< Mwanzo 36 >

1 Hivi ndivyo vizazi vya Esau (aliyeitwa pia Edom).
エサウ、すなわちエドムの系図は次のとおりである。
2 Esau akachukua wakeze kutoka kwa Wakanaani. Hawa walikuwa wake zake: Ada binti Eloni Mhiti; Oholibama binti Ana, mjukuu wa Zibeoni Mhivi; na
エサウはカナンの娘たちのうちから妻をめとった。すなわちヘテびとエロンの娘アダと、ヒビびとヂベオンの子アナの娘アホリバマとである。
3 Basemathi, binti Ishmaeli, dada wa Nebayothi.
また、イシマエルの娘ネバヨテの妹バスマテをめとった。
4 Ada akamzaa Elifazi kwa Esau, na Basemathi akamzaa Reueli.
アダはエリパズをエサウに産み、バスマテはリウエルを産み、
5 Oholibama akamzaa Yeushi, Yalamu, na Kora. Hawa walikuwa wana wa Esau waliozaliwa kwake katika nchi ya Kananaani.
アホリバマはエウシ、ヤラム、コラを産んだ。これらはエサウの子であって、カナンの地で彼に生れた者である。
6 Esau akawachukua wakeze, wanawe, binti zake, na watu wote wa nyumba yake, mifugo wake - wanyama wake wote, na mali yake yote, aliyokuwa amekusanya katika nchi ya Kanaani, na akaenda katika nchi iliyoko mbali kutoka kwa Yakobo nduguye.
エサウは妻と子と娘と家のすべての人、家畜とすべての獣、またカナンの地で獲たすべての財産を携え、兄弟ヤコブを離れてほかの地へ行った。
7 Alifanya hivi kwa sababu mali zao zilikuwa nyingi sana kwa wao kuishi pamoja. Nchi waliyokuwa wamekaa isingeweza kuwafaa kwa mifugo yao.
彼らの財産が多くて、一緒にいることができなかったからである。すなわち彼らが寄留した地は彼らの家畜のゆえに、彼らをささえることができなかったのである。
8 Hivyo Esau, aliyejulikana pia kama Edomu, akakaa katika nchi ya kilima Seiri.
こうしてエサウはセイルの山地に住んだ。エサウはすなわちエドムである。
9 Hivi ndivyo vizazi vya Esau, babu wa Waedomu katika nchi ya mlima Seiri.
セイルの山地におったエドムびとの先祖エサウの系図は次のとおりである。
10 Haya yalikuwa majina ya wana wa Esau: Elifazi mwana wa Ada, mkewe Esau; Reueli mwana wa Basemathi, mkewe Esau.
エサウの子らの名は次のとおりである。すなわちエサウの妻アダの子はエリパズ。エサウの妻バスマテの子はリウエル。
11 Wana wa Elifazi walikuwa Temani, Omari, Zefo, Gatamu, na Kenazi.
エリパズの子らはテマン、オマル、ゼポ、ガタム、ケナズである。
12 Timna, suria wa Elifazi, mwana wa Esau, akamzaa Amaleki. Hawa walikuwa wajukuu wa Ada, mkewe Esau.
テムナはエサウの子エリパズのそばめで、アマレクをエリパズに産んだ。これらはエサウの妻アダの子らである。
13 Hawa walikuwa wana wa Reueli: Nahathi, Zera, Shama, na Miza. Hawa walikuwa wajukuu wa Basemathi, mkewe Esau.
リウエルの子らは次のとおりである。すなわちナハテ、ゼラ、シャンマ、ミザであって、これらはエサウの妻バスマテの子らである。
14 Hawa walikuwa wana wa Oholibama, mkewe Esau, aliyekuwa binti Ana na mjukuu wa Zibeoni. Alimzalia Esau Yeushi, Yalamu, na Kora.
ヂベオンの子アナの娘で、エサウの妻アホリバマの子らは次のとおりである。すなわち彼女はエウシ、ヤラム、コラをエサウに産んだ。
15 Hizi zilikuwa koo kati ya vizazi vya Esau: uzao wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau: Temani, Omari, Zefo, Kenazi, Kora,
エサウの子らの中で、族長たる者は次のとおりである。すなわちエサウの長子エリパズの子らはテマンの族長、オマルの族長、ゼポの族長、ケナズの族長、
16 Gatamu, na Amaleki. Hivi vilikuwa vizazi vya koo kutoka kwa Elifazi katika nchi ya Edomu. Walikuwa wajukuu wa Ada.
コラの族長、ガタムの族長、アマレクの族長である。これらはエリパズから出た族長で、エドムの地におった。これらはアダの子らである。
17 Hizi zilikuwa koo kutoka kwa Reueli, mwana wa Esau: Nahathi, Zera, Shama, Miza. Hizi zilikuwa koo kutoka kwa Reueli katika nchi ya Edomu. Walikuwa wajukuu wa Basemathi, mkewe Esau.
エサウの子リウエルの子らは次のとおりである。すなわちナハテの族長、ゼラの族長、シャンマの族長、ミザの族長。これらはリウエルから出た族長で、エドムの地におった。これらはエサウの妻バスマテの子らである。
18 Hizi zilikuwa koo za Oholibama, mkewe Esau: Yeushi, Yalamu, Kora. Hizi ni koo zilizotoka kwa Oholibama mkewe Esau, binti Ana.
