< Ezekieli 38 >

1 Neno la Yahwe likanijia, likisema,
Neno la Bwana likanijia kusema:
2 “Mwanadamu, weka uso wako kumwelekea Gogu, nchi ya Magogu, kiongozi mkuu wa Mesheki na Tubali; na kutabiri dhidi yake.
“Mwanadamu, kaza uso wako dhidi ya Gogu, katika nchi ya Magogu, mkuu wa Roshi, Mesheki na Tubali, tabiri dhidi yake
3 Sema, 'Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Ni juu yako, Gogu, kiongozi mkuu wa Mesheki na Tubali.
na useme: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ee Gogu, mimi ni kinyume nawe, mtawala mkuu wa Roshi, Mesheki na Tubali.
4 Hivyo nitakugeuza na kuweka kulabu kwenye taya yako; nitakupeleka nje pamoja na jeshi lako lote, farasi, na waendesha farasi, wote wakiwa wamevaa silaha, kusanyiko kubwa pamoja na ngao ndogo na ngao kubwa, wote wakishikilia panga!
Nitakugeuza kuelekea ulikotoka na kukutia ndoana kwenye mataya yako na kukutoa nje wewe pamoja na jeshi lako lote, yaani, farasi wako, wapanda farasi wako waliojiandaa tayari kwa vita, pamoja na kundi kubwa la wajeuri wakiwa na ngao na vigao, wote wakipunga panga zao.
5 Persia, Kushi, Uajemi wapo pamoja nao, wote pamoja na ngao na chapeo!
Uajemi, Kushi na Putu watakuwa pamoja nao, wote wakiwa na ngao na kofia za chuma,
6 Gomeri na jeshi lake lote, na Beth-Togarma, kutoka sehemu za mbali ya kaskazini, na jeshi lake lote! Watu wengi wako pamoja nawe!
pia Gomeri pamoja na vikosi vyake vyote, na Beth-Togarma kutoka kaskazini ya mbali pamoja na vikosi vyake vyote, mataifa mengi wakiwa pamoja nawe.
7 Kuwa tayari! Ndio, jiandae na jeshi lako waliokusanyika pamoja na wewe, na amiri wao mkuu.
“‘Jiandae, uwe tayari, wewe na makundi yako yote ya wajeuri yaliyokusanyika pamoja nawe, nawe waamrishe.
8 Utaitwa baada ya siku nyingi, na baada ya miaka michache utaenda kwenye nchi iliyofunikwa kutoka upanga na ambayo iliyokusanywa kutoka watu wengi, iliyowkusanya kuwarudisha milima ya Israeli ambayo imeendelea kuangamizwa. Lakini watu wa nchi watatolewa na kabila za watu, na wataishi salama, wote!
Baada ya siku nyingi utaitwa vitani. Katika miaka ijayo, utaivamia nchi ile ambayo imepona kutoka vita, ambayo watu wake walikusanywa kutoka mataifa mengi kuja katika milima ya Israeli, ambayo kwa muda mrefu ilikuwa imeachwa ukiwa. Wameletwa kutoka mataifa na sasa wote wanaishi katika hali ya salama.
9 Hivyo utapanda juu kama tufani iendavyo; utakuwa kama wingu lililofunika nchi, wewe na jeshi lako lote, maaskari wako wote pamoja na wewe.
Wewe na vikosi vyako vyote na mataifa mengi yaliyo pamoja nawe mtapanda juu, mtawazoa kama tufani na kuifunika nchi kama wingu.
10 Bwana Yahwe asema hivi: Itakuwa siku hiyo hayo mawazo yataingia moyoni mwako, na utatunga njama mbaya.'
“‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Katika siku ile mawazo yataingia moyoni mwako nawe utapanga mipango mibaya.
11 Kisha utasema, 'nitapanda hata nchi iliyowazi; nitaenda hata kwa watu wapole waishio salama, wote wakiishi mahali ambapo hakuna kuta wala makomeo, na mahali ambapo hakuna malango ya mji.
Utasema, “Nitapigana vita na nchi ambayo vijiji vyake havina maboma. Nitawashambulia watu wanaoishi kwa amani na wasiotarajia vita: wote wanaishi bila maboma na bila malango na makomeo.
12 Nitanyakua mateka na kuiba mateka, ili nilete mkono wangu juu kuwaangamiza wale wakazi wapya, na juu ya watu waliokusanyika kutoka mataifa, watu wale waongezao wanyama na mali, na wale waishio katikatika ya dunia.'
Nitateka mateka na kuchukua nyara mali za wale waliorudi kuishi katika mahame na wale watu waliokusanywa kutoka kwa mataifa, ambao sasa wana mifugo na mali nyingi, wanaoishi katikati ya nchi.”
