< Ezekieli 42 >

1 Kisha yule mtu akanituma kwenda ua wa nje upande wa kaskazini, akanileta kwenye vyumba mbele ya ua wa nje na ukuta wa nje kaskazini.
Ndipo yule mtu akaniongoza kuelekea kaskazini mpaka kwenye ua wa nje na kunileta mpaka kwenye vyumba vinavyoelekeana na ua wa Hekalu na kuelekeana na ukuta wa nje upande wa kaskazini.
2 Hivyo vyumba vilikuwa dhiraa mia moja karibu na mbele yake na dhiraa hamsini upana.
Jengo ambalo mlango wake ulielekea kaskazini lilikuwa na urefu wa dhiraa mia moja na upana wa dhiraa hamsini.
3 Baadhi ya hivyo vyumba vilielekea ua wa ndani na vilikuwa na dhiraa ishirini kutoka patakatifu. Kulikuwa na vyumba vitatu vinavyolingana, na kingine juu kilichokuwa kimetazama chini kuelekea kingine vilikuwa vimefunguliwa, vilikuwa na pakutokea. Baadhi ya vyumba vilielekea nje kwenye ua wa nje.
Mbele ya zile dhiraa ishirini za ule ua wa ndani unaoelekeana na ile njia ya ua wa nje, kuliinuka vyumba virefu kimoja baada ya kingine vya ghorofa tatu.
4 Njia dhiraa kumi upana dhiraa mia moja urefu kueleikea mbele ya vyumba. Milango ya vyumba ilikuwa mbele kaskazini.
Mbele ya hivi vyumba kulikuwa na njia ya ndani yenye upana wa dhiraa kumi na urefu wa dhiraa mia moja. Milango yake ilikuwa upande wa kaskazini.
5 Lakini kumbi za juu zilikuwa ndogo, kwa ajili ya njia za kutembea zilichukua kutoka kwazo sehemu kubwa kulikuwa walivyofanya kwenye vyumba vya chini na katikati usawa wa jengo.
Basi vyumba vya juu vilikuwa vyembamba zaidi, kwa kuwa ujia ulichukua nafasi zaidi ndani yake kuliko katika vyumba vya sakafu ya chini na vya katikati ya jengo.
6 Kwa kuwa orofa tatu hapakuwa na mihimili, kama zile nyua, ambazo zilikuwa na mihimili. Hivyo usawa wa vyumba vya juu vilikuwa sawa sawa katika kipimo cha kulinganisha na vyumba vya chini na usawa wa katikakati.
Vyumba katika ghorofa ya tatu havikuwa na nguzo, kama kumbi zilivyokuwa nazo, kwa hiyo eneo la sakafu ya vyumba vya juu lilikuwa ni dogo kuliko la sakafu ya chini na ya kati.
7 Ukuta wa nje karibu na vyumba mbele ya ua wa nje, ua uliokuwa mbele ya vyumba. Huo ukuta ulikuwa dhiraa hamsini urefu.
Kulikuwa na ukuta wa nje uliokuwa sambamba na vile vyumba na ukumbi wa nje, ulitokeza urefu wa dhiraa hamsini.
8 Urefu wa vyumba vya ua wa nje ulikuwa dhiraa hamsini, na vyumba vilivyokuwa vimeelekea patakatifu vilikuwa dhiraa mia moja urefu.
Wakati safu ya vyumba katika ua wa nje vilikuwa na urefu wa dhiraa hamsini, vile vyumba vilivyokuwa karibu zaidi na Hekalu vilikuwa na urefu wa dhiraa mia moja.
9 Kulikuwa na mahali pa kuingilia kwenye vyumba vidogo zaidi kutoka upande mashariki, kuingia kutoka ua wa nje.
Vyumba vya chini vilikuwa na ingilio upande wa mashariki unapoingia kutoka ukumbi wa nje.
10 Karibu na ukuta wa ua wa nje juu ya upande wa mgaribi pa ua wa ndani, mbele ya patakatifu pa ua wa nje, pia kulikuwa na vyumba na njia ya mbele yao.
