< Ezekieli 48 >
1 Haya ndiyo majina ya makabila. Kabila la Dani litapokea sehemu moja ya nchi; mipaka yake itakuwa karibu na upande wa mashariki mpaka wa Israeli karibu na njia ya Hethloni na Lebo Hamathi. Mpaka wake utaenda hata karibu na Hazari Enani na karibu na mpaka wa Damaskasi hata upande wa kaskazini na kisha karibu na Hamathi. Mpaka wa Dani utaenda kutoka mashariki moja kwa moja hata Bahari Kubwa.
“Haya ndiyo majina ya makabila na sehemu zao: Kwenye mpaka wa kaskazini, Dani atakuwa na sehemu moja, mpaka huo utafuata barabara ya Hethloni hadi Lebo-Hamathi, Hasar-Enani hata mpaka wa kaskazini wa Dameski karibu na Hamathi utakuwa sehemu ya huo mpaka wake kuanzia upande wa mashariki hadi upande wa magharibi.
2 Kupakana na mpaka wa Dani, kutoka upande wa mashariki hata upande wa magharibi, Asheri itakuwa na fungu moja.
“Asheri atakuwa na sehemu moja, itapakana na nchi ya Dani kuanzia mashariki hadi upande wa magharibi.
3 Kupakana na mpaka wa Asheri kutoka upande wa mashariki hata magharibi, Naftali atakuwa na fungu moja.
“Naftali atakuwa na sehemu moja, itapakana na nchi ya Asheri kuanzia mashariki hadi magharibi.
4 Kupakana na mpaka wa Naftali kutoka upande wa mashariki hata magharibi, Manase atakuwa na fungu moja.
“Manase atakuwa na sehemu moja, itapakana na nchi ya Naftali kuanzia mashariki hadi magharibi.
5 Kupakana na mpaka wa Manase kutoka upande wa mashariki hata magharibi, Efraimu atakuwa na fungu moja.
“Efraimu atakuwa na sehemu moja, itapakana na nchi ya Manase kuanzia mashariki hadi magharibi.
6 Kupakana na mapaka wa Efraimu kutoka mashariki hata magharibi, Rubeni atakuwa na fungu moja.
“Reubeni atakuwa na sehemu moja, itapakana na nchi ya Efraimu kuanzia mashariki hadi magharibi.
7 Kupakana na mpaka wa Rubeni kutoka mashariki hata magharibi, Yuda atakuwa na fungu moja.
“Yuda atakuwa na sehemu moja, itapakana na nchi ya Reubeni kuanzia mashariki hadi magharibi.
8 Sadaka ya nchi ambayo mtaifanya itakuwa karibu na mpaka wa Yuda na hapohapo kutoka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; itakuwa ridhaa elfu ishirini na tano upana. Urefu unakaribiana na fungu la kabila moja kutoka upande wa mashariki hata upande wa magharibi, na hekalu litakuwa katikati yake.
“Kupakana na nchi ya Yuda kuanzia mashariki mpaka magharibi itakuwa ndiyo sehemu utakayoitoa ili kuwa toleo maalum. Itakuwa na upana wa dhiraa 25,000 na urefu wake kuanzia mashariki mpaka magharibi utakuwa ule ule wa sehemu moja ya kabila, mahali patakatifu patakuwa katikati ya eneo hilo.
9 Huu mji mtakao utoa sadaka kwa ajili ya Yahwe utakuwa na ridhaa elfu ishirini na tano urefu wake na ridhaa elfu kumi upana.
“Hiyo sehemu maalum mtakayotoa kwa Bwana itakuwa na urefu wa dhiraa 25,000 na upana wa dhiraa 10,000
10 Haya yatakuwa matoleo ya hili fungu takatifu la nchi: makuhani watakuwa na nchi watakayopewa kipimo chake ridhaa elfu ishirini na tano urefu kwa upande kaskazini; ridhaa elfu kumi upana upande wa magharibi; urefu wa ridhaa elfu kumi upande wa magharibi; na urefu rithaa elfu ishirini na tano upande wa kusini, pamoja na mahali patakatifu pa Yahwe katikati yake.
