< Ezekieli 43 >

1 Yule mtu kisha akanileta hata kwenye lango lililokuwa linaelekea mashariki.
領我到了面朝東的門那裏。
2 Tazama! Utukufu wa Mungu wa Israeli ukaja kutoka mashariki; sauti yake ilikuwa kama sauti ya maji mengi, na nchi iling'aa kwa utukufu wake.
看,以色列天主的光榮由東方而來,有一種響聲,像大水的澎湃聲,大地也因他的光榮而炫耀。
3 Yalikuwa yanalingana na sura ya ono nililolona, kulingana na ono nililokuwa nimeliona wakati alipokuja kuuteketeza mji, na maono yalikuwa kama maono ambayo niliyokuwa nimeyaona Keberi Kanali nikaanguka kifudi fudi.
我所見的神視與我前次來摧毀城市時所見的神視相似,神視的情形也與我以前在革巴爾河畔所見的神視一樣。於是我就伏地掩面。
4 Hivyo utukufu wa Yahwe ukaja kwenye nyumba ya karibu na njia ya lango lililokuwa wazi kwa upande wa magharibi.
上主的光榮由朝東的門進入聖殿。
5 Kisha Roho akanichukua na kunileta kwenye ua wa ndanni. Tazama! Utukufu wa Yahwe ulikuwa umeijaza nyumba.
神力將我提起,領我進入內院。看,上主的充滿了聖殿。
6 Mtu alisimama karibu na mimi, na nikamsikia mtu mwingine akizungumza na mimi kutoka kwenye nyumba.
當那人站在我身旁時,我聽見殿內有一位向我說話的,
7 Akanambia, “Mwanadamu, hapa ndipo mahali pangu pa enzi na mahali kwa ajili ya ya miguu yangu, ambapo nitaishi kati ya watu wa Israeli milele. Nyumba ya Israeli haitalikufuru tena jina langu takatifu-wao au wafalme wao katika mahali patakatifu pao.
對我說:「人子,這是安放我寶座的地方,這是我腳掌所踏的地方,我願在這裏永遠住在以色列子民中。以色列家族,他們和他們的的君王,不再以淫亂和自己君王的屍體,玷污我的聖名。
8 Hawatalikufuru tena jina langu takatifu kwa kuweka kizingiti chao karibu na kizingiti changu, na nguzo yao ya lango karibu na nguzo yangu ya lango, bila kitu lakini ukuta kati yangu na wao. Wamelikufuru jina langu kwa matendo yao machafu, hivyo nimewala kwa hasira yangu.
因為他們靠著我的門限安置他們的門限,在我與他們之間僅有一牆之隔。他們曾以自己所行的邪惡之事玷污了我的聖名,為此,我發怒將他們予以消滅。
9 Sasa waache waondoe udanganyifu wao na maiti za wafalme wao kutoka kwangu, na nitaishi katikati yao milele.
現今他們要從我面前,除去他們的淫亂和君王的屍體,這樣我要永遠住在他們中。
10 Mwanadamu, wewe mwenyewe utaiambia nyumba ya Israeli kuhusu nyumba hii hivyo watajiskia aibu ya uovu wao. Wanaweza kutafakari kuhusu haya maelezo.
人子,你要向以色列家族闡述這聖殿,使他們對自己的所行感到慚愧;闡述聖殿的完美和構造,
11 Kwa kuwa wameaibika kwa yote waliyoyafanya, kisha waonyeshe mchoro wa nyumba, maelezo yake, matokeo yake, maingio yake, na mchoro wake, sheria zake zote na kanuni. Kisha andika hivi chini mbele ya macho yao ili waweze kutunza michoro yote na kanuni zake zote, hivyo kama wazitiivo.
叫他們對自己的所行的醜事而感到慚愧。你要劃出殿的圖形、結構、出路、進口和所有的式樣,並將各種規定和和種法律告知他們,在他們眼前寫出好叫他們遵守各種法律和規定,一一奉行。
12 Hii ndiyo sheria kwa ajili ya nyumba: Kutoka kwenye kilele cha mlima hata mpaka wote unaoizunguka, patakuwa patakatifu sana. Tazama! Hii ndiyo sheria kwa ajili ya nyumba.
這是關於聖殿的規定:山頂周圍所有之地,是神聖不可侵犯的。
13 Hivi vitakuwa vipimo vya madhabahu katika dhiraa-hiyo dhiraa kuwa dhiraa ya kawaida na urefu wa kiganja. Hivyo mfereji ulio uzunguka madhabahu utakuwa dhiraa moja chini, na upana wake pia utakuwa dhiraa moja. Mpaka wa karibu uizungukayo machinjio shubiri moja. Hii itakuwa kitako cha madhabahu.
