< Hagai 2 >
1 Katika Mwezi wa saba siku ya ishirini na moja ya mwezi, Neno la Bwana lilikuja kwa mkono wa Nabii Hagai, na kusema,
七月二十一日,耶和华的话临到先知哈该说:
2 “Ongea na mkuu wa mkoa wa Yudah, Zerubabeli mwana wa Sheltieli, na kwa kuhani mkuu Yehozadaki; na kwa masalia ya watu. Waambie,
“你要晓谕犹大省长撒拉铁的儿子所罗巴伯和约撒答的儿子大祭司约书亚,并剩下的百姓,说:
3 Ni nani amebaki kati yenu aliuona utukufu wa nyumba ya kwanza? Na mnauonaje huu wa sasa? Je si kama si chochote machoni penu?
你们中间存留的,有谁见过这殿从前的荣耀呢?现在你们看着如何?岂不在眼中看如无有吗?”
4 Sasa, muwe hodari, Zerubabeli' -hili ni tamko la Bwana - na uwe hodari, kuhani mkuu Joshua mwana wa Yehozadaki; muwe hodari, enyi watu wa nchi! - hili ni tamko la Bwana - na kazi, kwa kuwa ni pamoja nawe! hili ni tamko la Bwana wa majeshi.
耶和华说:“所罗巴伯啊,虽然如此,你当刚强!约撒答的儿子大祭司约书亚啊,你也当刚强!这地的百姓,你们都当刚强做工,因为我与你们同在。这是万军之耶和华说的。
5 Kutegemeana na ahadi ilioko katika agano nililofanya na ninyi mlipotoka Misri na Roho yangu ilisimama katikati yenu, msiogope'
这是照着你们出埃及我与你们立约的话。那时,我的灵住在你们中间,你们不要惧怕。”
6 Kwa kuwa Bwana wa majeshi anasema hivi: 'kitambo kidogo kwa mara nyingine nitatikisa mbingu na dunia, bahari na nchi kavu!
万军之耶和华如此说:“过不多时,我必再一次震动天地、沧海,与旱地。
7 Na nitatikisa kila taifa, na kila taifa wataleta vitu vya thamani kwangu, na kuijaza nyumba hii na utukufu!' asema Bwana wa Majeshi
我必震动万国;万国的珍宝必都运来,我就使这殿满了荣耀。这是万军之耶和华说的。”
8 Dhahabu na fedha ni yangu' - hili ni tamko la Bwana wa majeshi.
万军之耶和华说:“银子是我的,金子也是我的。
9 Utukufu wa nyumba hii utakuwa mkuu zaidi ya utukufu wa nyumba ya kwanza ', asema Bwana wa majeshi,' na nitawapa amani katika sehemu hii'- hili ni Tamko la Bwana wa majeshi
这殿后来的荣耀必大过先前的荣耀;在这地方我必赐平安。这是万军之耶和华说的。”
10 Katika siku ya ishirini na nne mwezi wa tisa, mwaka wa pili wa utawala wa Dario, neno la Bwana lilimjia nabii Hagaina kusema,
大流士王第二年九月二十四日,耶和华的话临到先知哈该说:
11 “Bwana wa majeshi asema hivi: Muulize kuhani kuhusu sheria, na kusema:
万军之耶和华如此说:“你要向祭司问律法,
12 kama mtu akibeba nyama iliyotolewa kwa Bwana katika pindo la vazi lake, kama upindo utagusa mkate au mchuzi, mvinyo au mafuta, au chakula kingine, je chakula hicho kinafanyika kitakatifu?”Kuhani alijibu akasema, “hapana”
说:若有人用衣襟兜圣肉,这衣襟挨着饼,或汤,或酒,或油,或别的食物,便算为圣吗?”祭司说:“不算为圣。”
13 Halafu Hagai akasema.”Kama mtu mchafu najisi kwa ajili ya kumgusa maiti na kugusa vitu hivi, wote wanaweza kuwa wachafu?” Kuhani akajibu na kusema, “Ndiyo, watakuwa wachafu.”
哈该又说:“若有人因摸死尸染了污秽,然后挨着这些物的哪一样,这物算污秽吗?”祭司说:“必算污秽。”
14 Kwa hiyo Haghai akajibu nakusema, “Ni pamoja na hawa watu na pamoja na taifa liliko mbele yangu! - haya anayasema Bwana- na pia kila kitu kimekwisha kwa mkono wake: walichotoa hakikuwa kisafi kilikuwa kichafu.
于是哈该说:“耶和华说:这民这国,在我面前也是如此;他们手下的各样工作都是如此;他们在坛上所献的也是如此。”
15 Kwa hiyo, fikiri kutoka siku hii ya leo na za nyuma, kabla hata jiwe halijawekwa kwenye jiwe lingine katika hekalu la Bwana,
现在你们要追想,此日以前,耶和华的殿没有一块石头垒在石头上的光景。
16 ilikuwaje basi? kila mtu alipokuja kwenye vipimo ishirini vya nafaka, kumbe kulikuwa na vipimo kumi tu, na aliyekuja na aliyekuja kuchota divai ya vipimo hamsini, kumbe kuliwa na vipimo ishirini tu.
在那一切日子,有人来到谷堆,想得二十斗,只得了十斗。有人来到酒池,想得五十桶,只得了二十桶。
17 Niliwataabisha ninyi na kazi za mikono yenu kwa doa na koga, nalikini hamkunirudia'- asema Bwana.
在你们手下的各样工作上,我以旱风、霉烂、冰雹攻击你们,你们仍不归向我。这是耶和华说的。
18 tafakari siku hii ya leo na kuendelea, kutoka siku ya ishirini na nne katika mwezi mwezi wa tisa, toka siku ile msingi wa hekalu la Bwana kuwekwa. Tafakarini hilo!
你们要追想此日以前,就是从这九月二十四日起,追想到立耶和华殿根基的日子。
19 Je, bado kuna mbegu katika ghala? Mzabibu, mti wa mtini, komamanga, na mti wa mzeituni havikuzaa matunda! lakini kutoka siku hii ya leo nitawabariki!”'
仓里有谷种吗?葡萄树、无花果树、石榴树、橄榄树都没有结果子。从今日起,我必赐福与你们。
20 Tena neno la Bwana likaja kwa mara ya pili kwa Haghai siku ya ishiri na nne katika mwezi kusema,
这月二十四日,耶和华的话二次临到哈该说:
21 “Sema na mkuu wa mkoa wa Yuda, Zerubabeli umwambie, 'Nitatikisa mbingu na dunia.
“你要告诉犹大省长所罗巴伯说:我必震动天地。
22 kwa hiyo nitaanhusha kiti cha falme na kuharibu nguvu ya falme za mataifa! nitaangusha magahari na wapandao; farasi na wapanda farasi wataanguka, kila mmoja kwa sababu ya upanga wa ndugu zake.
我必倾覆列国的宝座,除灭列邦的势力,并倾覆战车和坐在其上的。马必跌倒,骑马的败落,各人被弟兄的刀所杀。
23 Siku hiyo '-hivi ndivyo asema Bwana wa Majeshi- 'Nitakuchukua wewe Zerubabeli mwana wa Sheltieli, kama mtumishi wangu'- hivi ndivyo Bwana anavyosema. “Nitakutuma kama pete ya muhuri wangu, kwa sababu mimi ndiye niliyekuchagua!'- asema Bwana wa majeshi!”
万军之耶和华说:我仆人撒拉铁的儿子所罗巴伯啊,到那日,我必以你为印,因我拣选了你。这是万军之耶和华说的。”