< Ezra 9 >

1 Kipindi mambo hayo yanatendeka, wakuu wakaja kwangu na kuniambia,”Watu wa Israel, Makuhani na walawi hawakuweza kujitenga wenyewe kutoka kwa watu wa nchi zingine na maovu yao: Wakanaani, Wahiti, Waperuzi, wayebusi, Waamoni, Wamoabu, Wamisri na Waamori.
Baada ya mambo haya kutendeka, viongozi walinijia na kusema, “Watu wa Israeli, wakiwemo makuhani na Walawi, hawakujitenga na majirani zao katika kufanya machukizo, kama yale ya Wakanaani, Wahiti, Waperizi, Wayebusi, Waamoni, Wamoabu, Wamisri na Waamori.
2 Kwa kuwa wamewachukua baadhi ya binti na watoto wa kiume, wamejichanganya watu watakatifu na watu wa nchi nyingine na wakuu na viongozi wamekuwa wa kwanza katika imani hii potofu.
Wamewaoa baadhi ya binti zao kuwa wake zao na wake za wana wao, nao wamechanganya taifa takatifu na watu waliowazunguka. Nao viongozi na maafisa wamekuwa mstari wa mbele katika njia hii potovu.”
3 Niliposikia haya, nikachana nguo zangu na kanzu na kunyoa nywele kichwani na ndevu na nikakaa chini kutafakari.
Niliposikia jambo hili nilirarua koti langu na joho langu, nikazingʼoa nywele za kichwa changu na ndevu zangu na kuketi nikishangaa.
4 Na wale wote waliotetemeka kwa neno la Mungu wa Israel kuhusu imani potofu walikusanyika kwangu wakati nimakaa chini nikiwa na aibu hadi kufikia kipindi cha sadaka za jioni.
Kisha kila mmoja aliyetetemeshwa na maneno ya Mungu wa Israeli alikusanyika kunizunguka kwa sababu ya upotovu huu wa hao watu waliorudi kutoka utumwani. Nami niliketi pale nikishangaa mpaka wakati wa dhabihu ya jioni.
5 Lakini katika sadaka ya jioni nikasimama kwenye nafasi yangu nikiwa mnyenyekevu na nguo ilichanika na kanzu, na nikapiga magoti na kunyoosha mikono yangu kwa Yahwe Mungu wangu. Nikasema
Ndipo wakati wa kutoa dhabihu ya jioni nikainuka kutoka kujidhili kwangu nikiwa na koti na joho langu lililoraruka, nikapiga magoti mikono yangu ikiwa imeinuliwa kwa Bwana Mungu wangu.
6 “Mungu wangu, nina aibu na sistahili kuinua uso wangu kwako, makosa yetu yamekuwa hadi kuvuka kichwani na maovu yetu yameongezeka kufika mbinguni.
Nami nikaomba: “Ee Mungu wangu, natahayari na kuona aibu kukuinulia uso wangu Mungu wangu, kwa sababu dhambi zetu zimejikusanya hata kupita juu ya vichwa vyetu na hatia yetu imefika mbinguni.
7 Kuanzia siku ya watangulizi wetu mpaka sasa tumekuwa katika maovu makuu. Makosa yetu, viongozi, makuhani, walikuwa katika mikono ya mfalme wa dunia hii, katika upanga, matekani na kunyanyaswa na tuna aibu ya uso hata leo.
Tokea siku za babu zetu mpaka sasa, hatia yetu imekuwa kubwa. Kwa sababu ya dhambi zetu, sisi na wafalme wetu na makuhani wetu tumekabiliwa na vita, utumwa, kutekwa na kudhiliwa katika mikono ya wafalme wa kigeni, kama ilivyo leo.
8 sasa kwa kipindi kifupi, neema kutoka kwa Yahwe Mungu wetu imekuja kutuacha mabaki wachache na kutupa kuhimmili sehemu takatifu. Hii ilikuwa ni kwa ajili ya Mungu wetu kututia nuru macho yetu na kutupa unafuuu sisi tulio watumwa.
