< Ezra 10 >
1 Wakati Ezra akiomba na kutubu, akalia na kujirusha chini mbele ya nyumba ya Mungu, kusanyiko kubwa la wanaume Israel, wanawake na watoto wakakusanyika kwake, kwa kuwa watu walikuwa wakilia sana.
2 Shekania mtoto wa Yehieli, mwana wa Elamu akamwambia Ezra, “Tumekuwa sio waaminifu kwa Mungu na tumeoa wanawake wa kigeni kutoka nchi nyingine. Lakini pamoja na hilo, bado kuna tumaini kwa Israel.
3 sasa natuweke agano pamoja na Mungu wetu kuwaondoa wanawake wote na watoto wao kulingana na maelekezo ya Bwana, na maelekezo ya wale wanaotetemeka kutokana na amri za Mungu wetu. na hii ifanyike kutokana na sheria.
4 Simama, jambo hili linakuhusu wewe, na sisis tuko pamoja na wewe, Uwe imara na kufanya hili.
5 Hivyo Ezra akasimama na kufanya makuhani na walawi na waisrael wote wakaahidi kufanya kwa njia hiyo. Hivyo wote wakatoa kiapo.
6 Ndipo Ezra akainuka kutoka mbele ya nyumba ya Mungu na kwenda kwenye chumba ya Yehohanani mtoto wa Eliashibu, Yeye hakula mkate au kunywa maji. Tangu alipokuwa akiomboleza kuhusiana na wale wenye imani haba waliokuwa uhamishoni.
7 Hivyo wakatuma neno katika Yuda na Yerusalem kwa watu wote waliorudi kutoka utumwani kukusanyika Yerusalem.
8 Yeyote ambaye hakuja katika siku tatu kutokana na maelekezo kutoka kwa wakuu na viongozi atachukuliwa mali zote na atatengwa na kusanyiko kuu la watu ambao walikuja kutoka uhamisho.
9 Hivyo watu wote wa Yuda na Benjamini wakakusanyika Yerusalem kwa siku tatu. Ilikuwa ni mwezi wa tisa na siku ya ishirini ya mwezi. watu wote wakasimama mbele ya nyumba ya Mungu na wakatetemeka kwa sababu ya neno na mvua.
10 Ezra kuhani akasimama na kusema, “Ninyi wenyewe mmefanya uasi, ninyi mmeishi na wanawake wa kigeni na kuongeza makosa ya Israel.
11 Lakini sasa mpeni sifa Yahwe, Mungu wa watangulizi wenu, na mfanye mapenzi yake, mjitenge na watu wa nchi na wanawake wa kigeni.
12 Kusanyiko lote likajibu kwa sauti. “Tutatenda kama ulivyosema,
13 haijalishi, kuna watu wengi na ni kipindi cha mvua. Hatuna nguvu ya kusimama nje na hii si siku moja au mbili za kufanya kazi, kwa kuwa tumekosea katika jambo hili.
14 Hivyo wakuu wetu wawakilishe kusanyiko lote, iwe kwamba wote walioruhusu wanawake wa kigeni kuishi katika miji yetu waje katika muda uliopangwa na viongozi wa mji na waamuzi wa mji hadi hapo hasira ya Mungu itakapoondoka kutoka kwetu.
15 Yonathan mtoto Asaheli na Yazeya mwana wa Tikwa wakapinga hili, Meshulamu na Shabethai mlawi wakawaunga mkono wao.
16 Hivyo watu waliotoka uhamishoni wakafanya hivi, Ezra kuhani akachagua wanaume, viongozi watamgulizi wa ukoo na nyumba, wao wote kwa majina na wakaliangalia suala hili siku ya kwanza ya mwezi wa kumi.
17 Siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza wakawa wamemaliza kuchunguza wale wanaume walioishi na wanawake wa kigeni.
18 Miongoni mwa wana wa kikuhani kuna wale walioishi na wanawake wa kigeni. Miongoni mwa wana wa Yoshua mtoto wa Yosadaki na kaka zake ambao walikuwa Maasela, Eliazeri, na Yaribu na Gedalia.
19 Hivyo wakaamua kuwaondoa wake zao. kwa kuwa walikuwa na makosa, wakatoa sadaka ya kondoo kwenye mifugo kwa ajili ya makosa yao.
20 Miongoni mwa wana wa Imeri, Hanani, na Zebadia.
21 Miongoni mwa wana wa Harimu, Maaseya, na Eliya na Shemaya, na Yehieli na Uzia.
22 Miongoni mwa wana wa Pashuri, Elasa
23 Miongoni mwa walawi: Yozabadi na Shimei na Kelaya (ndiye Kelita) na Pethaia, na Yuda na Eliezeri. Miongoni mwa waimbaji Eliashibu na. Miongoni mwa walinzi Shalumu, Telemu na Uri.
24 Miongoni mwa Israel waliobaki -
25 Miongoni mwa wana wa Paroshi, Ramia na Izia na Malkiya na Miyamini na Eliazari na Malkiya na Benaya
26 Miongoni mwa wana wa Elamu Mataniana Zekaria, na yeehieli, na Abdi na Yeremothi na Eliya.
27 Miongoni mwa wana wa Zatu: Elionai, na Eliashibu, na Matania na Yeremothi na Zabadi na Aziza.
28 Miongoni mwa wana wa Bebai Yehohanani, na Hanania na Zakai na Athlai.
29 Miongoni mwa wana wa bani: Meshulami na Maluki, na Adaya na Yashubu na Sheali na Yeremothi.
30 Miongoni mwa wana wa Pahath-Moabu, Adna, na kelali, na Benaya na Maaseya, na Matania, na Besaleli na Binti na Manase.
31 Na miongoni mwa wana wa Harimu: Eliezeri na Ishiya, na Malkiya na Shemaya na Shimeoni, na
32 Benyamini na Maluki na Shemaria
33 Miongoni mwa wana Hashumu: Matenai, na Matatana Zabadi, na Elifereti na Yeremai, na Manase, na Shimei.
34 Miongoni mwa wana wa Bani: Maadai, na Amramu na Aueli, na
35 Benaya, na Bedeya na Keluhi, na
36 wania, na Meremothi, Eliashibu,
37 Matania, na Matenai. na
38 Yaasi. Miongoni mwa wana wa Binui: Shimei,
39 Sheremia, na Nathani, na Adaya, na
40 Maknadebai, na Shashai, na Sharai
41 Azareri, na Sheremia, na Shemaria, na
42 Shalumu, na Amaria, na Yusufu.
43 Miongoni wa wana wa Nebo: Yeieli, na Mathiana zabadi, na Zebina, na Ido, na Yoeli na Benaya.
44 Hawa wote walikuwa wameoa wanawake wa kigeni na walikuwa wamezaa watoto baadhi yao.