Hii itakuwa ni sehemu takatifu kwa ajili ya makuhani. Itakuwa na urefu wa dhiraa 25,000 upande wa kaskazini, upana wa dhiraa 10,000 upande wa magharibi, dhiraa 10,000 upande wa mashariki na urefu wa dhiraa 25,000 upande wa kusini. Katikati yake patakuwa mahali patakatifu pa Bwana.
11 Hii itakuwa wakfu na makuhani wa safu ya Zadoki, aliyenitumikia kwa uaminifu na ambaye hakwenda nje ya mstari wakati watu wa Israeli walipoeenda nje ya mstari, kama Walawi walivyofanya.
Hii itakuwa kwa ajili ya makuhani waliowekwa wakfu, Wasadoki, waliokuwa waaminifu katika kunitumikia nao hawakupotoka kama Walawi walivyofanya wakati Waisraeli walipopotoka.
12 Sadaka yao itakuwa fungu la hiyo nchi takatifu sana, karibu na mpaka wa Walawi.
Itakuwa toleo maalum kwao kutoka sehemu takatifu ya nchi, yaani, sehemu takatifu sana, inayopakana na nchi ya Walawi.
13 Nchi ya Walawi karibu na mpaka wa nchi ya makuhani itakuwa ridhaa elfu ishirini na tano urefu na ridhaa elfu kumi upana. Urefu wote wa eneo la nchi utakuwa ridhaa elfu ishirini na tano urefu na ridhaa elfu ishirini upana.
“Kando ya nchi ya makuhani, Walawi watakuwa na mgawo wa urefu wa dhiraa 25,000 na upana wa dhiraa 10,000. Urefu wake utakuwa jumla dhiraa 25,000 na upana wa dhiraa 10,000.
14 Hawataiuza au kuibadilisha; hakuna malimbuko ya hiyo nchi ya Israeli itakayogawanywa kutoka haya maeneo, kwa kuwa yote ni matakatifu kwa ajili ya Yahwe.
Hawataruhusiwa kuuza wala kuibadilisha hata mojawapo. Hii ndiyo sehemu nzuri ya nchi kuliko nyingine zote, hivyo haitakuwa mikononi mwa watu wengine, kwa sababu ni takatifu kwa Bwana.
15 Nchi iliyobaki, ridhaa elfu kumi na tano upana na ridhaa elfu ishirini na tano urefu, itakuwa kwa wote wanayoitumia hiyo nchi, nyumba, na sehemu ya malisho; huo mji utakuwa katikati yake.
“Eneo linalobaki lenye upana wa dhiraa 5,000 na urefu wa dhiraa 25,000, litakuwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya mji, kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na malisho. Mji utakuwa katikati yake
16 Hivi ndivyo vitakuwa vipimo vya mji: upande wa kaskazini utakuwa ridhaa 4, 500 urefu; upande wa kusini utakuwa ridhaa 4, 500 urefu; upande wa magharibi utakuwa ridhaa 4, 500 urefu; na magharibi itakuwa ridhaa 4, 500 urefu.
nao utakuwa na vipimo hivi: upande wa kaskazini dhiraa 4,500, upande wa kusini dhiraa 4,500, upande wa mashariki dhiraa 4,500 na upande wa magharibi dhiraa 4,500.
17 Kutakuwa na malisho ya mji kuelekea kaskazini, ridhaa 250 kwenda chini; hata kusini, ridhaa 250 kwenda chini; kuelekea mashariki, ridhaa 250 kwenda chini, na kuelekea magharibi ridhaa 250 kwenda chini.
Sehemu ya malisho kwa ajili ya mji itakuwa na eneo la dhiraa 250 upande wa kaskazini, dhiraa 250 upande wa kusini, dhiraa 250 upande wa mashariki na dhiraa 250 upande wa magharibi.
