< Wagalatia 3 >
1 Wagalatia wajinga, ni jicho gani ovu lililowaharibu? Je Yesu Kristo hakuoneshwa kama msulubiwa mbele ya macho yenu?
Bhagalatia bhajinga, lihu leleku la uovu lalibhahalibu? Je Yesu Kristu alasibhu lepi katya msulubibwa palongolo pa mihu gha yhomo?
2 Mimi nataka tu kufahamu hili kutoka kwenu. Je mlimpokea Roho kwa matendo ya sheria au kwa kuamini kile mlichosikia?
Nene nilonda tu kumanya ele kuhomela kwa muenga. Je mwapokili Roho kwa matendo gha Sheria au ndo mwaamini kela kamwapeliki?
3 Je, ninyi ni wajinga kiasi hiki? Je mlianza katika Roho ili mmalize katika mwili?
Ko, muenga ni bhajinga kiasi ekhe? ko mwayandili mu Roho ili mmalai mu mbhele?
4 Je mliteseka kwa mambo mengi bure, kama kweli yalikuwa ya bure?
Ko mwatesiki kwa mambo mingi mebhwa, katya kueli ghayele gha mebhwa?
5 Je yeye atoaye Roho kwenu na kutenda matendo ya nguvu kati yenu hufanya kwa matendo ya sheria au kwa kusikia pamoja na imani?
Ko muene yaipisya Roho kwa muenga ni kubhomba matendo gha nghofo kwa yhomo iketa kwa matendo gha sheria au kwa kup'etela pamonga ni imani?
6 Abraham “Alimwamini Mungu akahesabiwa kuwa mwenye haki”.
Abraham “Amwamini K'yara ahesabibhu kujo mwenye haki”.
7 Kwa namna ile ile eleweni kwamba, wale ambao wanaamini ni watoto wa Abrahamu.
Kwa namna yela yela muyelewahi ya ndabha, bhala bhabhiamini yakuwa ni bhana bha Abraham.
8 Andiko lilitabiri kwamba Mungu angewahesabia haki watu wa mataifa kwa njia ya imani. Injili ilihubiriwa kwanza kwa Abrahamu: “katika wewe mataifa yote yatabarikiwa”.
Liyandiku latabilibhu yakuwa K'yara ngabhahesabili haki bhanu bha mataifa kwa njela ya imani. Injili yahubilibhu hosi kwa Abraham:”Kwa bhebhe mataifa ghoa ghibalikibhwa”.
9 Ili baadaye wale ambao wana imani wabarikiwe pamoja na Abrahamu, ambaye alikuwa na imani.
Ili kabhele bhabhayele niimani bhabalikibhuayi pamonga ni Abraham, yaayele ni imani.
10 Wale ambao wanategemea matendo ya sheria wako chini ya laana. Kwa kuwa imeandikwa, “Amelaaniwa kila mtu ambaye hashikamani na mambo yote yaliyoandikwa katika kitabu cha sheria, kuyatenda yote.”
Bhala bhoa bhabhitegemela matendo gha sheria bhayele pasi mu laana. Kwa ndabha iyandikibhu, “Alanibhu kila munu yaishikamanahee ni mambo ghoa ghaghayandikibhu mukitabu ka sheria, kughabhomba ghoa.”
11 Sasa ni wazi kwamba Mungu hamhesabii haki hata mmoja kwa sheria, kwa kuwa “Mwenye haki ataishi kwa imani”.
Henu ndo bhuasi yakuwa K'yara akamwesabilahee haki hata immonga musheria, kwa ndabha, “Yaayele ni haki alaishi ki imani”
12 Sheria haitokani na imani, lakini badala yake “Ambaye hufanya mambo haya katika sheria, ataishi kwa sheria.”
Sheria yihomelahe ni imani, Badala yaki “Yaifwanyai mambo agha kup'etela sheria, alaishi kisheria”.
13 Kristo alitukomboa sisi kutoka katika laana ya sheria wakati alipofanyika laana kwa ajili yetu. Kwa kuwa imeandikwa, “Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti.”
istu atukombhuili tete kuhomela mu laana ya sheria yapayafwanyikai laana kwajia yhoto. Kwa ndabha iyandikibhu, “Alanibhuayi” kila munu yaibinai munani mulibehe.”
14 Lengo lilikuwa kwamba, baraka ambazo zilikuwa kwa Ibrahimu zingekuja kwa watu wa mataifa katika Kristo Yesu, ili kwamba tuweze kupokea ahadi ya Roho kupitia imani.
Lilengo layele ya ndabha, baraka ambasyo sasa yele kwa Ibrahimu ngasaidai kwa bhanu bhamataifa kup'etela Yesu Kristu, yakuwa tubhwesyai kuyhopa ahadi ya Roho kup'etela imani.
15 Ndugu, ninazungumza kwa namna ya kibinadamu. Hata wakati ambapo agano la kibinadamu limekwisha kuwekwa imara, hakuna awezaye kupuuza au kuongezea.
Ndongo, nikabhajobhela na kibinadamu. Kabhele magono ambapo agano la kibinadamu palimalikai kubhekibhwa imara, ayelepi yaibhwesyai kupuuza au kuyongesela.
