< Ezekieli 40 >
1 Katika mwaka wa ishirini na tano wa kuhamishwa kwetu mwanzoni mwa mwaka siku ya kumi ya mwezi, katika mwaka wa kumi na nne baada ya mji kuchukuliwa-katika siku hiyo hiyo, mkono wa Yahwe ulikuwa juu yangu na alinichukua huko.
2 Katika maono ya Mungu akanileta hata nchi ya Israeli. Akanileta kupumzika juu ya kila mlima mrefu sana; upande wa kusini kulikuwa na monekano kana kwamba majengo ya mji.
3 Kisha akanileta huko. Tazama, kulikuwa na mtu! Mwonekano wake ulikuwa kama mwonekano wa shaba. Alikuwa na uzi wa kitani na mwanzi wa kupimia mkononi mwake, na alisimama katika lango la mji.
4 Huyo mtu akanambia, “Mwanadamu, tazama kwa macho yako na sikiliza kwa masikio yako, na elekeza moyo wako juu ya yote ninayokufunulia, kwa kuwa ulinileta hapa ili niweze kukufunulia haya wewe. Toa taarifa ya kila kitu utakachokiona kwa nyumba ya Israeli.
5 Kulikuwa ukuta uliokuwa umezunguka eneo la hekalu. Urefu wa kipimo cha mwanzi katika mkono wa mtu ulikuwa dhiraa sita urefu, kila urefu wa dhiraa ulikuwa dhiraa moja na kipimo cha kiganja cha mkono urefu. Aliupima ukuta; ulikuwa kipimo cha mwanzi mmoja na ufito mmoja urefu.
6 Kisha akaenda hata kwenye lango la hekalu lililokuwa limeelekea mashariki. Akapanda ngazi na kuipima kizingiti cha lango-mwanzi mmoja upana.
7 Vyumba vya ulinzi vilikuwa kila mwanzi mmoja urefu na mwanzi mmoja upana; kulikuwa na dhiraa tano katika kila vyumba viwili, na kizingiti cha lango la hekalu karibu na tawa la hekalu kilikuwa mwanzi mmoja urefu.
8 Akapima tawa la lango; ulikuwa mwanzi mmoja urefu.
9 Akapima tawa la lango. Ilikuwa mwanzi mmoja kwenda chini. Mihimili ilikuwa dhiraa mbili upana. Hili lilikuwa tawa la lango kuelekea hekalu.
10 Kulikuwa na vyumba vitatu vya ulinzi pande zote za lango la mashariki, na yote yalikuwa na kipimo kile kile, na kuta zilizokuwa zimezigawanya zilikuwa na kipimo kile kile.
11 Kisha yule mtu akapima upana wa njia ya lango la kuingia-dhiraa kumi; na akapima urefu wa njia ya lango la kuingia-dhiraa kumi na tatu.
12 Akaupima ukuta uliokuwa mpaka mbele ya vyumba-dhiraa moja urefu. Vyumba vilipimwa dhiraa sita kila upande.
13 Kisha akapima lango la njia kutoka kwenye paa ya chumba kimoja kuelekea chumba kingine-dhiraa ishirini na tano, kutoka lango la kuingia chumba cha kwanza kuelekea kile cha pili.
14 Kisha akapima ukuta uliokuwa umeenda kati ya vyumba vya ulinzi-dhiraa sitini urefu; alipima kwa mbali na tawa la lango.
15 Lango la kuingia kutoka lango la mbele kuelekea lango jingine la tawa la mwisho lilikuwa dhiraa hamsini.
16 Kulikuwa na madirisha yaliyokuwa yamefungwa kuelekea vyumba na kuelekea nguzo zake kati ya malango kuzunguka kote; na vivyo hivyo kwa mabaraza. Kulikuwa na madirisha pande zote za ndani, na kila mhimili ulikuwa umepambwa kwa mitende.
17 Kisha huyo mtu akanileta hata ua wa nje mwa hekalu. Tazama, kulikuwa na vyumba, na kulikuwa na kibamba katika ua, pamoja na vyumba thelathini baada ya kibamba.
18 Kibamba kilienda juu hata upande wa malango, na upana wake ulikuwa sawsawa na urefu wa malango. Hiki kilikuwa kibamba cha chini.
19 Kisha huyo mtu akapima umbali kutoka mebele ya lango la chini hata mbele ya lango la ndani; ilikuwa dhiraa mia moja upande wa mashariki, na sawasawa na upande wa kaskazini.
20 Kisha akapima urefu na upana wa lango lililokuwa upande wa kaskazini mwa ua wa nje.
21 Kulikuwa na vyumba vitatu pande zote za lango, na lango na matawa yake yalipimwa sawa na lango kubwa-dhiraa hamsini upana wote na dhiraa ishirini na tano upana.
22 Madirisha yake, tawa, vyumba, na mitende yake vilikabiliana na lango ambalo linaloelekea mashariki. Ngazi saba kuupandia juu hata kwenye tawa lake.
23 Kulikuwa na lango kwenye ua wa ndani mbele kuelekea mashariki; huyo mtu alipima kutoka lango moja hadi lango jingine-dhiraa mia moja umbali.
