< Ezekieli 46 >

1 Bwana Yahwe asema hivi: Lango la uzio wa ndani, linaloelekea mashariki, litafungwa kwa mda wa siku sita za kazi, lakini katika siku za Sabato litakuwa wazi, na katika siku ya mwezi mpya litafunguliwa.
主耶和华如此说:“内院朝东的门,在办理事务的六日内必须关闭;惟有安息日和月朔必须敞开。
2 Mwana wa mfalme ataingia kwa kutumia lango la njia ya nyuma ya varanda upande wa nje, na atasimama mbele ya muhimili wa mwimo wa lango la ndani wakati makuhani wakiwa wakitengeza sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya amani. Kisha ataabudu kwenye kizingiti cha lango la ndani na kutoka nje, lakini lango halitakuwa linafungwa hadi jioni.
王要从这门的廊进入,站在门框旁边。祭司要为他预备燔祭和平安祭,他就要在门槛那里敬拜,然后出去。这门直到晚上不可关闭。
3 Watu wa nchi pia wataabudu mbele ya Yahwe kwenye hili lango la kuingilia katika siku ya Sabato na siku mpya za mwezi.
在安息日和月朔,国内的居民要在这门口,耶和华面前敬拜。
4 Sadaka ya kuteketezwa ambayo mwana wa mfalme aitoayo kwa Yahwe katika siku ya Sabato itakuwa wanakondoo sita wasiokuwa na dosari na kondoo dume asiyekuwa na dosari.
安息日,王所献与耶和华的燔祭要用无残疾的羊羔六只,无残疾的公绵羊一只;
5 Sadaka ya unga pamoja na kondoo dume itakuwa efa moja, na sadaka ya unga pamoja na wanakondoo kiasi awezacho kutoa, na hini moja ya mafuta pamoja na kila efa ya unga.
同献的素祭要为公绵羊献一伊法细面,为羊羔照他的力量而献,一伊法细面加油一欣。
6 Katika siku ya mwezi mpya atatoa ng'ombe mchanga asiyekuwa na dosari kutoka kuchungwa, wanakondoo sita, na kondoo asyekuwa na dosari.
当月朔,要献无残疾的公牛犊一只,羊羔六只,公绵羊一只,都要无残疾的。
7 Atatengeneza sadaka ya unga ya efa moja kwa ajili ya ng'ombe na efa moja kwa ajili ya kondoo, na kwa kiasi awezacho kukitoa kwa ajili ya wanakondoo, na hini ya mafuta kwa kila efa ya unga.
他也要预备素祭,为公牛献一伊法细面,为公绵羊献一伊法细面,为羊羔照他的力量而献,一伊法细面加油一欣。
8 Wakati mwana wa mfalme atakapokuwa anaingia kwa njia ya lango lenye varanda, ataondoka kwa njia hiyo hiyo.
王进入的时候必由这门的廊而入,也必由此而出。
9 Lakini wakati watu wa nchi watakakuja kwa Yahwe katika sikukuu zilizoteuliwa, kila mmoja kuingia kupitia kwenye lango la kaskazini kuabudu ataondoka kupitia lango la kusini; na kila atakayeingillia kupitia lango la kusini atatoka kupitia lango la kaskazini. Hakuna atakayerudia kwa lile lango aliloingilia, kwa kuwa atatoka nje moja kwa moja.
“在各节期,国内居民朝见耶和华的时候,从北门进入敬拜的,必由南门而出;从南门进入的,必由北门而出。不可从所入的门而出,必要直往前行,由对门而出。
10 Mwana wa mfalme atakuwa kati yao; watakapoingia, ataingia ndani, na watakapoondoka, atatoka nao.
民进入,王也要在民中进入;民出去,王也要一同出去。
11 Kwenye sikukuu hizo, sadaka ya unga itakuwa efa moja ya unga kwa ng'ombe mmoja na efa moja kwa kondoo dume, na chochote atakacho kitoa pamoja na wanakondoo, na hini moja ya mafuta kwa kila efa.
“在节期和圣会的日子同献的素祭,要为一只公牛献一伊法细面,为一只公绵羊献一伊法细面,为羊羔照他的力量而献,一伊法细面加油一欣。
12 Wakati mwana wa mfalme atakapotoa sadaka atakayojisikia kutoa, labda sadaka ya kuteketezwa au sadaka ya amani kwa Yahwe, lango la kuelekea mashariki litafunguliwa kwa ajili yake. Atatoa sadaka yake ya kuteketezwa au sadaka ya amani kama afanyavyo siku ya Sabato. Kisha atatoka nje, na baada ya kutoka lango litafungwa.
