< Wahebrania 10 >
1 Kwa vile sheria ni kivuli cha mambo mema yajayo, si yale yaliyo halisi. Sheria kamwe haiwezi kuwakamilisha wale ambao wanaomkaribia Mungu kwa njia ya dhabihu zilezile ambazo makuhani waliendelea kutoa mwaka baada ya mwaka.
For the law, having a shadow of good things to come, and not the very image of the things, can never, with the same sacrifices, which they offer year by year continually, make a perfect expiation for those who come to them:
2 Au vinginevyo dhabihu hizo zisingeweza kukoma kutolewa? Kwa kigezo hicho waabuduo, wakiwa wamesafishwa mara moja, wasingelikuwa na utambuzi zaidi wa dhambi.
for then, would they not have ceased to be offered? because the worshipers, after being once cleansed, would no longer have a consciousness of sins.
3 Bali katika dhabihu hizo kuna ukumbusho wa dhambi zilizotendwa mwaka baada ya mwaka.
There is, however, in these sacrifices, a remembrance of sins every year.
4 Kwa kuwa haiwezekani kwa damu ya mafahari na mbuzi kuziondoa dhambi.
For it is impossible that the blood of bulls and of goats should take away sins.
5 Wakati Kristo alipokuja duniani, alisema, “Hamkutamani matoleo au dhabihu, badala yake, mliandaa mwili kwa ajili yangu.
Wherefore, when he comes into the world, he says: Sacrifice and offering thou hast not desired, but a body thou hast prepared me;
6 Hamkuwa na thamani katika matoleo yote ya kuteketezwa au dhabihu kwa ajili ya dhambi.
in whole burnt-offerings and offerings for sin, thou hast had no pleasure.
7 Kisha nilisema, “Ona, hapa ninayafanya mapenzi yako, Mungu, kama ilivyoandikwa kunihusu mimi katika gombo”.
Then, said I, Behold, I come, (in the roll of the book it is written of me, ) to do thy will, O God.
8 Alisema kama ilivyo semwa hapo juu: “Hamkutamani dhabihu, matoleo, au sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya dhambi, wala hukuona furaha ndani yake” dhabihu ambazo zinatolewa kulingana na sheria.
After saying above, Thou didst neither desire, nor take pleasure in sacrifice and offering and whole burnt-offerings and offerings for sin, which are offered according to the law,
9 Kisha alisema, “Ona, niko hapa kufanya mapenzi yako”. Ameweka pembeni taratibu zilizo za awali ili kuimarisha zile za pili.
then he said, Behold, I come to do thy will: he takes away the first, that he may establish the second.
10 Katika taratibu za pili, tumekwisha tengwa kwa Mungu kwa mapenzi yake kupitia kujitoa kwa mwili wa Yesu Kristo mara moja kwa nyakati zote.
By which will, we are sanctified through the offering of the body of Jesus Christ, once for all time.
11 Ni kweli, kila kuhani husimama kwa huduma siku kwa siku, akitoa dhabihu ile ile, ambayo, kwa vyovyote, kamwe isingeweza kuziondoa dhambi.
And every priest stands daily ministering, and offering oftentimes the same sacrifices, which can never take away sins:
12 Lakini baada ya Kristo kutoa dhabihu mara moja kwa dhambi milele yote, aliketi mkono wa kuume wa Mungu,
but after offering one sacrifice for sins, he himself sits continually at the right hand of God,
13 akisubiri mpaka maadui zake watiwe chini na kufanywa kiti kwa ajili ya miguu yake.
henceforth waiting till his enemies be made his footstool.
14 Kwa kuwa kwa njia ya toleo moja amewakamilisha milele wale ambao wametengwa kwa Mungu.
For by one offering, he has made a perfect and perpetual expiation for the sanctified.
15 Na Roho Mtakatifu pia ashuhudia kwetu. Kwa kuwa kwanza alisema,
And, indeed, the Holy Spirit is a witness for us. For after he had said before,
16 “Hili ni agano nitakalofanya pamoja nao baada ya siku hizo; asema Bwana: nitaweka sheria zangu ndani ya mioyo yao, na nitaziandika katika akili zao”.
This is the covenant that I will make with them after those days, says the Lord; putting my laws in their hearts, I will also write them in their understandings:
17 Kisha alisema, “Hawatazikumbuka tena dhambi na matendo yao mafu”.
he adds, And their sins and iniquities I will remember no more.
18 Sasa mahali palipo na msamaha kwa hawa, hakuna tena dhabihu yoyote kwa ajili ya dhambi.
Now, where remission of these is, there is no more offering for sin.