16 Sasa ahadi zilisemwa kwa Ibrahim na kwa kizazi chake. Haisemi, “kwa vizazi,” kumaanisha wengi, bali badala yake kwa mmoja pekee, “kwa kizazi chako,” ambaye ni Kristo.
Henu ahadi sajobhibhu kwa Ibrahimu ni kizazikya muene. Yijobhahee, “Kwa vizazi,” kumaanisya bhingi, badala yaki kwa mmonga yumuene, “Kwa kizazi kyako,” ambaye ndo Kristu.
17 Sasa nasema hivi, sheria ambayo ilikuja miaka 430 baadaye, haiondoi agano la nyuma lililowekwa na Mungu.
Henu nijobha nah, sheria ya yahidili miaka 430 badaye, yibhosya lepi agano la kunyuma lalibheki bhusima ni K'yara.
18 Kwa kuwa kama urithi ungelikuja kwa njia ya sheria, usingekuwa tena umekuja kwa njia ya ahadi. Lakini Mungu aliutoa bure kwa Ibrahimu kwa njia ya ahadi.
Yandabha kujo ulisi ngawahidili ki njela ya sheria, ngaiyelepi kabhele kuhida kwa njela ya ahadi. Ndabha K'yara apisili mebhwa kwa Ibrahimu kwa njela ya ahadi.
19 Kwa nini sasa sheria ilitolewa? Iliongezwa kwa sababu ya makosa, mpaka mzao wa Ibrahimu aje kwa wale ambao kwao alikuwa ameahidiwa. Sheria iliwekwa katika shinikizo kupitia malaika kwa mkono wa mpatanishi.
Kwandayakiki henu sheria yapisibhu? Yayongisibhu ndabha ya makosa, mpaka mzao wa Ibrahimu ulota kwa bhala ambabho kwa bhene amalili kuhaidibhwa. Sheria yabhekibhu ki shinikizo kup'etela malaika kwa kibhoko Kya kupatanisya.
20 Sasa mpatanishi humaanisha zaidi ya mtu mmoja, bali Mungu ni mmoja peke yake.
Henu mpatanishi imaanisya zaidi ya munu mmonga, ndo K'yara yumuene.
21 Kwa hiyo je sheria iko kinyume na ahadi za Mungu? La hasha! Kwa kuwa kama sheria iliyokuwa imetolewa ilikuwa na uwezo wa kuleta uzima, haki ingepatikana kwa sheria.
Kwa ele ko sheria iyele kinyume ni ahadi sa K'yara? La hasha! kwa ndabha sheria yaiyele ipisibhu iyele ni ubhueso wa kuleta usima, haki ngaipatikene kwa sheria.
22 Lakini badala yake, andiko limefunga mambo yote chini ya dhambi. Mungu alifanya hivi ili kwamba ahadi yake ya kutuokoa sisi kwa imani katika Yesu Kristo iweze kupatikana kwa wale wanao amini.
Badala yaki, liyandiku lifungili mambo ghoa pasi mu thambi. K'yara aketili naa ili ya ndabha ahadi ya muene ya kutookola tete kwa imani kup'etela Yesu Kristu lbhuesyai kupatikana kwa bhala bhabhiamini.
23 Lakini kabla ya imani katika Kristo haijaja, tulikuwa tumefungwa na kuwa chini ya sheria hadi uje ufunuo wa imani.
Kabula ya imani ya Kristu kuhida, twayele tufungibhu ni kuya pasi pa sheria hadi pawihidai ufunuo was imani.
24 Kwa hiyo sheria ilifanyika kiongozi wetu hadi Kristo alipokuja, ili kwamba tuhesabiwe haki kwa imani.
Kwa ele sheria yafwanyiki kwa kiongozi wa yhoto hadi Kristu pahaaidayi, ndabha tuhesabibhuayi mu haki ni mwimani.
25 Sasa kwa kuwa imani imekuja, hatuko tena chini ya mwangalizi.
Henu yandabha imani ihidili, tuyelepi kabhele pasi pabha angalizi.
26 Kwa kuwa ninyi nyote ni watoto wa Mungu kupitia imani katika Kristo Yesu.
Kwa ndabha muenga mwabhoa ndo bhana bha K'yara kup'etela imani ni Kristu Yesu.
27 Wote ambao mlibatizwa katika Kristo mmejivika Kristo.
Mwabhoa bhambatizibhu kup'etela Kristu mmjifwekili Kristu.
28 Hakuna Myahudi wala Myunani, mtumwa wala huru, mwanaume wala mwanamke, kwa kuwa ninyi nyote ni mmoja katika Kristo Yesu.
Ayelepi Myaudi wala Myunani, n'tumwa wala huru, bhagosi wala bhadala, kwandabha muenga mwabhoa n'do bhamonga kup'etela Kristu Yesu.
29 Kama ninyi ni wa Kristo, basi ni uzao wa Ibrahimu, warithi kwa mujibu wa ahadi.
Kama muenga ndo bha Kristu, basi ndo uzao wa Ibrahimu, bharithi mu jibu wa ahadi.