Upande wa kusini kufuata urefu wa ukuta wa ukumbi wa nje, unaopakana na ukumbi wa Hekalu na kuelekeana na ukuta wa nje, kulikuwa na vyumba
11 zilikuwa kama umbo la vyumba kwa upande wa kaskazini. Zilikuwa urefu ule ule na upana na matokeo yale yale na mipangilio na madirisha.
vyenye ujia unayopita mbele yake. Hivi vilifanana na vile vyumba vya upande wa kaskazini, vilikuwa na urefu na upana ulio sawa, mahali pa kutokea na vipimo vyake vilikuwa sawa. Kama ilivyokuwa milango ya upande wa kaskazini,
12 Kwa upande wa kusini kulikuwa na madirisha kwenye vyumba ambavyo vilikuwa kama yale yaliyokuwa upande wa kaskazini. Aya iliyokuwa ndani ilikuwa na mlango kwenye kichwa chake, na njia ilifunguliwa kwenye vyumba tafauti. Upande mashariki kulikuwa na malango wa njia kwenye njia mwishoni.
ndivyo ilivyokuwa milango ya vyumba vya upande wa kusini. Kulikuwa na ingilio kuanzia mwanzo wa njia ambao ulikuwa sambamba na ukuta wa pili uliokuwa upande wa mashariki, ambako ndiko kwa kuingia vyumbani.
13 Kisha yule mtu akanambia, “Vyumba vya kaskazini na vyumba vya kusini vilivyokuwa mbele ya ua wa nje ni vyumba vitakatifu amabapo makuhani wafanyao kazi karibu sana na Yahwe waweze kula chakula kitakatifu sana. Wataweka vitu vitakatifu sana-sadaka ya chakula, sadaka ya dhambi, na sadaka ya hatia-kwa kuwa hapa ni mahali patakatifu.
Kisha akaniambia, “Vyumba vya upande wa kaskazini na vya upande wa kusini ambavyo vinaelekeana na ukumbi wa Hekalu ni vyumba vya makuhani, mahali ambapo wale makuhani ambao humkaribia Bwana watakula zile sadaka takatifu sana. Huko ndiko watakakoweka zile sadaka takatifu sana, yaani, sadaka za nafaka, sadaka za dhambi na sadaka za hatia, kwa kuwa mahali ni patakatifu.
14 Wakati makuhani watakapoingia hapo, wasitoke nje ya mahali patakatifu kwa ua wa nje, bila kuweka mavazi karibu mahali wahudumupo, kwa kuwa hapa ni patakatifu. Hivyo watavalia mahali pengine nguo kabla ya kwenda karibu na watu.”
Mara makuhani waingiapo mahali patakatifu, hawaruhusiwi kwenda kwenye ukumbi wa nje mpaka wayaache mavazi ambayo walivaa wakiwa wanahudumu, kwa kuwa hayo mavazi ni matakatifu. Inawapasa kuvaa mavazi mengine kabla hawajakaribia eneo lililo wazi kwa ajili ya watu.”
15 Yule mtu akamaliza kupima ndani ya nyumba na kisha akanichukua nje ya lango lililokuwa limeelekea magharibi na kuzipima sehemu zote zilizokuwa zimepazunguka hapo.
Alipomaliza kupima vile vilivyokuwa katika eneo la ndani la Hekalu, akanitoa nje kupitia lango la upande wa mashariki na kupima eneo lote linalozunguka:
16 Akaupima upande wa mashariki na fimbo ya kupimia-dhiraa mia tano kwa fimbo ya kupimia.
Akapima upande wa mashariki kwa ule ufito wa kupimia, nao ulikuwa dhiraa 500
17 akaupima upande wa kaskazini-dhiraa mia tano na fimbo ya kupimia.
Akapima upande wa kaskazini, nao ulikuwa dhiraa 500 kwa ufito ule wa kupimia.
18 Pia akaupima upande wa kusini dhraa mia tano na fimbo ya kupimia.
Tena akapima upande wa kusini, nao ulikuwa dhiraa 500 kwa ufito ule wa kupimia.
19 Pia akageuka na kuupima upande wa magharibi dhiraa mia tano kwa fimbo ya kupimia,
Kisha akageukia upande wa magharibi na kuupima, ulikuwa dhiraa 500 kwa ufito ule wa kupimia.
20 Akaipima pande nne. Ilikuwa na ukuta umeizunguka ilikuwa dhiraa mia tano urefu, na dhiraa mia tano upana, kulitenganisha umbo takatifu kutoka ambapo ni pa kawada.
Hivyo akapima eneo katika pande zote nne. Lilikuwa na ukuta kulizunguka wenye urefu wa dhiraa 500 na upana wa dhiraa 500, uliotenganisha mahali Patakatifu na eneo la watu wote.

< Ezekieli 42 >