< Wagalatia 1 >
1 Mimi ni Paulo mtume. Mimi sio mtume kutoka kwa wanadamu wala kupitia kwa mwanadamu, lakini kupitia kwa Yesu Kristo na Mungu Baba aliyemfufua kutoka kwa wafu.
Nene na Paulo na n'tume. Nene na n'tume lepi kuhomela kwa bhanadamu, ila kup'etela Yesu Kristu ni K'yara Dadi yaamfufuili kuhomela KU wafu.
2 Pamoja na ndugu wote na mimi, ninayaandikia makanisa ya Galatia.
Pamonga ni bhalongo bhangu bhoa ni nene, nikabhayandikila makanisa gha Bhagalatia.
3 Neema iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo,
Neema iyelai kwa yhomo ni amani yayihomela kwa K'yara Dadi wayhoto ni Bwana Yesu Kristu.
4 aliyejitoa mwenyewe kwa ajili ya dhambi zetu ili kwamba atukomboe na nyakati hizi za uovu, kutokana na mapenzi ya Mungu wetu na Baba. (aiōn )
Yajipisili yumuene kwajia thambi sayhoto ndabha abhuesyakutokombola mu magono agha ghauovu, kup'etela mapenzi ghaki K'yara wayhoto na ni Dadi. (aiōn )
5 Kwake uwe utukufu milele na milele. (aiōn )
Kwa muene uyela utukufu milele na milele. (aiōn )
6 Ninashangaa kwamba mnageukia haraka kwenye injili nyingine. Ninashangaa kwamba mnageukia mbali kutoka kwake yeye aliyewaita kwa neema ya Kristo.
Nishangala ndabha mwigeukila haraka mu injili yhenge. Nishangala kabhele mwigeukila patali kuhomela kwa muene yaabhakutili kwa neema said Kristu.
7 Hakuna injili nyingine, lakini kuna baadhi ya watu wanao wasababishieni nyinyi matatizo na kutaka kubadilisha injili ya Kristo.
Iyelepi injili yhenge, ila bhayele baadhi ya bhanu bhabhilonda kubhasababishila muenga matatisu ni kulonda kubadilisya injili ya kristu.
8 Lakini hata kama ni sisi au malaika kutoka mbinguni atatangaza kwenu injili tofauti na ile tuliyoitangaza kwenu, na alaaniwe.
Hata Kama kujobhela tete au malaika kuhomela kumbinguni alatangasya kwa muenga injili yayele tofauti ni yhela yatatangasyai kwa muenga, na alanibhuayi.
9 Kama tulivyo sema mwanzoni, na sasa nasema tena, “Kama kuna mtu atawatangazia kwenu injili tofauti na mliyoipokea, na alaaniwe.”
Katya katajobhai kamuandi, ni henu mjobha kabhele,”Katya ayele munu alabhatangasila kwa muenga injili yaiyele tofauti na ya mwapokili, alanibhuayi”.
10 Kwani sasa hivi ninatafuta uthibitisho wa watu au Mungu? Ninatafuta kuwafurahisha wanadamu? Kama ninaendelea kujaribu kuwafurahisha wanadamu, mimi sio mtumishi wa Kristo.
Kwani henu nilonda uthibitisho wa bhanu au K'yara? nilonda kubhafulaisya muenga bhanadamu? Katya niyendelela kubhajalibu kubhafulaisya bhanadamu, nene na n'tumishi he wa Kristu.
11 Ndugu, ninataka ninyi mjue kwamba injili niliyoitangaza haitokani na wanadamu.
Ndongo, nilonda muenga mmanyai ya kuwa injili yanatangasili yitokana lepi ni bhanadamu.
12 Sikuipokea kutoka kwa mtu, wala sikufundishwa. Badala yake, ilikuwa ni kwa ufunuo wa Yesu Kristo kwangu.
Naipokili lepi kuhomela kwa bhanu, wala nafundisibhu lepi. Badala yaki, yayele kwa ufunuo wa Yesu Kristu kwa nene.
13 Mmekwisha sikia juu ya maisha yangu ya nyuma katika dini ya Kiyahudi, jinsi nilivyokuwa nikilitesa kwa ukali kanisa la Mungu zaidi ya kipimo na kuliteketeza.
Mwalili kup'eleka juu ya maisha gha nene gha kunyuma kup'etela dini ya kiyahudi, kanayele kanatesyai kiukali li kanisa la k'yara zaidi ya kiphemu ni kuliteketesya.
14 Nilikuwa nimeendelea katika Dini ya Kiyahudi zaidi ya ndugu zangu wengi Wayahudi. Nilikuwa na bidii sana katika tamaduni za baba zangu.
Kanayele niyendelili kup'etela dini ya kiyaudi kuzidi bhalongobhangu bhingi bhayaudi. Nayele ni bidii sana kup'etela mu tamaduni sa bha Dadi bhangu.
15 Lakini Mungu alipendezwa kunichagua mimi kutoka tumboni mwa mama. Aliniita mimi kupitia neema yake
Ila K'yara apendisibhu kunichagula nene kuhomela mulileme la mabhu. Anikutili nene kup'etela neema sa muene.
16 kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili kwamba nimtangaze yeye miongoni mwa watu wa mataifa. Wala sikutafuta ushauri wa mwili na damu
Kumdhihirisha mwana munu mugati mwa nene, ili yandabha ni mtangasyai muene pamiongoni mwa bhanu bha mataifa. Wala nalondili lepi ushauli wa mbhele ni muasi
17 na sikupanda kwenda Yerusalem kwa wale waliokuwa mitume kabla yangu. Badala yake nilienda Uarabuni na baadae kurudi Damesiki.
na nakwelili lepi kulota kuyerusalem kwa bhala bhabhayeli mitume kabula ya nene. Badala yake nalotili uarabuni ni kabhele kukelebhuka Damesiki.
18 Kisha baada ya miaka mitatu nilipanda kwenda Yerusalemu kumtembelea Kefa, nikakaa naye kwa siku kumi na tano.
Kabhele badala ya miaka midatu nakwelili kulota Yerusalem kun'gendela kefa, natamili naku kwa mogono kumi na tano.
19 Lakini sikuona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndungu yake na Bwana.
Lakini nabhuee mitume bhangi labuda Yakobo, ndongho munu ni Bwana.
20 Tazama, mbele za Mungu, sidanganyi kwa kile niandikacho kwenu.
Langai, palongolo K'yara, nikofyalepi kwa eke kani yandika kwa muenga.
21 Kisha nilikwenda mikoa ya Shamu na Kilikia.
Kabhele nalotili kumikoa ya Shamu ni kilikia.
22 Sikuwa najulikana kwa macho kwa makanisa ya Uyahudi yale yaliyokuwa katika Kristo,
Nama nyikanai lepi kwa mihu kwa makanisa gha uyaudi ghala ghaghayele kup'etela Kristu,
23 lakini walikuwa wakisikia tu, “Yeye aliyekuwa akitutesa sasa anatangaza imani aliyokuwa akiiharibu.”
Ila bhayele bhakipeleka to, “Muene ayele kututesya henu itangasya imani yaya haribuayi”.
24 Walikuwa wakimtukuza Mungu kwa ajili yangu.
Bhayele kumtukuza K'yara kwajia nene.