< Wahebrania 13 >
1 Basi upendo wa ndugu na uendelee.
Endeleeni kupendana kama ndugu.
2 Msisahau kuwakaribisha wageni, maana kwa kufanya hivi, baadhi wamewakaribisha malaika pasipo kujua.
Msisahau kuwakaribisha wageni, kwa kuwa kwa kufanya hivyo, watu wengine waliwakaribisha malaika pasipo kujua.
3 Kumbuka wote waliomo gerezani, kana kwamba mulikuwa nao kule pamoja nao, na kama miili yenu ilitendewa kama wao.
Wakumbukeni wale waliofungwa gerezani kana kwamba ninyi mmefungwa pamoja nao. Pia wakumbukeni wale wanaotendewa vibaya, kana kwamba ni ninyi wenyewe mnateswa.
4 Basi ndoa na iheshimiwe na wote na basi kitanda cha ndoa kifanywe kuwa safi, kwa maana Mungu atawahukumu waasherati na wazinzi.
Ndoa na iheshimiwe na watu wote, nayo malazi yawe safi, kwa kuwa Mungu atawahukumu wazinzi na waasherati wote.
5 Basi njia zenu za maisha ziwe huru katika upendo wa pesa. Muwe wanoridhika na vitu mulivyonavyo, kwani Mungu mwenyewe alisema, “Sitawaacha ninyi kamwe, wala kuwatelekeza ninyi.”
Yalindeni maisha yenu msiwe na tabia ya kupenda fedha, bali mridhike na vile mlivyo navyo, kwa sababu Mungu amesema, “Kamwe sitakuacha, wala sitakupungukia.”
6 Basi tulidhikeni ili tusema kwa ujasiri, “Bawa ni msaidizi wangu; Sitaogopa. Mwanadamu aweza kunifanya nini?”
Kwa hiyo tunaweza kusema kwa ujasiri, “Bwana ni msaada wangu; sitaogopa. Mwanadamu anaweza kunitenda nini?”
7 Wafikirieni wale walio waongoza, wale waliongea neno la Mungu kwenu, na kumbukeni matokeo ya mienendo yao; igeni imani zao.
Wakumbukeni viongozi wenu, wale waliowaambia neno la Mungu. Angalieni matokeo ya mwenendo wa maisha yao mkaiige imani yao.
8 Yesu Kristo ni yeye jana, leo, na ata milele. (aiōn )
Yesu Kristo ni yeye yule jana, leo na hata milele. (aiōn )
9 Usije ukaongozwa na mafundisho mbalimbali ya kigeni kwani ni vizuri kwamba moyo ujengwe kwa neema, na siyo kwa sheria kuhusu chakula hayo hayatawasaidia wale wanaoishi kwa hayo.
Msichukuliwe na kila aina ya mafundisho ya kigeni. Ni vyema mioyo yenu iimarishwe kwa neema, wala si kwa sheria kuhusu utaratibu wa vyakula, ambavyo havina faida kwa wale wanaozishika hizo sheria.
10 Tunayo madhabau ambayo wale wanaotumika ndani ya hekalu hawana haki ya kula.
Sisi tunayo madhabahu ambayo wale wanaohudumu katika hema hawana haki ya kula vile vitu vilivyowekwa juu yake.
11 Kwa kuwa damu za wanyama, zilizotolewa dhabihu kwa ajili ya dhambi, ililetwa na kuhani mkuu ndani ya sehemu takatifu, lakini miili yao ilichomwa nje ya kambi.
Kuhani mkuu huchukua damu ya wanyama na kuiingiza Patakatifu pa Patakatifu, kama sadaka ya dhambi, lakini miili ya hao wanyama huteketezwa nje ya kambi.
12 Kwa hiyo Yesu naye aliteseka nje ya lango la mji, hili kwamba kuweka wakfu watu kwa Mungu kupitia damu yake.
Vivyo hivyo, Yesu naye aliteswa nje ya lango la mji ili awatakase watu kwa damu yake mwenyewe.
13 Na kwa hiyo twendeni kwake nje ya kambi, tukizibeba fadheha zake.
Kwa hiyo, basi na tumwendee nje ya kambi, tukiichukua aibu aliyobeba.