“Lakini sasa, kwa muda mfupi, Bwana Mungu wetu amekuwa na neema kwa kutuachia mabaki na kutupa mahali imara katika mahali pake patakatifu, hivyo Mungu wetu atupa mwanga machoni petu na unafuu katika utumwa wetu.
9 Kwa kuwa sisi tu watumwa, lakini Mungu bado hajatusahau lakini ameongeza agano la uaminifu kwetu, ameyatenda haya mbele ya macho ya mfalme wa Uajemi ili kwamba haweze kutupatia nguvu mpya. Ili kwamba tuweze kujenga nyumba ya Mungu na tuweze kuondoa majuto. Alitenda hayo ili kwamba aweze kutupatia msingi wa usalama katika Yuda na Yerusalem.
Ingawa tu watumwa, Mungu wetu hajatuacha katika kufungwa kwetu. Ametuonyesha huruma mbele ya wafalme wa Uajemi: Ametujalia maisha mapya kwa kujenga upya nyumba ya Mungu wetu na kukarabati magofu yake, naye ametupa ukuta wa ulinzi katika Yuda na Yerusalemu.
10 Lakini sasa Mungu wetu, tuseme nini baaada ya haya? Tumesahau amri zako.
“Lakini sasa, Ee Mungu wetu, tunaweza kusema nini baada ya hili? Kwa maana tumedharau maagizo
11 amri ambazo uliwapa manabii watumishi wako, pale uliposema, “Nchi hii mnayoingia kuimiliki ni nchi chafu. Imechanganyikana na watu wasio na utaratibu. ameenea kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa uchafu wao.
uliyoyatoa kupitia watumishi wako manabii uliposema: ‘Nchi mnayoiingia kuimiliki ni nchi iliyochafuliwa na uovu wa watu wake. Kwa matendo yao ya machukizo wameijaza nchi kwa unajisi wao kutoka mwisho mmoja hadi mwingine.
12 Hivyo sasa, msiwape binti zenu kwa watoto wao, msichukue binti zao kwa ajili ya watoto wenu, msitafute amani kwao na fadhili, ili kwamba muweze kuwa imara na kula vizuri vya nchi, hivyo utasababisha watoto wenu kumiliki kwa wakati wote.”
Kwa hiyo, msiwaoze binti zenu kwa wana wao wala binti zao kwa wana wenu. Msitafute mkataba wa urafiki nao kwa wakati wowote. Ndipo mtakapofanikiwa na kula mema ya nchi na kuwaachia watoto wenu nchi hiyo kama urithi wao wa milele.’
13 Baada ya yote kutokea kwetu kwa sababu ya uovu wetu na makosa yetu makuu, tokea hapo, Mungu wetu, hukutazama makosa yetu na kutuadhibu tulivyostahili na ukatuacha kama mabaki.
“Yale yaliyotupata ni matokeo ya matendo yetu mabaya, pia hatia yetu kubwa. Hata hivyo, wewe Mungu wetu, umetuadhibu kidogo kuliko dhambi zetu zilivyostahili na umetupa mabaki kama haya.
14 Tunaweza kuvunja tena amri zako na kuingiliana katika ndoa, na hawa watu wasiofuata utaratibu? Je hautachukia na kututowesha sote hakuna wa kubaki, hakuna wa kutoroka?
Je, tutavunja maagizo yako tena na kuoana na watu ambao hufanya mambo ya machukizo? Je, hutakuwa na hasira ya kutosha juu yetu na kutuangamiza, bila kutuachia mabaki wala atakayenusurika?
15 Yahwe, Mungu wa Israel, wewe ni mwenye haki, kwa kuwa tumebaki wachache mabaki hadi siku ya leo. Tazama, tuko mbele yako na makosa yetu, kwa kuwa hakuna hata mmoja anayeweza kusimama mbele kwa sababu ya hili.
Ee Bwana, Mungu wa Israeli, wewe ni mwenye haki! Leo hii tumeachwa kama mabaki. Tupo hapa mbele zako na hatia yetu, ingawa katika hali hii hakuna hata mmoja wetu anayeweza kusimama mbele zako.”

< Ezra 9 >