18 Eneo lililobaki la matoleo matakatifu litanyooshwa ridhaa elfu kumi hata mashariki na ridhaa elfu kumi kuelekea magharibi. Litanyooshwa karibu na mpaka wa matoleo matakatifu, na mazao yake yatakuwa chakula kwa ajili ya wale wanaofanya kazi katika nchi.
Eneo linalobaki, linalopakana na sehemu takatifu likiwa na urefu sawa nalo, litakuwa dhiraa 10,000 upande wa mashariki na dhiraa 10,000 upande wa magharibi. Mazao yake yatawapa watumishi wa mji chakula.
19 Wale wafanyao kazi katika mji, watu wote wa kabila za Israeli, watailima hiyo nchi.
Watumishi wa mji wanaolima shamba hili watatoka katika makabila yote ya Israeli.
20 Matoleo yote ya nchi yatapimwa ridhaa elfu ishirini na moja kwa ridhaa elfu ishirini na tano. Kwa njia hii mtatengeneza matoleo matakatifu ya nchi, pamoja na nchi kwa ajili mji.
Eneo lote la hiyo sehemu litakuwa mraba, yaani, dhiraa 25,000 kila upande. Kama toleo maalum mtatenga sehemu takatifu, pamoja na milki ya mji.
21 Mabaki ya nchi mojawapo upande wa matoleo matakatifu na eneo la mji litakuwa kwa ajili ya mwana wa mfalme. Eneo la nchi ya mwana wa mfalme kuelekea mashariki litanyooshwa kwa ridhaa elfu ishirini na tano kutoka kwenye mpaka wa matoleo matakatifu hata mpaka wa mashariki-na eneo lake kuelekea mpaka wa magharibi. Katikati kutakuwa matolea matakatifu, na mahali patakatifu pa hekalu patakuwa katikati yake.
“Eneo linalobaki pande zote za eneo linalofanya sehemu takatifu na milki ya mji litakuwa mali ya mkuu atawalaye. Eneo hili litaenea upande wa mashariki kuanzia kwenye dhiraa 25,000 za sehemu takatifu hadi mpaka wa mashariki na kuelekea upande wa magharibi kuanzia kwenye dhiraa 25,000 hadi mpaka wa magharibi. Maeneo yote haya mawili yanayoenda sambamba na urefu wa sehemu za makabila yatakuwa ya mkuu anayetawala, na sehemu ile takatifu pamoja na mahali patakatifu pa Hekalu itakuwa katikati yake.
22 Nchi imenyooka kutoka mali ya Walawi na eneo la mji katikati yake litakuwa kwa ajili ya mwana wa mfalme; itakuwa kati ya mpaka wa Yuda na mpaka wa Benjamini-hiyo nchi itakuwa kwa ajili ya mwana wa mfame.
Kwa hiyo milki ya Walawi na milki ya mji vitakuwa katikati ya eneo lile ambalo ni mali ya mkuu anayetawala. Eneo la mkuu anayetawala litakuwa kati ya mpaka wa Yuda na mpaka wa Benyamini.
23 Kwa kabila zitakazobaki, mafungu yao yataunganishwa kutoka upande wa mashariki. Benjamini atapokea fungu moja.
“Kuhusu makabila yaliyobaki: Benyamini atakuwa na sehemu moja, itakayoanzia upande wa mashariki hadi upande wa magharibi.
24 Kupakana na mpaka wa Benjamini kutoka upande wa mashariki hata magharibi, Simioni atakuwa na fungu moja.
“Simeoni atakuwa na sehemu moja, itakayopakana na nchi ya Benyamini kuanzia mashariki hadi magharibi.
25 Kupakana na mpaka wa Isakari kutakuwa na fungu moja.
“Isakari atakuwa na sehemu moja, itakayopakana na nchi ya Simeoni kuanzia mashariki hadi magharibi.
