< Ezekieli 5 >

1 “Kisha wewe mwana wa adamu, chukua upanga mkali kama wembe wa kinyozi kwa ajili yako mwenyewe, na pitisha hayo makali juu ya kichwa chako na ndevu zako, kisha chukua mizani za kupimia uzito na uzigawanye nywele zako.
人の子よ、鋭いつるぎを取り、それを理髪師のかみそりとして、あなたの頭と、ひげとをそり、はかりで量って、その毛を分けなさい。
2 Choma theluthi ya tatu ya hiyo kwa moto katikati ya mji wakati siku za kuzingirwa zitakapokamilika, na chukua theluthi ya nywele na uipige kwa panga na kuuzunguka mji. Kisha tawanya theluthi yake kwenye upepo, na nitasogeza panga karibu ili kufukuza watu.
その三分の一は包囲の期間の終る時、町の中で火で焼き、また三分の一を取り、つるぎで町のまわりでこれを打ち、さらに三分の一を風に散らしなさい。わたしはつるぎを抜いて、彼らのあとを追う。
3 Lakini chukua kiasi kidogo cha nywele na zifunge kwenye pindo za nguo yako.
あなたはその毛を少し取って、衣のすそに包み、
4 Kisha chukua tena zile nyewele na zitupe katikati ya moto; na zichome kwenye moto; kutoka hapo utatoka nje kwenda nyumba zote za Israeli.”
またそのうちから少しを取って火の中に投げ入れ、火でこれを焼きなさい。火はその中から出て、イスラエルの全家に及ぶ。
5 Bwana Yahwe asema hivi, “Hii ndio Yerusalemu katikati ya mataifa, nilipomuweka, na ambapo nilipomzunguka kwa nchi zingine.
主なる神はこう言われる、わたしはこのエルサレムを万国の中に置き、国々をそのまわりに置いた。
6 Lakini anaudhaifu wa kukataa amri zangu zaidi kuliko mataifa yalivyo, na sheria yangu zaidi kuliko mataifa ambayo yanayomzunguka. Watu wamezikataa humuku zangu na kuacha kutembea katika sheria zangu.”
エルサレムは他の国々よりも悪しく、わたしのおきてにそむき、そのまわりの国々よりもわたしの定めにそむいた。すなわち彼らはわたしのおきてを捨て、わたしの定めに歩まなかった。
7 Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi, “Kwa sababu mmekuwa kikwazo kuliko mataifa ambayo yanayowazunguka na kuacha kutembea kwenye amri zangu wala kutenda kulingana na amri zangu, wala hata kutenda kulingana na amri za mataifa yanayowazunguka,”
それゆえ主はこう言われる、あなたがたはそのまわりにいる異邦人よりも狂暴であって、わたしの定めに歩まず、わたしのおきてを行わず、むしろ、あなたがたの回りにいる異邦人のおきてを守っていた。
8 kwa hiyo Bwana asema hivi, “Tazama! Mimi mwenyewe nitatenda juu yenu. Nitato hukumu kati yenu ili mataifa waone.
それゆえ主なる神はこう言われる、見よ、わたしはあなたを攻め、異邦人の目の前で、あなたの中にさばきを行う。
9 Nitawafanyia yale ambayo sijawahi kuyafanya na kile ambacho sintokifanya tena, kwa sababu ya matendo yenu ya kuchukiza.
あなたのもろもろの憎むべき事のために、わたしがまだした事のないような事、またこの後ふたたびしないような事をあなたに対してする。
10 Kwa hiyo baba watawala watoto kati yenu, na watoto watawala baba zao, kwa kuwa nitafanya hukumu juu yenu na kuwatawanya kila mahali wote ninyi mliobaki.
それゆえ、あなたのうちで父はその子を食い、子はその父を食う。わたしはあなたに対してさばきを行い、あなたのうちの残りの者をことごとく四方の風に散らす。
11 Kwa hiyo, kama niishivyo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-bila shaka hii ilikuwa kwa sababu umapanajisi patakatifu pangu kwa mambo ya machukizo yako yote na kwa matendo yako yote niyachukiayo, kwamba mimi mwenyewe nitakupunguza katika hesabu; jicho langu halitakuhurumia, na sintoacha kukuharibu.
それゆえ、主なる神は言われる、わたしは生きている。あなたはその忌むべき物と、その憎むべき事とをもって、わたしの聖所を汚したので、わたしは必ずあなたの数を減らす。わたしの目はあなたを惜しみ見ず、またわたしはあなたをあわれまない。
12 Theluthi yenu mtakufa kwa tauni, na wataliwa na njaa katikati yenu. Theluthi wataanguka kwa upanga likiwazunguka. Kisha nitawatawanya theluthi katika mahali pote, na nitafuatisha upanga kuwafukuza pia.
あなたの三分の一はあなたの中で疫病で死に、ききんで滅び、三分の一はあなたのまわりでつるぎに倒れ、三分の一は四方の風に散らされる。わたしはつるぎを抜いてそのあとを追う。
13 Hivi ndivyo ghadhabu yangu itavyokamilika, na nitasababisha ghadhabu yangu juu yao hata kulala. Nitajiridhisha, na watajua kwamba, mimi Yahwe, nimenena kwa ghadhabu yangu wakati nitakapo kamilisha ghadhabu yangu dhidi yao.
こうしてわたしは怒りを漏らし尽し、憤りを彼らの上に漏らして、満足する。こうして、わたしの憤りを彼らの上に漏らし尽した時、彼らは主であるわたしが熱心に語ったことを知るであろう。
14 Nitakufanya mkiwa kwa mataifa yanayokuzunguka kwenye uso wa kila mtu apitaye karibu.
わたしはまわりにある国々の中と、すべてそばを通る者の目の前であなたを滅亡とあざけりに渡す。
15 Hivyo Yerusalemu itakuwa jambo kwa watu wengine kushutumu na kufanya mzaha, na chukizo kwa mataifa ambayo yanayowazunguka. Nitafanya hukumu dhidi yenu kwa ghadhabu na hasira, na kwa kukemea kwa hasira-Mimi, Yahwe nimesema hivi!
わたしが怒りと、憤りと、重い懲罰とをもって、あなたに対してさばきを行う時、あなたはそのまわりにある国々のあざけりとなり、そしりとなり、戒めとなり、驚きとなる。これは主であるわたしが語るのである。
16 Nitatuma mishale mikali ya njaa juu yenu ambayo itakuwa na maana ya kwamba nitawaharibu. Kwa kuwa nitaongeza njaa juu yenu na kuvunja tegemeo lenu la mkate.
すなわち、わたしがあなたを滅ぼすききんの矢、滅亡の矢をあなたに放つ時、わたしはあなたを滅ぼすために放つのだ。わたしはあなたの上にききんを増し加え、あなたがつえとするパンを打ち砕く。
17 Nitaleta njaa na majanga dhidi yenu hivyo mtakuwa wagumba. Tauni na damu zitapita kati yako, na nitaleta upanga dhidi yenu-Mimi Yahwe, nimesema hivi.”
わたしはあなたにききんと野獣を送って、あなたの子を奪い取り、また疫病と流血にあなたの中を通らせ、またつるぎをあなたに送る。主であるわたしがこれを言う」。

< Ezekieli 5 >