< Ezra 6 >
1 Na mfalme dario akaamuru uchunguzi ufanyike katika nyumba ya kumbukumbu Babeli.
達理阿王遂下令,檢查在巴比倫貯藏寶物的檔案室。
2 Na katika mji wa Akmetha huko media chuo kilionekana: Kumbukumbu yake ilisema:
在厄克巴塔納,即在瑪待省的王堡內,發現了一宗案卷,上邊這樣的記載:「備忘錄:
3 “Katika mwaka wa kwanza mfalme Koresh, Koreshi alitoa amri kuhusu nyumba ya Mungu Yerusalem:'Na nyumba ijengwe iwe sehemu ya kutoa dhabihu, misingi yake iwekwe, urefu wake uwe sitini,
居魯士王元年,居魯士曾為耶路撒冷天主的殿宇,頒發上諭:殿宇應予重建,為在那裏舉行祭獻,奉獻火祭;殿應高六十肘,寬六十肘,
4 na upana wake uwe sitini, sehemu tatu za mawe makubwa na sehemu moja ya mbao mpya, na gharama hizo zitalipwa kutoka nyumba ya mfalme.
三層用方石,一層用木料修建;所有費用概出自室。
5 Sasa vilirudishwe tena vitu vya dhahabu na fedha vilivyokuwa kwenye nyumba ya Mungu ambavyo Nebukadineza alivichukua kuvipeleka Babeli kutoka kwenye Hekalu Yerusalem. Na avirudishe tena Yerusalem Hekaluni. Na utaviweka tena kwenye nyumba ya Mungu.
此外,凡拿步高王取耶路撒冷殿宇,而運到巴比倫的,天主殿宇的那些金銀器,冊都應歸還,送回耶路撒冷的殿宇內,各放在原處,安置在天主的殿宇內。
6 Sasa Tetanai, mkuu wa jimbo ngambo ya mto, Shethar - Bozenai na wenzao walio katika mji ngambo ya mto, wakajitenga,
河西州長塔特乃的同僚官員,應退出那地,
7 wakaacha kazi ya nyumba ya Mungu pekee. Viongozi na wazee wa kiyahudi watajenga nyumba ya Mungu mahali pake.
不可干涉天主殿宇的工程,任憑猶太人的總督和猶太人的長老,在原處重建天主的殿宇。
8 Ninatoa agizo kwamba lazima lifanyike kwa wazee wa kiyahudi wanaojenga nyumba ya Mungu: Mchango kutoka kwa mfalme ushuru ngambo ya mto, utatumika katika kuwalipa watu hawa ili kwamba kazi yao isiweze kusimama.
此外,我且頒下此旨,諭令你們為協助猶太人的長老,修建天主的殿應行的事:由河西收入王室的賦稅,給那些人撥出充分的經費,不得有誤!
9 Chochote kitakachohitajika, ngombe wachanga, kondoo au kondoo wa sadaka ya kutekezwa kwa ajili ya Mungu wa mbinguni, ngano, chumvi, divai na mafuta kadri ya maagizo ya makuhani wa Yerusalem - wapatie vitu hivi kila siku bila kikomo.
他們向上天大王,獻全燔祭所需要是牛犢、公綿羊和羔羊,以及麵、鹽、酒和油,應按耶路撒冷的司祭所指定的,每天供應,不得有誤!
10 fanya hivyo ili kwamba wataleta sadaka kwa Mungu wa mbinguni na wataomba kwa ajili yangu mfalme na watoto wangu.
好使他們向上天的大王,奉獻馨香祭,為君王和王孫的長壽祈禱。
11 Mimi nina agiza kwamba yeyote atakayevunja amri hii, Chuma kitolewe katika nyumba yake. Na awekwe juu yake. Na nyumba yake itabadilishwa kuwa takataka kwa sababu hii.
我今頒下此令:凡有敢刪改此令者,應把他屋內的樑木拆出,堅起來,把他懸在上邊;令他的房屋從此成為糞堆。
12 Mungu huyu aliyesababisha jina lake kuwepo atamwondoa mfalme au mtu atakayebadili agizo hili au kuondosha nyumba ya Mungu katika Yerusalem. Mimi Dario nimeagiza hili, lifanyike kwa makini.