19 Kwa hiyo, ndugu, tunao ujasiri wa kuingia mahali patakatifu zaidi kwa damu ya Yesu.
Having therefore, brethren, confidence to enter the holiest by the blood of Jesus,
20 Hiyo ni njia ambayo ameifungua kwa ajili yetu kwa njia ya mwili wake, mpya na hai inayopitia kwenye pazia.
by a new and living way which he has dedicated for us, through the vail, that is, his flesh;
21 Na kwa sababu tunaye kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu,
and having a great high, priest over the house of God,
22 na tumkaribie na moyo wa kweli katika utimilifu wa uhakika wa imani tukiwa na mioyo iliyonyunyiziwa safi kutoka uovu wa dhamiri na kuwa na miili yetu iliyooshwa kwa maji safi.
let us draw near with a true heart, in full assurance of faith, having; our hearts sprinkled from an evil conscience, and our bodies washed with pure water;
23 Basi na tushikilie kwa uthabiti katika ungamo la ujasiri wa tumaini letu, bila ya kugeuka, kwa sababu Mungu aliyeahidi ni mwaminifu.
let us hold fast the unwavering confession of our hope, for he is faithful who has promised;
24 Na tuzidi kutafakari namna ya kumtia moyo kila mmoja kupenda na matendo mema.
and let us consider one another that we may excite to love and good works,
25 Na tusiache kukusanyika pamoja, kama wafanyavyo wengine. Badala yake, kutiana moyo kila mmoja zaidi na zaidi, kama muonavyo siku inakaribia.
not forsaking the assembling of ourselves together, as is the custom of some; but exhorting one another, and so much the more, as you see the day approaching.
26 Kama tukifanya makusudi kuendelea kutenda dhambi baada ya kuwa tumepokea elimu ya ukweli, Dhabihu nyingine ya dhambi haisalii tena.
For if we sin willfully, after we have received the knowledge of the truth, there remains no longer a sacrifice for sins;
27 Badala yake, kuna tarajio pekee la hukumu ya kutisha, na ukali wa moto ambao utawateketeza maadui wa Mungu.
but a certain fearful looking for of judgment, and a fiery indignation which will devour the adversaries.
28 Yeyote ambaye ameikataa sheria ya Musa hufa bila rehema mbele ya ushuhuda wa mashahidi wawili au watatu.
He that despised Moses law, died without mercy, on the testimony of two or three witnesses:
29 kiwango gani zaidi cha adhabu unafikiri kinamstahiri kilammoja ambaye amemdharau mwana wa Mungu, yeyote aliyeitendea damu ya agano kama kitu kisicho kitakatifu, damu ambayo kwayo aliiweka wakfu kwa Mungu - yeyote ambaye amemtukana Roho wa neema?
of how much severer punishment do you think he shall be thought worthy, who has trodden under foot the Son of God, and has counted the blood of the covenant, with which he was sanctified, a common thing, and has done despite to the Spirit of grace?
30 Kwakuwa tunajua mmoja ambaye aliyesema, “Kisasi ni changu, nitalipa”. Na tena, “Bwana atawahukumu watu wake”.
For we know him who has said, Vengeance is mine, I will repay, says the Lord. And again, The Lord will judge his people.
31 Ni jambo la kuogofya mtu kuangukia katika mikono ya Mungu aliye hai!
It is a fearful thing to fall into the hands of the living God.
32 Lakini kumbuka siku zilizopita, baada ya kutiwa kwenu nuru, ni jinsi gani mliweza kuvumilia maumivu makali.
But remember the former days, in which, after you were enlightened, you endured a great conflict of sufferings;
33 Mlikuwa mmewekwa wazi katika dhihaka ya matukano na mateso, na mlikuwa washiriki pamoja na wale waliopitia mateso kama hayo.
partly, while you became a public spectacle, by reproaches and afflictions: partly, while you became partakers with those who were so treated.
34 Kwa kuwa mlikuwa na moyo wa huruma kwa hao waliokuwa wafungwa, na mlipokea kwa furaha adhabu ya urithi wenu, mkijua kwamba ninyi wenyewe mlikuwa na urithi bora na wa kudumu milele.
For you sympathized with me in my bonds, and endured joyfully the seizure of your possessions, knowing that you have for yourselves a better and abiding substance in the heavens.
35 Kwa hiyo msiutupe ujasiri wenu, ulio na zawadi kuu.
Cast not away, therefore, your confidence, which has a great reward.
36 Kwa kuwa mnahitaji uvumilivu, ili kwamba mpate kupokea ambacho Mungu amekiahidi, baada ya kuwa mmekwisha yatenda mapenzi yake.
For you have need of patience, that, after you have done the will of God, you may receive the promise.
37 Kwa kuwa baada ya kitambo kidogo, mmoja anayekuja, atakuja hakika na hatakawia.
For yet a very, very little while, and He that comes will come, and will not delay.
38 Mwenye haki wangu ataishi kwa imani. Kama atarudi nyuma, sitapendezwa naye.”
But the just by faith shall live; and if he draw back, my soul will have no pleasure in him.
39 Lakini sisi si kama wale warudio nyuma kwa kuangamia. Badala yake, sisi ni baadhi ya wale tulio na imani ya kuzilinda roho zetu.
But we are not of those who draw back to perdition; but of those who believe to the saving of the soul.