26 Kupakana na mpaka wa Isakari kutoka mashariki hata magharibi, Zebuloni atakuwa na fungu moja.
“Zabuloni atakuwa na sehemu moja, itakayopakana na nchi ya Isakari kuanzia mashariki hadi magharibi.
27 Hata kusini mwa mpaka wa Zebuloni, kutoka upande wa mashariki hata upande wa magahribi, kutakuwa na nchi ya Gadi-fungu moja.
“Gadi atakuwa na sehemu moja, itakayopakana na nchi ya Zabuloni kuanzia mashariki hadi magharibi.
28 Mpaka wa kusini mwa Gadi kutanyooshwa kutoka Tamari hata kwenye maji ya Meriba Kadeshi, mbele hadi kijito cha Misri, na kisha hata Bahari kuu.
“Mpaka wa kusini wa Gadi utapita kusini kuanzia Tamari hadi maji ya Meriba-Kadeshi, kisha kupitia upande wa Kijito cha Misri hadi Bahari Kuu.
29 Hii ndiyo nchi ambayo mtakazo gawana; kutakuwa na urithi wa makabila ya Israeli. Haya yatakuwa mafungu yao. Hivi ndivy Bwana Yahwe asemavyo.
“Hii ndiyo nchi mtakayogawanya kuwa urithi kwa makabila ya Israeli, nazo zitakuwa sehemu zao,” asema Bwana Mwenyezi.
30 Hawa ndio watakaoishi kutoka kwenye nchi: upande wa kaskazini, ambapo patapimwa ridhaa 4, 500 kwa urefu,
“Haya yatakuwa ndiyo malango ya mji ya kutokea: Kuanzia upande wa kaskazini, ambayo urefu wake ni dhiraa 4,500, utakuwa na malango matatu,
31 kutakuwa na malango matatu, yaitwayo kwa ajili ya Israeli: lango moja kwa ajili ya Rubeni, lango moja kwa ajili ya Yuda, na lango moja kwa ajili ya Walawi.
malango hayo ya mji yatapewa majina ya makabila ya Israeli. Malango hayo matatu ya upande wa kaskazini moja litakuwa lango la Reubeni, lango la Yuda na lango la Lawi.
32 Kwa upande wa mashariki, ambapo patapimwa ridhaa 4, 500 kwa urefu, kutakuwa na malango matatu: lango moja kwa ajili ya Yusufu, lango moja kwa ajili ya Benjamini, na lango moja kwa ajili ya Dani.
“Upande wa mashariki, wenye urefu wa dhiraa 4,500, utakuwa na malango matatu: lango la Yosefu, lango la Benyamini na lango la Dani.
33 Kwa upande wa mashariki, kutakuwa na kipimo cha ridhaa 4, 500 urefu, kutakuwa na malango matatu: lango moja kwa ajili ya Simioni, lango moja kwa ajili ya Isakari, na moja kwa ajili ya Zebuloni.
“Upande wa kusini, wenye urefu wa dhiraa 4,500, utakuwa na malango matatu: lango la Simeoni, lango la Isakari na lango la Zabuloni.
34 Kwa upande wa magharibi, ambao kipimo chake kitakuwa ridhaa 4, 500, kutakuwa ba malango matatu: lango moja kwa ajili ya Gadi, lango moja kwa ajili ya Asheri, na lango moja kwa ajili ya Naftali.
“Upande wa magharibi, wenye urefu wa dhiraa 4,500, utakuwa na malango matatu: lango la Gadi, lango la Asheri na lango la Naftali.
35 Umbali kuuzunguka mji utakuwa ridhaa elfu kumi na nane; kutoka hiyo siku, jina la huo mji litakuwa “Yahwe yupo hapo.”
“Urefu wote kuzunguka utakuwa dhiraa 18,000. “Nalo jina la mji huo kuanzia wakati huo na kuendelea litakuwa: Bwana yupo hapa.”