14 Kwani hatuna makao ya kudumu katika mji huu. Badala yake tutafute mji ambao unakuja.
Kwa kuwa hapa hatuna mji udumuo, bali tunautafuta ule ujao.
15 Kupitia Yesu mnapaswa mara kwa mara kujitoa sadaka ya kumtukuza Mungu, kumsifu kwamba tunda la midomo yetu likili jina lake.
Basi kwa njia ya Yesu, tuzidi kumtolea Mungu dhabihu ya sifa, yaani matunda ya midomo inayolikiri Jina lake.
16 Na usisahau kufanya mazuri na kusadiana ninyi kwa ninyi, kwa kuwa ni kwa sadaka kama hiyo ndiyo Mungu hupendezwa sana.
Na msiache kutenda mema na kushirikiana vile vitu mlivyo navyo, kwa kuwa dhabihu kama hizo ndizo zinazompendeza Mungu.
17 Tiini na kujishusha kwa viongozi wenu, kwani wanaendelea kuwalinda kwa ajili ya nafsi zenu, kama wale watakaotoa hesabu. Tiini ili kwamba viongozi wenu waweze kuwatunza kwa furaha, na sio kwa huzuni, ambayo haitawasaidia.
Watiini viongozi wenu na kujinyenyekeza chini ya mamlaka yao. Kwa maana wao wanakesha kwa ajili yenu kama watu watakaopaswa kutoa hesabu. Watiini ili wafanye kazi yao kwa furaha, wala si kama mzigo, maana hiyo haitakuwa na faida kwenu.
18 Tuombeni, kwani tuna uhakikwa kwamba tuna dhamira njema, tunatamani kuishi maisha ya heshima katika mambo yote.
Tuombeeni. Tuna hakika kuwa tunayo dhamiri safi na shauku ya kuishi kwa uadilifu kwa kila njia.
19 Na nyote ninawatia moyo zaidi mfanye hivi, ili kwamba niweze kurudi kwenu hivi karibuni.
Ninawasihi zaidi mniombee ili nipate kurudishwa kwenu upesi.
20 Sasa Mungu wa amani, ambaye aliwaleta tena kutoka kwa wafu mchungaji mkuu wa kondoo, Bwana wetu Yesu, kwa damu ya agano la milele, (aiōnios )
Basi Mungu wa amani, ambaye kwa damu ya Agano la milele alimleta tena kutoka kwa wafu Bwana wetu Yesu, yule Mchungaji Mkuu wa kondoo, (aiōnios )
21 Atawapa uwezo kwa kila jambo zuri kufanya mapenzi yake, akifanya kazi ndani yetu iliyo njema ya kupendeza machoni pake, kupitia Yesu Kristo, kwake uwe utukufu milele na milele. Amina. (aiōn )
awafanye ninyi wakamilifu mkiwa mmekamilishwa katika kila jambo jema ili mpate kutenda mapenzi yake, naye atende ndani yetu kile kinachompendeza machoni Pake, kwa njia ya Yesu Kristo, ambaye utukufu una yeye milele na milele. Amen. (aiōn )
22 Sasa ninakutia moyo, ndugu, kuchukualiana na neno la kutia moyo ambalo kwa ufupi nililiandika kwenu.
Ndugu zangu, nawasihi mchukuliane na maneno yangu ya maonyo, kwa kuwa nimewaandikia waraka mfupi tu.
23 Fahamu kwamba ndugu yetu Timotheo ameshaachiwa huru, ambaye pamoja naye nitawaona kama atakuja hivi karibuni.
Nataka ninyi mjue kwamba ndugu yetu Timotheo amefunguliwa kutoka gerezani. Akifika mapema, nitakuja pamoja naye kuwaona.
24 Salimia viongozi wako wote na waumini wote. Wale wanaotoka Italia wanakusalimia.
Wasalimuni viongozi wenu wote na watakatifu wote. Wale wa kutoka Italia wanawasalimu.
25 Na neema iwe nanyi nyote.
Neema iwe nanyi nyote. Amen.