficacia
19 Hivyo sheria haikufanya chochote kikamilifu. Isipokuwa, kulikuwa na ujasiri mzuri kwa hayo tunamsogelea Mungu.
(pues la Ley nada perfeccionó). Pero fue introducción a una mejor esperanza por la cual nos acercamos a Dios,
20 Na Ujasiri huu mzuri haukutokea pasipo kuzungumzia kiapo, kwa hili makuhani wengine hawakuchukua kiapo chochote.
lo cual fue hecho con juramento. Porque ciertamente ellos son declarados sacerdotes sin juramento,
21 Lakini Mungu alichukua kiapo wakati aliposema kuhusu Yesu, “Bwana ameapa na hatabadilisha mawazo yake.' wewe ni kuhani milele.” (aiōn )
pero Éste, con el juramento del que le dice: [El] Señor juró y no cambiará de parecer: Tú eres sacerdote para siempre. (aiōn )
22 Kwa hili Yesu pia amekuja kuwa dhamana ya agano bora.
Por tanto Jesús es Garante de un mejor Pacto.
23 Kwa hakika, kifo huzuia makuhani kuhudumu milele. Hii ni kwa sababu walikuwapo makuhani wengi, mmoja baada ya mwingine.
Los sacerdotes fueron muchos, porque la muerte les impedía permanecer.
24 Lakini kwa sababu Yesu anaishi milele, ukuhani wake haubadiliki. (aiōn )
Pero [Jesús], por cuanto permanece para siempre, tiene un sacerdocio inmutable. (aiōn )
25 Kwa hiyo yeye pia anaweza kwa ukamilifu kukamilisha kuwaokoa wanaomkaribia Mungu kupitia kwake, kwa kuwa yeye anaishi daima kwa kuomba kwa ajili yao.
Por tanto puede también salvar para siempre a los que por medio de Él se acercan a Dios, y vive siempre para interceder por ellos.
26 Kwa hiyo kuhani mkuu wa namna hii anastahili kwetu. Asiye na dhambi, hatia, msafi, aliyetengwa kutoka kwa wenye dhambi, na amekuwa juu kuliko mbingu.
Porque este Sumo Sacerdote también nos convenía santo, inocente, sin mancha, separado de los pecadores y más exaltado que los cielos,
27 Yeye hakuwa na uhitaji, mfano wa makuhani wakuu, kutoa dhabihu kila siku, kwanza kwa dhambi yake mwenyewe, na baadaye kwa dhambi za watu. Alifanya hivi mara moja kwa wote, alipojitoa yeye mwenyewe.
que no necesita, como los sumos sacerdotes, ofrecer sacrificios cada día, primero por sus propios pecados y después por los del pueblo, porque esto lo hizo al ofrecerse una vez para siempre.
28 Kwa sheria huwateua watu dhaifu kuwa makuhani wakuu, lakini neno la kiapo, lililokuja baada ya sheria, alimteua Mwana, aliyefanywa kuwa mkamilifu milele. (aiōn )
Porque la Ley designa como sumos sacerdotes a hombres que tienen debilidad, pero la Palabra del juramento, que es posterior a la Ley, [designa] al Hijo declarado perfecto para siempre. (aiōn )