祭壇按肘──肘為一肘加一掌──的尺寸如下:底座高一肘,邊寬一肘,在底座四周邊緣有一掌深的溝漕:這是壇座。
14 Usawa wa kutoka kwenye mferji hadi kwenye machinijo ya chini ya madhabahu itakuwa dhiraa mbili, na hiyo machinjio yenyewe itakuwa dhiraa moja upana. Kisha kutoka machinjio madogo hadi kwenye machinjio makubwa ya madhabahu, itakuwa dhiraa nne, na machinjio makubwa yatakuwa dhraa moja upana.
地上的底座到下層台座高二肘,邊寬一肘;從小台座到大台座高四肘,邊寬一肘。
15 Meko juu ya madhabahu kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa ni dhiraa nne juu, na kuna pembe nne zilizoelekea juu kwenye meku.
至於壇爐,高四肘;壇爐之上有四個角突出,高一肘。
16 Meku ina dhiraa kumi na moja urefu na dhiraa kumi na mbili upana, za mraba.
壇爐一二肘畏,十二肘寬;四面成一正方形。
17 Mpaka wake ni dhiraa kumi na nne urefu na dhiraa kumi na nne upana pande zake zote nne, na ukingo wake ni nusu dhiraa upana. Mfereji ni dhiraa moja upana kuzuka kote pamoja na ngazi zielekeazo mashariki.”
台座十四肘長,面面共十四肘寬;四周有半肘的溝槽;周圍還有寬一肘的底座。石階向東。
18 Kisha akanambia, “Mwanadamu, Bwana Yahwe asema hivi: Hizi ndizo sheria kwa ajili ya madhabahu katika siku watakayoitengeza, kwa ajili kutoa sadaka ya kuteketezwa kwenye hiyo, na kwa jili ya kunyunyiza damu juu yake.
以後他向我說:「人子,吾主上主這樣說:祭壇造成之日,在上面獻全燔祭和灑血的規定如下:
19 Utatoa ng'ombe kutoka kwenye kundi kama sadaka ya dhambi kwa ajili ya Walawi makuhani ambao ni uzao wa Zadoki, wale wajao karibu nami kunitumikia-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
你應給那走近我事奉我的匝多克的後裔肋未司祭──吾主上主的斷語──一頭牛犢,獻為贖罪祭。
20 Kisha utachukua baadhi ya damu yake na kuiweka juu pembe nne za madhabahu na pande nne za machinjio na kuuzunguka ukingo; utaitakasa na kufanya upatanisho kwa ajili yake.
你要取血塗在祭壇的四角,台座的四角和周圍的溝槽上,應這樣為祭壇贖罪取潔。
21 Kisha chukua ng'ombe kama sadaka ya dhambi na iteketezwe katika eneneo lililotengwa la nje ya patakatifu.
此外,再取一頭公牛作贖罪祭,在聖殿固定的地方,聖所之外,將牠焚化。
22 Kisha katika siku ya pili utatoa mbuzi dume asiyekuwa na dosari kutoka kundini kama sadaka ya dhambi; makuhani wataisafisha madhabahu kama walivyoisafisha kwa ng'ombe.
第二天要獻一隻無瑕的小公山羊為贖罪祭,如獻公牛犢所行的一樣,為祭壇取潔。
23 Utakapomaliza kusafisha, toa ng'ombe asiyekuwa na dosari kutoka kwenye mifugo na kondoo dume asiyekuwa na dosari kutoka kundini.
你行完贖罪祭之後,應獻一頭無瑕的公牛和羊群中一隻無瑕瑕的公羊,
24 Watoe mbele ya Yahwe; makuhani watanyunyiza chumvi juu yao na kuwainua juu kama sadaka ya kutekezwa kwa Yahwe.
把牠獻在上主前,司祭在上面撒上鹽,獻予上主為全燔祭。
25 Utaandaa mbuzi dume kama sadaka ya dhambi kila siku kwa mda wa siku saba, na makuhani pia wataandaa ng'ombe asiye na dosari kutoka kwenye kundi na kondoo dume kutoka kwenye kundi.
七天之久,你應每天獻一隻公山羊為贖罪祭,還應獻一頭公牛和羊群中一隻公羊,都應純潔無瑕。
26 Wataipatanisha madhabahu kwa siku saba na kuitakasa, wataitakasa kwa njia hii.
七天之久為祭壇贖罪取潔,予以祝聖。
27 Watamaliza hizi siku saba, na katika siku ya nane na kuendelea itakuwa kwamba makuhani wataandaa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani kwenye madhabahu, ndipo nitakapowakubali-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”
這日期滿了,即第八日及以後,司祭才可以在祭壇上奉獻你們的全燔祭與和平祭,如此我才喜悅你們──吾主上主的斷語。」

< Ezekieli 43 >