< Mwanzo 23 >

1 Sara akaishi mika mia moja na ishirini na saba. Hii ndiyo ilikuwa ni miaka ya maisha ya Sara.
撒拉享寿一百二十七岁,这是撒拉一生的岁数。
2 Sara akafa katika Kiriathi Arba, ambayo ni Hebroni, katika nchi ya Kanaani. Abraham akaomboleza na kumlilia Sara.
撒拉死在迦南地的基列·亚巴,就是希伯 。亚伯拉罕为她哀恸哭号。
3 Kisha Abraham akainuka na kutoka kwa mkewe aliye kufa, akanena na watoto wa kiume wa Hethi, akisema,
后来亚伯拉罕从死人面前起来,对赫人说:
4 “Mimi ni mgeni kati yenu. Tafadhari nipatieni mahali pa kuzikia miongoni mwenu, ili kwamba niweze kuzika wafu wangu.”
“我在你们中间是外人,是寄居的。求你们在这里给我一块地,我好埋葬我的死人,使她不在我眼前。”
5 Wana wa Hethi wakamjibu Abraham, wakasema,
赫人回答亚伯拉罕说:
6 “Tusikilize, bwana wangu. Wewe ni mwana wa Mungu miongoni mwetu. Zika wafu wako katika makaburi yetu utakayochagua. Hakuna miongoni mwetu atakaye kuzuilia kaburi lake, kwa ajili ya kuzikia wafu wako.”
“我主请听。你在我们中间是一位尊大的王子,只管在我们最好的坟地里埋葬你的死人;我们没有一人不容你在他的坟地里埋葬你的死人。”
7 Abraham akainuka na kusujudu chini kwa watu wa nchi ile, kwa wana wa Hethi.
亚伯拉罕就起来,向那地的赫人下拜,
8 Akawaambia, akisema, “ikiwa mmekubali mimi kuzika wafu wangu, ndipo nisikilizeni, msihini Efroni mwana wa Sohari kwa ajili yangu.
对他们说:“你们若有意叫我埋葬我的死人,使她不在我眼前,就请听我的话,为我求琐辖的儿子以弗 ;
9 Mwambieni aniuzie pango la Makpela, ambalo analimiliki, ambalo liko mwishoni mwa shamba lake. Kwa bei kamili aniuzie waziwazi mbele ya watu kama miliki ya kuzikia.”
把田头上那麦比拉洞给我;他可以按着足价卖给我,作我在你们中间的坟地。”
10 Efroni alikuwa ameketi miongoni mwa wana wa Hethi, hivyo Efroni Mhiti akamjibu Abraham alipowasikia wana wa Hethi, wote ambao walikuwa wamekuja langoni mwa mji wake, akasema,
当时以弗 正坐在赫人中间。于是,赫人以弗 在城门出入的赫人面前对亚伯拉罕说:
11 “Hapana, bwana wangu, nisikilize. Ninakupatia shamba na pango ambalo limo ndani yake. Ninakupatia mbele ya wana wa watu wangu. Ninakupatia uzike wafu wako.”
“不然,我主请听。我送给你这块田,连田间的洞也送给你,在我同族的人面前都给你,可以埋葬你的死人。”
12 Kisha Abraham akasujudu chini mbele ya watu wa nchi ile.
亚伯拉罕就在那地的人民面前下拜,
13 Akamwambia Efroni watu wa nchi ile wakisikiliza, akasema, ikiwa uko radhi, tafadhari nisikilize. Nitalipia shamba. Chukua fedha kwangu, na nitazika wafu wangu pale.”
在他们面前对以弗 说:“你若应允,请听我的话。我要把田价给你,求你收下,我就在那里埋葬我的死人。”
14 Efroni akamjibu Abraham, akisema,
以弗 回答亚伯拉罕说:
15 “Tafadhari bwana wangu, nisikilize. Kipande cha ardhi kinathamani ya shekeli mia nne za fedha, na hiyo ni kitu gani kati yangu mimi na wewe? wazike wafu wako.”
“我主请听。值四百舍客勒银子的一块田,在你我中间还算什么呢?只管埋葬你的死人吧!”
16 Abraham akamsikiliza Efroni na akampimia Efroni kiwango cha fedha alizosema mbele ya wana wa Helthi wakisikiliza, shekeli mia nne za fedha, kwa mujibu wa viwango vya vipimo vya kibiashara.
亚伯拉罕听从了以弗 ,照着他在赫人面前所说的话,把买卖通用的银子平了四百舍客勒给以弗 。
17 Kwa hiyo shamba la Efroni, lililokuwa katika Makpela, mbele ya Mamre, shamba pamoja na pango lililokuwamo ndani yake na miti yote iliyokuwamo ndani ya shamba na iliyokuwa mpakani ikatolewa
于是,麦比拉、幔利前、以弗 的那块田和其中的洞,并田间四围的树木,
18 kwa Abraham kwa njia ya manunuzi mbele ya wana wa Hethi, na mbele ya wote waliokuja malangoni pa mji wake.
都定准归与亚伯拉罕,乃是他在赫人面前并城门出入的人面前买妥的。
19 Baada ya haya, Abraham akamzika Sara mkewe katika pango la shamba la Makpela, lililo mbele ya Mamre, ambayo ni Hebroni, katika nchi ya Kanaani.
此后,亚伯拉罕把他妻子撒拉埋葬在迦南地幔利前的麦比拉田间的洞里。(幔利就是希伯 )。
20 Kwa hiyo shamba pamoja na pango likatolewa na wana wa Hethi kwa Abraham kama milki na eneo la kuzikia.
从此,那块田和田间的洞就借着赫人定准归与亚伯拉罕作坟地。

< Mwanzo 23 >