< Wagalatia 1 >

1 Mimi ni Paulo mtume. Mimi sio mtume kutoka kwa wanadamu wala kupitia kwa mwanadamu, lakini kupitia kwa Yesu Kristo na Mungu Baba aliyemfufua kutoka kwa wafu.
作使徒的保羅(不是由於人,也不是藉着人,乃是藉着耶穌基督,與叫他從死裏復活的父上帝)
2 Pamoja na ndugu wote na mimi, ninayaandikia makanisa ya Galatia.
和一切與我同在的眾弟兄,寫信給加拉太的各教會。
3 Neema iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo,
願恩惠、平安從父上帝與我們的主耶穌基督歸與你們!
4 aliyejitoa mwenyewe kwa ajili ya dhambi zetu ili kwamba atukomboe na nyakati hizi za uovu, kutokana na mapenzi ya Mungu wetu na Baba. (aiōn g165)
基督照我們父上帝的旨意,為我們的罪捨己,要救我們脫離這罪惡的世代。 (aiōn g165)
5 Kwake uwe utukufu milele na milele. (aiōn g165)
但願榮耀歸於上帝,直到永永遠遠。阿們! (aiōn g165)
6 Ninashangaa kwamba mnageukia haraka kwenye injili nyingine. Ninashangaa kwamba mnageukia mbali kutoka kwake yeye aliyewaita kwa neema ya Kristo.
我希奇你們這麼快離開那藉着基督之恩召你們的,去從別的福音。
7 Hakuna injili nyingine, lakini kuna baadhi ya watu wanao wasababishieni nyinyi matatizo na kutaka kubadilisha injili ya Kristo.
那並不是福音,不過有些人攪擾你們,要把基督的福音更改了。
8 Lakini hata kama ni sisi au malaika kutoka mbinguni atatangaza kwenu injili tofauti na ile tuliyoitangaza kwenu, na alaaniwe.
但無論是我們,是天上來的使者,若傳福音給你們,與我們所傳給你們的不同,他就應當被咒詛。
9 Kama tulivyo sema mwanzoni, na sasa nasema tena, “Kama kuna mtu atawatangazia kwenu injili tofauti na mliyoipokea, na alaaniwe.”
我們已經說了,現在又說,若有人傳福音給你們,與你們所領受的不同,他就應當被咒詛。
10 Kwani sasa hivi ninatafuta uthibitisho wa watu au Mungu? Ninatafuta kuwafurahisha wanadamu? Kama ninaendelea kujaribu kuwafurahisha wanadamu, mimi sio mtumishi wa Kristo.
我現在是要得人的心呢?還是要得上帝的心呢?我豈是討人的喜歡嗎?若仍舊討人的喜歡,我就不是基督的僕人了。
11 Ndugu, ninataka ninyi mjue kwamba injili niliyoitangaza haitokani na wanadamu.
弟兄們,我告訴你們,我素來所傳的福音不是出於人的意思。
12 Sikuipokea kutoka kwa mtu, wala sikufundishwa. Badala yake, ilikuwa ni kwa ufunuo wa Yesu Kristo kwangu.
因為我不是從人領受的,也不是人教導我的,乃是從耶穌基督啟示來的。
13 Mmekwisha sikia juu ya maisha yangu ya nyuma katika dini ya Kiyahudi, jinsi nilivyokuwa nikilitesa kwa ukali kanisa la Mungu zaidi ya kipimo na kuliteketeza.
你們聽見我從前在猶太教中所行的事,怎樣極力逼迫殘害上帝的教會。
14 Nilikuwa nimeendelea katika Dini ya Kiyahudi zaidi ya ndugu zangu wengi Wayahudi. Nilikuwa na bidii sana katika tamaduni za baba zangu.
我又在猶太教中,比我本國許多同歲的人更有長進,為我祖宗的遺傳更加熱心。
15 Lakini Mungu alipendezwa kunichagua mimi kutoka tumboni mwa mama. Aliniita mimi kupitia neema yake
然而,那把我從母腹裏分別出來、又施恩召我的上帝,
16 kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili kwamba nimtangaze yeye miongoni mwa watu wa mataifa. Wala sikutafuta ushauri wa mwili na damu
既然樂意將他兒子啟示在我心裏,叫我把他傳在外邦人中,我就沒有與屬血氣的人商量,
17 na sikupanda kwenda Yerusalem kwa wale waliokuwa mitume kabla yangu. Badala yake nilienda Uarabuni na baadae kurudi Damesiki.
也沒有上耶路撒冷去見那些比我先作使徒的,惟獨往阿拉伯去,後又回到大馬士革。
18 Kisha baada ya miaka mitatu nilipanda kwenda Yerusalemu kumtembelea Kefa, nikakaa naye kwa siku kumi na tano.
過了三年,才上耶路撒冷去見磯法,和他同住了十五天。
19 Lakini sikuona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndungu yake na Bwana.
至於別的使徒,除了主的兄弟雅各,我都沒有看見。
20 Tazama, mbele za Mungu, sidanganyi kwa kile niandikacho kwenu.
我寫給你們的不是謊話,這是我在上帝面前說的。
21 Kisha nilikwenda mikoa ya Shamu na Kilikia.
以後我到了敘利亞和基利家境內。
22 Sikuwa najulikana kwa macho kwa makanisa ya Uyahudi yale yaliyokuwa katika Kristo,
那時,猶太信基督的各教會都沒有見過我的面。
23 lakini walikuwa wakisikia tu, “Yeye aliyekuwa akitutesa sasa anatangaza imani aliyokuwa akiiharibu.”
不過聽說那從前逼迫我們的,現在傳揚他原先所殘害的真道。
24 Walikuwa wakimtukuza Mungu kwa ajili yangu.
他們就為我的緣故,歸榮耀給上帝。

< Wagalatia 1 >