< Mwanzo 6 >

1 Ikawa wakati watu walipoanza kuongezeka juu ya uso wa nchi na wana wa kike wakazaliwa kwao,
Watu walipoanza kuongezeka idadi katika uso wa dunia na watoto wa kike wakazaliwa kwao,
2 wana wa Mungu walipoona kuwa mabinti wa wanadamu ni wenye kuvutia. waliwachukua kuwa wake zao, kila waliye mchagua.
wana wa Mungu wakawaona kuwa hao binti za wanadamu walikuwa wazuri wa sura, wakaoa yeyote miongoni mwao waliyemchagua.
3 Yahwe akaema, “roho yangu haitasalia kwa mwanadamu milele, kwa kuwa wao ni nyama. Wataishi miaka 120.”
Ndipo Bwana akasema, “Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye ni wa kufa, siku zake zitakuwa miaka 120.”
4 Majitu makubwa yalikuwa juu ya uso wa nchi nyakati hizo, na hata baada ya hapo. Hii ilitokea wakati wana wa Mungu walipowaoa binti za wanadamu, na kupata watoto pamoja nao. Hawa walikuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa.
Wanefili walikuwako duniani siku hizo, na baadaye, hao wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu na kuzaa nao. Wanefili walikuwa mashujaa na watu waliojulikana wa zamani hizo.
5 Yahwe akaona kwamba uovu wa watu umezidi katika nchi, na kwamba mawazo ya mioyo yao daima inaelekea tu katika uovu.
Bwana akaona jinsi uovu wa mwanadamu ulivyokuwa mkubwa duniani, na ya kuwa kila mwelekeo wa mawazo ya moyo wake wakati wote ulikuwa mbaya tu.
6 Yahwe akajuta kuwa amemuumba mwanadamu juu ya nchi, na ikamuhuzunisha moyo wake.
Bwana akasikitika kwamba alimuumba mwanadamu duniani, moyo wa Mungu ukajaa masikitiko.
7 Kwa hiyo Yahwe akasema, “Nitamfutilia mbali mwanadamu ambaye nimemuumba katika uso wa nchi; mwanadamu na wanyama wakubwa, na vitambaavyo na ndege wa angani, kwa kuwa nimehuzunika kuwa nimeviumba.”
Kwa hiyo Bwana akasema, “Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemuumba kutoka kwenye uso wa dunia, wanadamu na wanyama, pamoja na viumbe vitambaavyo na ndege wa angani. Kwa maana nasikitika kuwaumba.”
8 Lakini Nuhu akapata neema ya upendeleo machoni pa Yahwe.
Lakini Noa akapata kibali machoni pa Bwana.
9 Kulikuwa na matukio kumuhusu Nuhu. Nuhu alikuwa mtu mwenye haki, na asiye na lawama miongoni mwa watu wa kipindi chake. Nuhu alitembea na Mungu.
Hivi ndivyo vizazi vya Noa. Noa alikuwa mtu wa haki, na mkamilifu miongoni mwa watu wa wakati wake, tena alitembea na Mungu.
10 Nuhu akafanyika baba wa wana watatu wa kiume: Shem, Ham na Yafeti.
Noa alikuwa na wana watatu: Shemu, Hamu na Yafethi.
11 Nchi iliharibika mbele za Mungu, na ikajaa ghasia.
Wakati huu dunia ilikuwa imejaa uharibifu na ukatili machoni pa Mungu.
12 Mungu akaiona nchi; tazama, ilikuwa imeharibika, kwa kuwa wote wenye mwili walikuwa wameharibu njia zao juu ya nchi.
Mungu akaona jinsi dunia ilivyoharibika, kwa maana watu wote duniani walikuwa wameharibu njia zao.
13 Mungu akamwambia Nuhu, “Nimeona kuwa sasa niwakati wa mwisho kwa wote wenye mwili, kwa kuwa inchi imejaa ghasia kutokana na wao. Hakika, nitawaharibu wao pamoja na nchi.
Kwa hiyo Mungu akamwambia Noa, “Nitawaangamiza watu wote, kwa kuwa dunia imejaa ukatili kwa sababu yao. Hakika mimi nitaangamiza watu pamoja na dunia.
14 Tengeneza safina ya mti wa mvinje kwa ajili yako. Tengeneza vyumba katika safina, na vifunike kwa lami ndani na nje.
Kwa hiyo jitengenezee safina kubwa kwa mbao za mvinje, tengeneza vyumba ndani yake na uipake lami ndani na nje.
15 Hivi ndivyo utakavyofanya: urefu wa safina dhiraa miatatu, upana wake dhiraa hamsini, kwenda juu kwake dhiraa thelathini.
Hivi ndivyo utakavyoitengeneza: Safina iwe na urefu wa dhiraa 300, upana wake dhiraa hamsini na kimo chake dhiraa thelathini.
16 Tengeneza paa la safina, na ulimalize kwa kipimo cha dhiraa kutoka juu ubavuni. Weka mlango katika ubavu wa safina na utengeneze dari ya chini, ya pili na ya tatu.
Itengenezee paa na umalizie safina kwa kuacha nafasi ya dhiraa moja juu. Weka mlango ubavuni mwa safina, na uifanye ya ghorofa ya chini, ya kati na ya juu.
17 Sikiliza, nimekaribia kuleta gharika ya maji juu ya nchi, kuharibu wenye mwili wote wakaao ndani ya nchi wenye pumzi ya uhai chini ya mbingu. Kila kitu kilichopo juu ya nchi kitakufa.
Nitaleta gharika ya maji juu ya nchi ili kuangamiza uhai wote chini ya mbingu, kila kiumbe chenye pumzi ya uhai ndani yake. Kila kitu juu ya nchi kitaangamia.
18 Lakini nitalifanya thabiti agano langu na wewe. Utaingia ndani ya safina, wewe, na wana wako wa kiume, na mke wako, pamoja na wake za wanao.
Lakini Mimi nitaweka Agano langu na wewe, nawe utaingia ndani ya Safina, wewe pamoja na mke wako, wanao na wake zao.
19 Kwa kila kiumbe hai chenye mwili, viwili vya kila aina utavileta ndani ya safina, ili visalie hai pamoja nawe, vya kike na vya kiume.
Utaingiza ndani ya Safina kila aina ya kiumbe hai wawili wawili, wa kiume na wa kike, ili kuwahifadhi hai pamoja na wewe.
20 Katika ndege kwa jinsi yake, na wanyama wakubwa kwa jinsi yake, kila kitambaacho ardhini kwa jinsi yake, viwili viwili vya kila aina vitakuja kwako ili viwe salama.
Wawili wa kila aina ya ndege, wa kila aina ya mnyama na wa kila aina ya kitambaacho ardhini watakuja kwako ili wahifadhiwe hai.
21 Kusanya kila aina ya chakula kinacholiwa kwa ajili yako na ukitunze, ili kwamba viwe chakula chako na chao.”
Utachukua kila aina ya chakula kitakacholiwa, na ukiweke akiba kama chakula kwa ajili yako na yao.”
22 Kwa hiyo Nuhu akafanya hivi. kulingana na yote ambayo Mungu alimuagiza, ndivyo alifanya.
Noa akafanya kila kitu kama vile Mungu alivyomwamuru.

< Mwanzo 6 >

The World is Destroyed by Water
The World is Destroyed by Water