凡有敢刪改此令,對耶路撒冷的天主殿宇,敢於破壞的王侯和人民,願那使己名住在那裏的天主將他毀滅! 我達理阿頒發此令,應悉依照遵行! 」
13 Na kwa sababu ya amri iliyotumwa na mfalme Dario, Tatenai kiongozi mji ngambo ya mto na Sheshthar -Bozenai na wenzao. wakafanya kila kitu kama Mfalme Dario alivyoagiza.
於是河西長塔特乃和他們的同僚,全照達理阿王所頒佈的,一一遵行。
14 Hivyo wazee wa kiyahudi wakajenga kama Hagai na Zakaria walivyoelekeza kwa kutabiri. Wakajenga kama amri ilivyotolewa na Mungu wa Israel na Koreshi, Dario na Artashasta mfalme wa Uajemi.
猶太人的長老遂繼續修建,因著先知哈蓋,和依多的兒子匝利亞的鼓勵,進行的很是順利;如此他們遵照以色列天主的旨意,並按照波斯王居魯士和達理阿的諭令,完成了修殿的工程。
15 Nyumba ikakamilika siku ya tatu ya mwezi wa adari, katika mwaka wa sita wa kutawala mfalme Dario.
聖殿完工的日期,是在達理阿王在位第六年,「阿達爾」月初三日。
16 watu wa Israel, makuhani, walawi na watu waliobaki wa uhamisho wakasheherekea kuweka wakfu nyumba ya Mungu kwa furaha.
以色列子民、司祭、肋未人和其餘由充軍歸來的人,興高彩烈,為天主的殿舉行了奉獻禮。
17 Wakatoa ngombe mia moja, kondoo mia moja na kondoo wengine mia nne kwa ajili ya kuweka wakfu nyumba ya Mungu. Mbuzi wa kiume kumi na wawili walitolewa kama sadaka ya dhambi kwa ajili ya waisrael wote kila kabila katika Israel.
天主聖殿的奉獻禮,奉獻了牛犢一百頭,公綿羊二百隻,羔羊四百隻;又照以色列支派的數目,a了十二隻公山羊,為贖全叵的罪。
18 Pia wakawapa wajibu makuhani na walawi kufanya mgawanyo wa kazi ya Mungu katika Yerusalem. Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Musa.
他們又派定了司祭,按照他們的編制,肋未人,按照他們的班次,在耶路撒冷值班奉侍天主,全照梅瑟書上所記載的。
19 Hivyo wale waliokuwa utumwani wakasherehekea pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza.
由充軍歸來的子民,於正月十四日,舉行了逾越節。
20 Makuhani na walawi wakajitakasa wenyewe na wakachinja pasaka ya sadaka kwa ajili ya waliokuwa mateka wakiwemo na wao wenyewe.
肋未人全都聖潔了自己,他們既已聖潔了,就為所有充軍歸來的人,並為他們的兄弟司祭和自己,宰殺了逾越節羔羊。
21 watu wa Israel ambao walikula nyama ya Pasaka ni wale waliorudi kutoka uhamishoni na walikuwa wamejitenga wenyewe kutoka kwa watu wasio safi wa nchi ile na kumchagua Yahwe, Mungu wa Israel.
凡由充軍歸來的以色列子民,並所有戒絕當地民族不潔的人,尋求上主以色列的天主,都吃了逾越節羔羊。
22 Walifurahi na kushangilia siku kuu ya mikate isiyochacha kwa siku saba, kwa sababu Yahwe amewarejeshea furaha na ameugeuza moyo wa mfalme wa Ashuru, na kuwatia nguvu kwa kazi ya nyumba, nyumba ya Mungu wa Israel.
七天之久,歡樂地舉行了無酵節,因為上主使亞述王的心傾向他們,協助了他們修建以色列天主的聖殿,都非常歡樂。