< Wahebrania 3 >
1 Kwa hiyo, ndugu watakatifu, washiriki wa wito wa mbinguni, mumfikiri Yesu, Mtume na Kuhani Mkuu wa ukiri wetu.
Wherefore, holy brethren, partakers of a heavenly calling, consider the apostle and high-priest of our profession, Jesus;
2 Alikuwa mwaminifu kwa Mungu aliyemteua, kama Musa alivyokuwa mwaminifu pia katika nyumba yote ya Mungu.
who was faithful to him that appointed him, as also was Moses in all his house.
3 Kwa kuwa Yesu amehesabiwa kuwa na heshima kubwa kuliko aliyokuwa nayo Musa, kwa sababu yule anayejenga nyumba anahesabiwa kuwa na heshima kubwa kuliko nyumba yenyewe.
For he hath been counted worthy of more glory than Moses, inasmuch as greater than the house is he who built it.
4 Kwa kuwa kila nyumba hujengwa na mtu fulani, lakini yule anayejenga kila kitu ni Mungu.
For every house is builded by some one; but he who built all things is God.
5 Hakika Musa alikuwa mwaminifu kama mtumishi katika nyumba yote ya Mungu, akitoa ushuhuda kuhusu mambo yatakayosemwa wakati ujao.
And Moses indeed was faithful in all his house as a servant, that he might testify of those things which were to be spoken;
6 Lakini Kristo ni Mwana katika usimamizi wa nyumba ya Mungu. Sisi ni nyumba yake kama tutashikilia haraka katika kujiamini na fahari ya kujiamini.
but Christ as a son over his house; whose house are we, if we hold fast the confidence and joyousness of our hope.
7 Kwa hiyo, ni kama Roho Mtakatifu asemavyo, “Leo, kama utasikia sauti yake,
Wherefore, as the Holy Spirit saith: “To-day, if ye hear his voice,
8 Usiufanye moyo wako kuwa mgumu kama Waisraeli walivyofanya katika uasi, katika wakati wa kujaribiwa nyikani.
harden not your hearts, as in the provocation, in the day of the temptation in the wilderness,
9 Huu ulikuwa wakati ambao baba zenu waliniasi kwa kunijaribu, na wakati, kwa miaka arobaini, waliona matendo yangu.
where your fathers tempted me by proving me, and saw my works forty years.
10 Kwa hiyo sikufurahishwa na kizazi hicho. Nilisema, 'Wanapotea kila mara katika mioyo yao, na hawajui njia zangu.
Wherefore I was offended with that generation, and said, They always err in their heart, but they knew not my ways;
11 Ni kama vile nilivyoapa katika hasira yangu: hawataiingia raha yangu.”
so I swore in my wrath, They shall not enter into my rest.”
12 Muwe waangalifu, ndugu, ili kwamba usije ukawepo moyo mwovu wa kutokuamini kwa mmoja wenu, moyo ambao utakwenda mbali na Mungu aliye hai.
Take heed, brethren, lest there be in any one of you an evil heart of unbelief, in departing from the living God.
13 Badala yake, mhamasishane kila siku kila mmoja na mwenzie, ili kila iitwapo leo mtamani, ili kwamba mmoja kati yenu asifanywe kuwa mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.
But exhort one another daily, as long as it is called To-day, that none of you may be hardened through the deceitfulness of sin.
14 Kwa maana tumekuwa washiriki wa Kristo ikiwa tutashikamana na uthabiti wetu kwa nguvu katika yeye kutoka mwanzo hadi mwisho.
For we have become partakers of Christ, if we hold fast our first confidence firm to the end.
15 Kuhusu hili imekwisha kusemwa, “Leo kama mtaisikiliza sauti yake, msiifanye mioyo yenu kuwa migumu, kama Waisraeli walivyofanya wakati wa uasi.”
When it is said, “To-day, if ye hear his voice, harden not your hearts, as in the provocation,”
16 Ni akina nani hao waliomsikia Mungu na kuasi? Hawakuwa wale wote ambao Musa alikuwa amewaongoza kutoka Misri?
who then, when they had heard, provoked? Was it not all who came out of Egypt by means of Moses?
17 Na kina nani ambao Mungu aliwakasirikia kwa miaka arobaini? Siyo pamoja na wale waliotenda dhambi, ambao miili yao iliyokufa ililala jangwani?
And with whom was he offended forty years? Was it not with those who sinned, whose carcasses fell in the wilderness?
18 Ni akina nani aliowaapia Mungu kwamba hawataingia katika raha yake, kama siyo wale ambao hawakumtii yeye?
And to whom did he swear that they should not enter into his rest, except to those who were disobedient?
19 Tunaona kwamba hawakuweza kuingia katika raha yake kwa sababu ya kutokuamini.
So then we see that they could not enter in because of unbelief.