< Ezra 4 >
1 Ndipo maadui wa Yuda na Benjamini waliposikia kwamba watu waliokuwa uhamishoni walikuwa wanajenga Hekalu la Yahwe, Mungu wa Israel.
2 Hivyo wakamkaribia Zerubabeli na wakuu wa jamii yao. Wakawaambia: Mturuhusu tujenge pamoja nanyi, kama ninyi, tunamtafuta mungu wenu, na tumejitoa kwake tangu siku ambapo, Esar-hadoni, mfalme wa Ashuru alipotuleta mahali hapa.”
3 Lakini Zerubabeli, Yoshua na wakuu wa kale wa jamii wakasema, “sio wewe, lakini sisi ndio tunaowajibika kujenga nyumba ya Mungu wetu, Sisi ndio tutakaomjengea Yawe, Mungu wa Israel, kama vile mfalme koreshi mfalme wa Ashuru alivyoagiza.”
4 Hivyo watu wa nchi wakadhoofisha mikono ya wayahudi, wakawafanya wayahudi waogope kujenga nyumba.
5 Pia wakawahonga washauri ili kuwachanganya katika mipango yao. Walitenda haya kipindi chote cha Koreshi na kipindi cha utawala wa Dario mfalme wa Uajemi.
6 Tena katika kuanza kutawala kwake Ahasuero wakaandika mashitaka dhidi ya wenyeji wa Yuda na Yerusalem
7 Ilikuwa siku za Ahasuero ambazo Artashasta, Mithredathi, na Tabeeli na wenzake wakamwandikia Ahasuero. Barua iliandikwa Kiaramu na kutafsiliwa.
8 Rehumu jemedari na Shimshai mwandishi wakaandika hivi kwa Artashasta kuhusu Yerusalem.
9 Tena Rehumu, Shimshai na wenzao ambao ni waamuzi na maofisa wengine wa Serikali, kutoka Waarkewi, Wababeli na washushami katika Waelami,
10 nao wakaandika barua na waliungana na watu wakuu na mheshimiwa Asur - bani - pali aliwalazimisha kukaa Samalia pamoja na waliobaki katika mji ngambo ya mto.
11 Hii ni nakala waliotuma kwa Artashasta: “Watumishi wako, watu wa mji ngambo ya mto, waandika hivi:
12 Mfalme atambue kwamba Wayahudi waliotoka kwako wamefanya kinyume chetu hapa Yerusalem wamejenga mji wa uasi. Wamekamilisha ukuta na marekebisho ya misingi.
13 Sasa mfalme atambue kwamba endapo mji utajengwa na kuta zake kukamilika, hawatatoa ushuru na kodi, lakini watawadhuru wafalme.
14 Hakika kwa kuwa tumekula chumvi ya Ikulu, haitopendeza sisi kuona heshima ya mfalme inavunjwa, kwa sababu hiyo tunamtaarifu mfalme
15 kufanya uchunguzi wa kumbukumbu ya baba yake, na kujiridhisha kuwa mji huu ulikuwa wa uharibifu ambao utawadhuru wafalme na miji. Ulisababisha matatizo mengi kwa wafalme na miji. Ilikuwa ni kitovu cha uhalibifu tokea siku nyingi. Ni kwa sababu hiyo mji uliteketezwa.
16 Tunamtaarifu mfalme kuwa endapo mji na ukuta ukijengwa, Hakuna kitakachobakia kwa ajili yako katika mji ngambo ya mto.”
17 Ndipo mfalme akarudisha majibu kwa Rehumu na Shimshai na wenzao katika Samalia na waliobaki katika mji ngambo ya mto. “Amani iwe pamoja nanyi.
18 Barua mliyonitumia imetafsiliwa na kusomwa kwangu.
19 Hivyo niliagiza uchunguzi ufanywe na ikabainika kwamba zamani uliasi na kuwafitinisha wafalme.
20 Wafalme wakuu walitawala Yerusalem yote na kuongoza kila sehemu ya mji ngambo ya mto. Ada na kodi walilipwa.
21 Sasa, wekeni agizo kwa watu hawa wasiendelee na kujenga mji mpaka nitakapotoa amri.
22 Muwe waangalifu msipuuze hili. Kwa nini kuruhusu tishio hili kuongezeka na kusababisha hasara kwa matakwa ya ufalme?
23 Baada ya amri ya mfalme Artashasta kusomwa mbele ya Rehumu, Shimshai na wenzao, wakaondoka haraka kwenda Yerusalem, na wakawalazimisha Wayahudi kuacha kujenga.
24 Hivyo kazi ya nyumba ya Mungu Yerusalem ikasitishwa mpaka kutawala mara ya pili kwa mfalme Dario wa Uajemi.