エサウの妻アホリバマの子らは次のとおりである。すなわちエウシの族長、ヤラムの族長、コラの族長。これらはアナの娘で、エサウの妻アホリバマから出た族長である。
19 Hawa walikuwa wana wa Esau na koo zao.
これらはエサウすなわちエドムの子らで、族長たる者である。
20 Hawa walikuwa wana wa Seiri Mhori, wenyeji wa nchi hiyo: Lotani, Shobali, Zibeoni, Ana,
この地の住民ホリびとセイルの子らは次のとおりである。すなわちロタン、ショバル、ヂベオン、アナ、
21 Dishoni, Ezeri, na Dishani. Hizi zilikuwa koo the Wahori, wenyeji wa Seiri katika nchi ya Edomu.
デション、エゼル、デシャン。これらはセイルの子ホリびとから出た族長で、エドムの地におった。
22 Wana wa Lotani walikuwa Hori na Hemani, na Timna alikuwa dada wa Lotani.
ロタンの子らはホリ、ヘマムであり、ロタンの妹はテムナであった。
23 Hawa walikuwa wana wa Shobali: Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo, na Onamu.
ショバルの子らは次のとおりである。すなわちアルワン、マナハテ、エバル、シポ、オナム。
24 Hawa walikuwa wana wa Zibeoni: Aia na Ana. Huyu ndiye Ana aliyeona chemichemi za moto nyikani, alipokuwa akichunga punda wa Zibeoni babaye.
ヂベオンの子らは次のとおりである。すなわちアヤとアナ。このアナは父ヂベオンのろばを飼っていた時、荒野で温泉を発見した者である。
25 Hawa walikuwa watoto wa Ana: Dishoni na Oholibama, binti Ana.
アナの子らは次のとおりである。すなわちデションとアホリバマ。アホリバマはアナの娘である。
26 Hawa walikuwa wana wa Dishoni: Hemdani, Eshbani, Ithrani, na Kerani.
デションの子らは次のとおりである。すなわちヘムダン、エシバン、イテラン、ケラン。
27 Hawa walikuwa wana wa Ezeri: Bilhani, Zaavani, na Akani.
エゼルの子らは次のとおりである。すなわちビルハン、ザワン、アカン。
28 Hawa walikuwa wana wa Dishani: Uzi na Arani.
デシャンの子らは次のとおりである。すなわちウズとアラン。
29 Hizi zilikuwa koo za Wahori: Lotani, Shobali, Zibeoni, na Ana,
ホリびとから出た族長は次のとおりである。すなわちロタンの族長、ショバルの族長、ヂベオンの族長、アナの族長、
30 Dishoni, Ezeri, Dishani: hizi zilikuwa koo za Wahori, kulingana na ukoo ulivyoorodheshwa katika nchi ya Seiri.
デションの族長、エゼルの族長、デシャンの族長。これらはホリびとから出た族長であって、その氏族に従ってセイルの地におった者である。
31 Hawa walikuwa wafalme waliomiliki katika nchi ya Edomu kabla ya mfalme yeyote kumilika juu ya Waisraeli:
イスラエルの人々を治める王がまだなかった時、エドムの地を治めた王たちは次のとおりである。
32 Bela mwana wa Beori, alitawala huko Edomu, na jina la mji wake lilikuwa Dinhaba.
ベオルの子ベラはエドムを治め、その都の名はデナバであった。
33 Bela alipofariki, kisha Yobabu mwana wa Zera kutoka Bozra, akatawala mahali pake.
ベラが死んで、ボズラのゼラの子ヨバブがこれに代って王となった。
34 Yobabu alipofariki, Hushamu aliyekuwa wa nchi ya Watemani, akatawala mahali pake.
ヨバブが死んで、テマンびとの地のホシャムがこれに代って王となった。
35 Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi aliyewashinda Wamidiani katika nchi ya Moabu, akatawala mahali pake. Jina la mji wake lilikuwa Avithi.
ホシャムが死んで、ベダデの子ハダデがこれに代って王となった。彼はモアブの野でミデアンを撃った者である。その都の名はアビテであった。
36 Hadadi alipofariki, kisha Samla wa Masreka akatawala mahali pake.
ハダデが死んで、マスレカのサムラがこれに代って王となった。
37 Samla alipofariki, kisha Shauli wa Rehobothi kando ya mto alitawala mahali pake.
サムラが死んでユフラテ川のほとりにあるレホボテのサウルがこれに代って王となった。
38 Shauli alipofariki, kisha Baali Hanani mwana wa Akbori akatawala mahali pake.
サウルが死んでアクボルの子バアル・ハナンがこれに代って王となった。
39 Baali Hanani mwana wa Akbori, alipokufa, kisha Hadari akatawala mahali pake. Jina la mji wake lilikuwa Pau. Jina la mkewe lilikuwa Mehetabeli, binti Matredi, mjukuu wa Me Zahabu.
アクボルの子バアル・ハナンが死んで、ハダルがこれに代って王となった。その都の名はパウであった。その妻の名はメヘタベルといって、メザハブの娘マテレデの娘であった。
40 Haya ndiyo yalikuwa majina ya wakuu wa koo kutoka uzao wa Esau, kwa kufuata koo zao na maeneo yao, kwa majina yao: Timna, Alva, Yethethi,
エサウから出た族長の名は、その氏族と住所と名に従って言えば次のとおりである。すなわちテムナの族長、アルワの族長、エテテの族長、
41 Oholibama, Ela, Pinoni,
アホリバマの族長、エラの族長、ピノンの族長、
42 Kenazi, Temani, Mbza,
ケナズの族長、テマンの族長、ミブザルの族長、
43 Magdieli, na Iramu. Hawa walikuwa wakuu wa ukoo wa Edomu, kwa kufuata makao yao katika nchi waliyomiliki. Nao ni Esau, baba wa Waedomu.
マグデエルの族長、イラムの族長。これらはエドムの族長たちであって、その領地内の住所に従っていったものである。エドムびとの先祖はエサウである。

< Mwanzo 36 >