24 Kisha huyo mtu akanileta hata kwenye lango la kuingia la kusini, na kuta zake na tawa vilipimwa sawa kama malango mengine ya nje.
25 Kulikuwa na madirisha yaliyofungwa katika lango la njia na tawa lake kama lile lango. Lango la kusini na tawa lake vilipimwa dhiraa hamsini urefu na dhiraa ishirini na tano upana.
26 Kulikuwa na ngazi saba hadi kwenye lango na matawa yake, na kulikuwa na mitende iliyochongoka juu ya kuta pande zote.
27 Kulikuwa na lango la ua wa ndani upande wa kusini, na yule mtu akapima kutoka hilo lango hata lango la kuingia upande wa kusini-dhiraa mia moja umbali.
28 Kishi huyo mtu akanileta hata ua wa ndani karibu na lango lake la kusini, ambalo lilikuwa na vipimo vile vile kama malango mengine.
29 Vyumba vyake, kuta, na matao vilipimwa sawa kama malango mengine; kulikuwa na madirisha kuzunguka matao yote. Lango la ndani na matao yake yalipimwa dhiraa hamsini urefu na dhiraa ishirini na tano upana.
30 Pia kulikuwa na matao pande zote za kuta za ndani; haya yalikuwa dhiraa ishirini na tano urefu na dhiraa tano upana.
31 Hili tawa lilielekea ua wa nje pamoja na mitende iliyochongwa juu ya kuta zake na ngazi nane kuupandia.
32 Kisha yule mtu akanileta hata kwenye ua wa ndani karibu na njia ya kaskazini na kulipima lango, ambalo lilikuwa na vipimo sawa kama malango mengine.
33 Vyumba vyake, kuta, na matawa yalikuwa na kipima sawa kama cha malango, na kulikuwa na madirisha pande zote. Laango la ndani na matawa yake yalikuwa dhiraa hamsini urefu na dhiraa ishirini na tano upana.
34 Matawa yake yalielekea nje ya ua; ilikuwa na mitende pande zote za hiyo na ngazi nane za kuupandia.
35 Kisha huyo mtu akanileta hata lango la kaskazini na kulipima; likapimwa vivyo hivyo kama malango mengine.
36 Vyumba vyake, kuta, na ukumbi vilipimwa sawa na malango mengine, na kulikuwa na madirisha pande zote. Njia ya lango na matao yake yalipimwa dhiraa hamsini urefu na upana dhiraa ishirini na tano.
37 Tatawa lake lilielekea ua wa nje; ilikuwa na mitende pande zote za huo na ngazi nane kuupandia.
38 Kulikuwa na chumba pamoja na mlango karibu na kila lango la ndani. Hapa ndipo ambako walipooshea sadaka za kutekezwa.
39 Kulikuwa na meza mbili kila upande wa kila ukumbi, ambako sadaka ya kuteketezwa ilipochinjiwa, na pia sadaka ya dhambi na sadaka ya hatia.
40 Karibu na ukuta wa ua, kuelekea juu kwenye lango kuelekea kaskazini, kulikuwa na meza mbili. Pia kwa upande mwingine kulikuwa na meza mbili kwenye lango la ukumbi.
41 Kulikuwa na meza nne pande zote karibu na lango; wakachinja wanyama juu ya meza nane.
42 Kulikuwa na meza nne za mawe yaliyochongwa kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, dhiraa moja na nusu urefu, dhiraa moja na nusu upana, na kimo dhiraa moja. Juu yake waliweka vyombo pamoja ambavyo walivichinjia sadaka za kuteketezwa kwa ajili ya sadaka.
43 Kulabu mbili ujazo wa kiganja urefu uliokuwa umeunganishwa katika ua pande zote, na nyama ya matoleo ilikuwa imewekwa juu ya meza.
44 Karibu na lango la ndani, katika ua wa ndani, kulikuwa na vyumba vya waimbaji. Moja ya hivi vyumba kilikuwa upande wa kaskazini, na kingine kusini.
45 Kisha yule mtu akanambia, “Hiki chumba kinachoelekea kusini ni kwa ajili ya makuhani walio zamu katika hekalu.
46 Chumba kilichoelekea kaskazini kilikuwa kwa ajili ya makuhani waliokuwa zamu kwenye madhabahu. Hawa ni wana wa Sadoki ambaye huja humkaribia Yahwe kumtumikia; ambao ni miongoni mwa wana wa Lawi.”
47 Kisha akaupima ule ua-dhiraa mia moja urefu na dhiraa mia moja upana mraba, pamoja na madhabahu mbele ya nyumba.
48 Kisha yule mtu akanileta hata kwenye varanda ya nyumba na kupima mwimo wa milango yake-ilikuwa dhiraa tano unene upande huu. Njia ya kuingilia yenyewe ilikuwa dhiraa kumi na nne, na kuta pande zote za huo zilikuwa dhraa tatu upana.
49 Urefu wa ukumbi ulikuwa dhiraa ishirini, na upana wake ulikuwa dhiraa kumi na moja. Kulikuwa na ngazi zilizokuwa zimepanda juu na nguzo zilizokuwa zimesimama pande zote za huo.