< Mwanzo 49 >

1 Kisha Yakobo akawaita wana wake, na kusema: “Jikusanyeni pamoja, ili niwaambie yatakayowapata nyakati zijazo.
雅各伯叫了他的兒子們來說:「你們聚在一起,我要將你們日後所遇到的事告訴你們。
2 Kusanyikeni ninyi wenyewe na msikilize, enyi wana wa Yakobo. Msikilizeni Israeli, baba yenu.
雅各伯的兒子! 你們集合靜聽,靜聽你們父親以色列的話:
3 Reubeni, wewe ni mzaliwa wangu wa kwanza, nguvu zangu, na mwanzo wa uwezo wangu, aliyesalia katika heshima na nguvu.
勒烏本,你是我的長子,我的力量,我壯年的首生;你過於暴燥,過於激烈,
4 Asiyezuilika kama maji yarukayo, hautakuwa na umaharufu, kwa sababu ulikwenda juu ya kitanda cha baba yako. Hata ukakitia unajisi; ulikipanda kwa kuvizia.
沸騰有如滾水。你不能佔據首位,因為你侵犯了你父親的床第,上去玷污了我的臥榻。
5 Simoni na Lawi ni ndugu. Panga zao ni silaha za vurugu.
西默盎和肋未實是一對兄弟;他們的刀劍是殘暴的武器。
6 Ee nafsi yangu, usiingie barazani pao; usiingie katika mikutano yao, kwani moyo wangu unaheshima kubwa kwa ajili yao. Kwani katika hasira yao waliua watu. Iliwapendeza kuwakata visigino ng'ombe.
我的心靈決不加入他們的陰謀,我的心神決不參與他們的聚會;因為他們在盛怒下屠殺了人,任意割斷了牛的腿筋。
7 Hasira yao na ilaaniwe, kwani ilikuwa kali - na ukali wao, kwani ulikuwa ni katili. Nitawagawa katika Yakobo na kuwatawanya katika Israeli.
他們的忿怒這樣激烈,他們的狂暴這樣凶狠,實可詛咒! 我要使他們分散在雅各伯內,使他們散居在以色列中。
8 Yuda, ndugu zako watakusifu. Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba yako watainama mbele zako
猶大! 你將受你兄弟的讚揚;你的手必壓在你仇敵的頸上;你父親的兒子要向你俯首致敬。
9 Yuda ni mwana simba. Mwanangu, umetoka katika mawindo yako. Alisimama chini, alijikunyata kama simba, kama simba jike. Je nana atakayejaribu kumwamsha?
猶大是隻幼獅;我兒,你獵取食物後上來,屈身伏臥,有如雄獅,又如母獅,誰敢驚動﹖
10 Fimbo haitaondoka katika Yuda, wala fimbo ya utawala kutoka katika miguu yake, hata atakapo kuja Shilo. Mataifa yatamtii.
權杖不離猶大,柄杖不離他腳間,直到那應得權杖者來到,萬民都要歸順他。
11 Kumfunga punda wake kwenye mzabibu, na mwanapunda wake katika mzabibu mzuri, amefua mavazi yake katika divai, na kanzu yake katika damu ya vichala vya mzabibu.
他將自己的驢繫在葡萄樹上,將自己的驢駒拴在優美的葡萄樹上;在酒中洗自己的衣服,在葡萄汁中洗自己的外氅。
12 Macho yake yatakuwa mausi kama mvinyo, na meno yake meupe kama maziwa.
他的雙眼因酒而發紅,他的牙齒因乳而變白。
13 Zabuloni atakaa katika fukwe ya bahari. Atakuwa bandari kwa ajili ya meli, na mpaka wake utakuwa hata Sidoni.
則步隆將居於海濱,成為船隻停泊的口岸,與漆冬毗連。
14 Isakari ni punda mwenye nguvu, ajilazaye kati ya kondoo.
依撒加爾是匹壯驢,臥在圈中;
15 Anaona mahali pazuri pa kupumzikia na nchi ya kupendeza. Atainamisha bega lake kwa mzigo na kuwa mtumishi wake.
他覺得安居美好,地方優雅;便屈肩負重,成為服役的奴隸。
16 Dani atawaamua watu wake kama mojawapo ya makabila ya Israeli.
丹將如以色列的一個支派,衛護自己的人民。
17 Dani atakuwa nyoka kando ya njia, nyoka mwenye sumu aumaye visigino vya farasi katika njia, hivyo aongozaye farasi huanguka nyuma.