王预备甘心献的燔祭或平安祭,就是向耶和华甘心献的,当有人为他开朝东的门。他就预备燔祭和平安祭,与安息日预备的一样,献毕就出去。他出去之后,当有人将门关闭。”
13 Kwa kuongeza, utatoa mwanakondoo asiyekuwa na dosari mwenye umri wa mwaka mmoja kama sadaka ya kuteketezwa kwa Yahwe kila siku; utafanya hivi kila asubuhi.
“每日,你要预备无残疾一岁的羊羔一只,献与耶和华为燔祭;要每早晨预备。
14 Utatoa sadaka ya unga pamoja nayo kila asubuhi, efa sita na sehemu ya tatu ya hini ya mafuta kuchanganya na sadaka ya unga kwa ajili ya Yahwe, kulingana na sheria ilivyo.
每早晨也要预备同献的素祭,细面一伊法六分之一,并油一欣三分之一,调和细面。这素祭要常献与耶和华为永远的定例。
15 Watandaa mwanakondoo, sadaka ya kuteketezwa, na mafuta kila asubuhi, sadaka ya kuteketezwa ya kudumu.
每早晨要这样预备羊羔、素祭,并油为常献的燔祭。”
16 Bwana Yahwe asema hivi: Kama mwana wa mfalme akitoa zawadi kwa mmoja wa watoto wake, imekuwa urithi wake. Itakuwa mali ya mtoto wake, imekuwa urithi.
主耶和华如此说:“王若将产业赐给他的儿子,就成了他儿子的产业,那是他们承受为业的。
17 Lakini kama akimpatia zawadi kutoka urithi wake kwa mmoja wa watumishi wake, kisha itakuwa ya huyo mtumishi mpaka mwaka wa uhuru, na kisha itarudi kwa mwana wa mfalme. Urithi wake yamkini ukawa kwa ajili ya watoto wake.
倘若王将一分产业赐给他的臣仆,就成了他臣仆的产业;到自由之年仍要归与王。至于王的产业,必归与他的儿子。
18 Mwana wa mfalme hatawaondolea urithi wa watu kutoka kwenye mali zao wenyewe; ataandaa kwa ajili ya watoto wake mali ili kwamba watu wangu wasitawanyike, kila mtu kutoka mali kwenye yake mwenyewe.”
王不可夺取民的产业,以致驱逐他们离开所承受的;他要从自己的地业中,将产业赐给他儿子,免得我的民分散,各人离开所承受的。”
19 Kisha yule mtu akaniletea kwenye lango la kutokea hata kwenye vyumba vitakatifu kwa ajili ya makuhani, vilivyokuwa vimeelekea kaskazini na tazama! Kulikuwa na sehemu mbele magharibi.
那带我的,将我从门旁进入之处、领进为祭司预备的圣屋,是朝北的,见后头西边有一块地。
20 Akanambia, “Hii ndio sehemu ambayo makuhani watakapo chemshia sadaka ya hatia na sadaka ya dhambi na walipookea sadaka ya unga. Wasilete sadaka nje ya uzio, kwa kuwa watu watatakaswa.”
他对我说:“这是祭司煮赎愆祭、赎罪祭,烤素祭之地,免得带到外院,使民成圣。”
21 Kisha akanileta kwenye uzio wa nje akaniongoza kuzunguka pembe nne za uzio, nikaona kwamba katika kila pembe ya uzio kulikuwa na uwanja.
他又带我到外院,使我经过院子的四拐角,见每拐角各有一个院子。
22 Katika hizo pembe nne za nje ya uzio kulikuwa na nzio nne ndogo, dhiraa arobaini urefu na thelathini upana. Ukubwa ule ule kwa nzio zote nne.
院子四拐角的院子,周围有墙,每院长四十肘,宽三十肘。四拐角院子的尺寸都是一样,
23 Kulikuwa na safu zilizokuwa zimetengenezwa kwa mawe kuzizunguka zote nne, na meko ya kupikia ilikuwa chini ya safu ya jiwe.
其中周围有一排房子,房子内有煮肉的地方。
24 Yule mtu akanambia, “Hizi ndizo sehemu ambazo watumishi watachemshia dhabihu za watu.”
他对我说:“这都是煮肉的房子,殿内的仆役要在这里煮民的祭物。”

< Ezekieli 46 >