< Ezekieli 8 >

1 Hivyo ikawa kuhusu katika mwaka wa sita na mwezi wa sita, katika siku ya tano ya mwezi, nilipokuwa nimeketi kwenye nyumba yangu na wazee wa Yuda waliketi mbele yangu, kwamba mkono wa Bwana Yahwe ukanijaza juu yangu huko.
第六年六月初五日,我坐在家中;犹大的众长老坐在我面前。在那里主耶和华的灵降在我身上。
2 Hivyo nikaona, na tazama, kulikuwa na mfano kama mwonekano wa mwanadamu. Kutoka kwenye mwonekano wake wa nyonga kwenda chini kulikuwa na moto. Na kutoka kwenye nyonga kwenda juu kulikuwa na mwonekano wa kitu kinachong'aa, kama mng'ao wa chuma.
我观看,见有形象仿佛火的形状,从他腰以下的形状有火,从他腰以上有光辉的形状,仿佛光耀的精金。
3 Kisha akanyoosha kutoka kwenye mkono na kunichukua kwa nywele za kichwa changu; Roho akaniacha juu kati ya dunia na mbingu, na katika maono kutoka kwa Mungu, akaniletea hata Yerusalemu, kwenye mlango wa kuingia ndani ya lango la kaskazini, ambako sanamu ile iletayo wivu mkubwa ilipokuwa imesiamama.
他伸出仿佛一只手的样式,抓住我的一绺头发,灵就将我举到天地中间,在 神的异象中,带我到耶路撒冷朝北的内院门口,在那里有触动主怒偶像的坐位,就是惹动忌邪的。
4 Kisha tazama, utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa huko, kulingana na ono nililokuwa nimeliona kwenye uwanda.
谁知,在那里有以色列 神的荣耀,形状与我在平原所见的一样。
5 Kisha akanambia, “Mwanadamu, inua juu macho yako kwenda upande wa kaskazini.” Hivyo nikainua macho yangu kuelekea kaskazini, na kwenye lango la kaskazini kulekea kwenye madhabahu, huko kwenye lango la kuingilia, kulikuwa na sanamu ya wivu.
神对我说:“人子啊,你举目向北观看。”我就举目向北观看,见祭坛门的北边,在门口有这惹忌邪的偶像;
6 Hivyo akanambia, “Mwanadamu, unaona wanayoyafanya? Haya ni machukizo makubwa ambayo nyumba ya Israeli wanayoyafanya hapa kunifanya niende mbali kutoka patakatifu pangu. Lakini utageuka na kuona machukizo makubwa zaidi.”
又对我说:“人子啊,以色列家所行的,就是在此行这大可憎的事,使我远离我的圣所,你看见了吗?你还要看见另有大可憎的事。”
7 Kisha akanileta hata kwenye mlango wa uzio, na nikatazama, kulikuwa na shimo kwenye ukuta.”
他领我到院门口。我观看,见墙上有个窟窿。
8 Akanambia, “Mwanadamu, chimba kwenye huu ukuta.” Basi nikachimba kwenye huo ukuta, na kulikuwa na mlango.
他对我说:“人子啊,你要挖墙。”我一挖墙,见有一门。
9 Kisha akanambia, “Nenda na ukaone machukizo ya uovu ambayo wanayoyafanya hapa.”
他说:“你进去,看他们在这里所行可憎的恶事。”
10 Basi nilipokuwa nikienda ndani na nikaona, na tazama! Kulikuwa na kila umbo la vitu vikitembea polepole na mnyama achukizaye sana! Kila sanamu wa nyumba ya Israeli ilikuwa imechongwa kwenye ukuta pande zote.
我进去一看,谁知,在四面墙上画着各样爬物和可憎的走兽,并以色列家一切的偶像。
11 Wazee sabini wa wa nyumba ya Israeli walikuwa huko, na Yaazania mwana wa Shafani alikuwa amesimama katikati yao. Walikuwa wamesimama mbele ya picha, na kila mtu alikuwa na chetezo kwenye mkono wake ili kwamba harufu ya ubani ingeweza kupanda juu.
在这些像前有以色列家的七十个长老站立,沙番的儿子雅撒尼亚也站在其中。各人手拿香炉,烟云的香气上腾。
12 Akanambia, “mwanadamu, unaona kile ambacho wazee wa nyumba ya Israeli wanachokifanya kwenye giza? Kila mmoja hufanya hivi kwenye chumba cha sanamu yake, kwa kuwa husema, 'Yahwe hatuone! Yahwe ameitelekeza hii nchi.”'
他对我说:“人子啊,以色列家的长老暗中在各人画像屋里所行的,你看见了吗?他们常说:‘耶和华看不见我们;耶和华已经离弃这地。’”
13 Kisha akanambia, “Geuka tena na tazama machukizo makubwa ambayo wanayoyafanya.”
他又说:“你还要看见他们另外行大可憎的事。”
14 Tena akanileta kwenye lango la kuingia la nyumba ya Yahwe lililokuwa upande waa kaskazini, na tazama! Wanawake walikuwa wameketi huko wakimlilia Tamuzi.
他领我到耶和华殿外院朝北的门口。谁知,在那里有妇女坐着,为搭模斯哭泣。
15 Hivyo akanambia, “Umeiona hii, mwanadamu? Geuka tena na uone machukizo makubwana zaidi kuliko hayo.”
他对我说:“人子啊,你看见了吗?你还要看见比这更可憎的事。”
16 Akanileta hata kwenye uzio wa ndani wa nyumba ya Yahwe, na tazama! huko kwenye lango la kuingia kwenye madhabahu, kulikuwa na takribani watu ishirini na tano waliokuwa wamelipa mgongo hekalu la Yahwe na nyuso zao kuelekea mashariki, na walikuwa wakiabudu jua.
他又领我到耶和华殿的内院。谁知,在耶和华的殿门口、廊子和祭坛中间,约有二十五个人背向耶和华的殿,面向东方拜日头。
17 Akanambia, “Unaona hii, mwanadamu? Je ni kitu kidigo kwa ajili ya nyumba ya Yuda kufanya haya machukizo wanayoyafanya? Kwa kuwa wameijaza nchi kwa uovu na wamerudi tena ili kuniletea hasira, kuweka tawi kwenye pua zao.
他对我说:“人子啊,你看见了吗?犹大家在此行这可憎的事还算为小吗?他们在这地遍行强暴,再三惹我发怒,他们手拿枝条举向鼻前。
18 Hivyo nitatenda miongoni mwao pia; jicho langu halitakuwa na huruma, sitaacha kuwaharibu. hata watalia kwenye masikio yangu kwa sauti kubwa, sitawasikia.”
因此,我也要以忿怒行事,我眼必不顾惜,也不可怜他们;他们虽向我耳中大声呼求,我还是不听。”

< Ezekieli 8 >