丹必似路邊的長蟲,道旁的毒蛇,咬傷馬蹄,使騎士向後跌下。
18 Ninaungoja wokovu wako, Yahwe.
上主! 我期待你的救援!
19 Gadi - wapanda farasi watamshambulia, lakini yeye atawapiga katika visigino vyao.
加得要受襲擊者襲擊,但他要襲擊他們的後隊。
20 Vyakula vya Asheri vitakuwa vingi, naye ataandaa vyakula vya kifalme.
阿協爾的食物肥美,將供給君王的佳餚。
21 Naftali ni dubu jike asiyefungwa; atakuwa na watoto wa dubu walio wazuri.
納斐塔里是隻被釋放的母鹿,發出悅耳的歌詠。
22 Yusufu ni tawi lizaalo, tawi lizaalo karibu na kijito, ambaye matawi yake yako juu wa ukuta.
若瑟是一株茂盛的果樹,一株泉旁茂盛的果樹;枝條蔓延牆頭。
23 Mpiga mishale atamshambulia na kumrushia na kumsumbua.
弓手令他苦惱,向他射擊,與他對敵;
24 Lakini upinde wake utakuwa imara, na mikono yake itakuwa hodari kwa sababu ya mikono ya Mwenyenguvu wa Yakobo, kwa ajili ya jina la Mchungaji, Mwamba wa Israeli.
但他的弓仍舊有力,他的手臂依然靈活;這是因了雅各伯的大能者之手,因了以色列的牧者和磐石之名;
25 Mungu wa baba yako atakusaidia na Mungu Mwenye enzi atakubariki kwa baraka mbinguni juu, baraka za vilindi vilivyo chini, na baraka za maziwa na tumbo.
這是因為你父親的天主扶助了你,全能者天主,以天上高處的祝福,以地下深淵蘊藏的祝福,以哺乳和生育的祝福,祝福了你。
26 Baraka za baba yako ni kuu kuliko baraka za milima ya zamani au vitu vilivyotamaniwa vya milima ya kale. Na viwe katika kichwa cha Yusufu, hata juu ya taji ya kifalme kichwani pa ndugu zake.
你父親的祝福,遠超過古山岳的祝福,永遠丘陵的願望;願這些祝福都降在若瑟頭上,降在他兄弟中被選者的額上。
27 Benjamini ni mbwamwitu mwenye njaa. Wakati wa asubuhi atalarua mawindo, na jioni atagawa mateka.”
本雅明是隻掠奪的豺狼:早上吞食獵物,晚上分贓。」
28 Haya ni makabila kumi na mbili ya Israeli. Hiki ndicho baba yao alichowambia alipowabariki. Aliwabariki kila mmoja kwa baraka iliyomstahili.
以上是以色列十二支派,以及他們的父親對他們所說的話。他祝福了他們,以適合每人的祝福,祝福了他們。
29 Kisha akawaelekeza na kuwaambia, “Ninakaribia kwenda kwa watu wangu. Mnizike pamoja na babu zangu katika pango lililoko katika shamba la Efroni Mhiti,
以後雅各伯又囑咐他們,對他們說:「我快要歸到我親族那裏去,你們應將我葬在赫特人厄斐龍田裏的山洞裏,與我的祖先在一起。
30 katika pango lililo katika shamba la Makpela, karibu na Mamre katika nchi ya Kanaani, shamba Ibrahimu alilolinunua kwa Efron Mhiti kwa ajili ya eneo la kuzikia.
這山洞是在客納罕地,面對瑪默勒的瑪革培拉的田內;這塊田原是亞巴郎由赫特人厄斐龍買了來作為私有墳地,
31 Pale walimzika Ibrahimu na Sara mkewe; pale wakamzika Isaka na Rebeka mkewe; na pale nikamzika Lea.
在那裏葬了亞巴郎和他的妻子撒辣,在那裏葬了依撒格和他的妻子黎貝加;我也在那裏葬了肋阿。
32 Shamba na pango lililomo lilinunuliwa kutoka kwa watu wa Hethi.”
這塊田地和其中的山洞是由赫特人買來的。」
33 Yakobo alipomaliza maagizo hayo kwa wanawe, akaiweka miguu yake kitandani, akakata roho, akawaendea watu wake
雅各伯給他的兒子們立完遺囑以後,便將腳縮到床上,斷氣而死,歸到他親族那裏去了。

< Mwanzo 49 >