< Ezekieli 4 >
1 “Lakini wewe, mwana wa adamu, chukua tofali wewe mwenyewe na uliweke mbele yako. Kisha chonga mji wa Yerusalemu juu yake.
Et tu fili hominis sume tibi laterem, et pones eum coram te: et describes in eo civitatem Ierusalem.
2 Kisha laza kuizunguka, ngome juu yake. Anza kushambulia juu yake na weka makambi kuizunguka. Weka shambulio la ghasia kuizunguka.
Et ordinabis adversus eam obsidionem, et aedificabis munitiones, et comportabis aggerem, et dabis contra eam castra, et pones arietes in gyro.
3 Kisha chukua kwa ajili yako mwenyewe sufuria ya chuma na itumie kama ukuta wa chuma kati yako mwenyewe na mji na weka uso wako dhidi yake. Kwa kuwa utazingirwa, na utaweka ukombozi juu yake. Hii itakuwa alama kwa nyumba ya Israeli.
Et tu sume tibi sartaginem ferream, et pones eam in murum ferreum inter te, et inter civitatem: et obfirmabis faciem tuam ad eam, et erit in obsidionem, et circumdabis eam: signum est domui Israel.
4 Kisha, lala juu upande wako wa kushoto na weka dhambi ya nyumba ya Israeli juu yake; utazibeba dhambi zao kwa hesabu za siku ambazo ulizolala juu ya nyumba ya Israeli.
Et tu dormies super latus tuum sinistrum, et pones iniquitates domus Israel super eo numero dierum, quibus dormies super illud, et assumes iniquitatem eorum.
5 Mimi mwenyewe nakuagiza kwako siku moja kuwakilisha kila mwaka wa adhabu yao: siku 390! Katika njia hii, utachukua dhambi ya nyumba ya Israeli.
Ego autem dedi tibi annos iniquitatis eorum, numero dierum trecentos et nonaginta dies: et portabis iniquitatem domus Israel.
6 Wakati utakapomaliza hizi siku, kisha lala chini kwa mara ya pili kwa upande wako wa kulia, kwa kuwa utabeba dhambi ya nyumba ya Yuda kwa siku arobaini. Nakuteua wewe siku moja kwa kila mwaka.
Et cum compleveris haec, dormies super latus tuum dexterum secundo: et assumes iniquitatem domus Iuda quadraginta diebus. diem pro anno, diem, inquam, pro anno dedi tibi.
7 Weka uso wako chini kuelekea Yerusalemu ambayo ni chini ya ngome, na kwa mkono wako funua unabii dhidi
Et ad obsidionem Ierusalem convertes faciem tuam, et brachium tuum erit extentum: et prophetabis adversus eam.
8 yake. Tazama! naweka vifungo juu yako hivyo hutarudi kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine hadi utakapoliza siku zako za kuzingirwa kwako.
Ecce circumdedi te vinculis: et non te convertes a latere tuo in latus aliud, donec compleas dies obsidionis tuae.
9 Chukua ngano kwa ajili yako, shayiri, dengu, mtama, kusemethi; viweke kwenye chombo kimoja na tengeneza mkate kwa ajili yako kulingana na hesabu ya siku ambazo utakazo lala katika ya upande wako. Kwa siku 390 utaula.
Et tu sume tibi frumentum, et hordeum, et fabam, et lentem, et milium, et viciam: et mittes ea in vas unum, et facies tibi panes numero dierum, quibus dormies super latus tuum: trecentis et nonaginta diebus comedes illud.
10 Chakula utakachokula kitapimwa, shekeli ishirini kwa siku, na utakila kwa mda uliopangwa kila siku.
Cibus autem tuus, quo vesceris, erit in pondere viginti stateres in die: a tempore usque ad tempus comedes illud.
11 Kisha utakunywa maji, kwa kuyapima sehemu ya sita ya hini, na utayanywa kwa mda uliopangwa.
Et aquam in mensura bibes, sextam partem hin: a tempore usque ad tempus bibes illud.
12 Utakila kama keki za shayiri, lakini utaioka kwenye kinyesi kikavu cha mwanadamu mbele ya macho yao!”
Et quasi subcinericium hordeaceum comedes illud: et stercore, quod egreditur de homine, operies illud in oculis eorum.
13 Kwa kuwa Yahwe asema, “Hii inamaana kwamba ule mkate ambao watu wa Israeli watakula kitakuwa kinajisi, huko miongoni mwa mataifa ambapo nitakaowafukuza.”
Et dixit Dominus: Si comedent filii Israel panem suum pollutum inter Gentes, ad quas eiiciam eos.
14 Lakini nikasema, “Ee, Bwana Yahwe! Sijawahi kuwa najisi! sijawahi kula kitu chochote ambacho kimekufa au kitu chochote kilichouawa na wanyama, kutoka mdomoni mwangu hadi sasa, wala nyama ya kunuka haijawahi kuingia kinywani mwangu!”
Et dixi: Ah, ah, ah, Domine Deus, ecce anima mea non est polluta, et morticinum, et laceratum a bestiis non comedi ab infantia mea usque nunc, et non est ingressa in os meum omnis caro immunda.
15 Ndivyo alivvyo niambia, “Tazama! Nimekupa mbolea ya ng'ombe badala ya kinyesi cha mwanadamu ili uweze kuandaa mkate wako juu ya hayo.”
Et dixit ad me: Ecce dedi tibi fimum boum pro stercoribus humanis: et facies panem tuum in eo.
16 Pia akanambia, “Mwana wa adamu! Tazama! Nalivunja gongo la mkate katika Yerusalemu, na watakula mkate ukiwa umepimwa katika wasiwasi na kunywa maji kwa kuyapima katika hofu.
Et dixit ad me: Fili hominis: Ecce ego conteram baculum panis in Ierusalem: et comedent panem in pondere, et in solicitudine: et aquam in mensura, et in angustia bibent:
17 Kwa sabau watapungukiwa na mkate na maji, kila mtu atafadhaishwa na ndugu yake na kumpoteza kwa sababu ya udhalimu wao.”
Ut deficientibus pane et aqua, corruat unusquisque ad fratrem suum: et contabescent in iniquitatibus suis.