13 Sheba na Denani, na wafanya biashara wa Tarshishi pamoja na mahodari wake wote watakwambia, 'Je, umekuja kuteka nyara? Je, umewakusanya majeshi yako kuchukua mateka, kuchukua fedha na dhahabu, kuchukua mifugo yao na mali na kuwakokota mateka wengi sana?'
Sheba na Dedani pamoja na wafanyabiashara wa Tarshishi na vijiji vyake vyote watakuambia, “Je, umekuja kuteka mateka? Je, umekusanya makundi yako ya wajeuri ili kuchukua nyara mali, kutwaa fedha na dhahabu, kutunyangʼanya mifugo na mali na kuteka nyara nyingi zaidi?”’
14 Kwa hiyo tabiri, mwanadamu, na mwambie Gogu, 'Bwana Yahwe asema hivi: Katika siku hiyo, wakati watu wangu Israeli watakapoishi salama, je, hutajifunza kuhusu wao?
“Kwa hiyo, mwanadamu, tabiri na umwambie Gogu: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Katika siku ile, watu wangu Israeli watakapokuwa wanaishi salama, Je, wewe mwenyewe hutalijua hilo?
15 Utakuja kutoka mahali pangu mbali katika kaskazini pamoja na jeshi kubwa, wote wakiendesha farasi, kusanyiko kubwa, jeshi kubwa.
Utakuja kutoka kwako huko kaskazini ya mbali, ukiwa pamoja na mataifa mengi, wote wakiwa wamepanda farasi, kundi kubwa, jeshi kuu.
16 Utawashambulia watu wangu Israeli kama wingu lifunikavyo nchi. Katika siku za baadaye nitakuleta juu ya nchi yangu, ili mataifa wanijue nitakapojifunua mwenyewe kupitia wewe, Gogu, kuwa mtakatifu mbele ya macho yao.
Utakuja dhidi ya watu wangu Israeli kama wingu lifunikavyo nchi. Siku zijazo, ee Gogu, nitakuleta wewe dhidi ya nchi yangu, ili kwamba mataifa wapate kunijua Mimi nitakapojionyesha mtakatifu kwa kukupitia wewe mbele ya macho yao.
17 Bwana Yahwe asema hivi: Je, wewe siye yule ambaye niliyeongea naye katika siku za zamani kwa mkono wa watumishi wangu, manabii wa Israeli, waliotabiri katika mda wao wenyewe kwa miaka niliyowaleta juu yao?
“‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Je, wewe si yule niliyenena juu yako katika siku za zamani kwa kupitia kwa watumishi wangu manabii wa Israeli? Wakati ule walitabiri kwa miaka mingi kwamba ningekuleta upigane nao.
18 Basi itakuwa katika siku hiyo wakati Gogu atakapo ishambulia nchi ya Israeli-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-ghadhabu yangu itapanda katika hasira yangu.
Hili ndilo litakalotokea katika siku ile: Gogu atakaposhambulia nchi ya Israeli, hasira yangu kali itaamka, asema Bwana Mwenyezi.
19 Katika wivu wangu katika hasira ya moto wangu, ninasema kwamba katika siku hiyo kutakuwa na tetemeko kubwa la nchi katika nchi ya Israeli.
Katika wivu wangu na ghadhabu yangu kali ninasema kuwa wakati ule patakuwepo tetemeko kuu katika nchi ya Israeli.
20 Watatetemeka mbele yangu-samaki wa baharini na ndege wa angani, wanyama wa mashambani, na viumbe watambaao juu ya nchi, na kila mtu aliyeko juu ya uso wa nchi. Milima itaangushwa chini majabali yataanguka, hadi kila ukuta utaanguka kwenye nchi.
Samaki wa baharini, ndege wa angani, wanyama wa kondeni, kila kiumbe kitambaacho ardhini, na watu wote walio juu ya uso wa nchi watatetemeka mbele zangu. Milima itapinduka, majabali yatapasuka na kila ukuta utaanguka chini.
21 Nitaita upanga dhidi yake juu ya milima yangu yote-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-upanga wa kila mtu utakuwa kinyume na ndugu yake.
Nitaita upanga vita dhidi ya Gogu juu ya milima yangu yote, asema Bwana Mwenyezi. Upanga wa kila mtu utakuwa dhidi ya ndugu yake.
22 Kisha nitamuhukumu kwa tauni na damu; nakufurika mvua na mvua ya mawe na kuchoma asidi nitainyeshea chini juu yake na jeshi lake na mataifa mengi yaliyo pamoja naye.
Nitatekeleza hukumu juu yake kwa tauni na kwa umwagaji wa damu. Nitaifanya mvua ya mafuriko kunyesha, mvua ya mawe na moto wa kiberiti juu yake na juu ya vikosi vyake na juu ya mataifa mengi walio pamoja naye.
23 Kwa kuwa nitaonyesha ukuu wangu na utakatifu wangu na nitafanya kujulikana mimi mwenyewe katiaka macho ya mataifa mengi, na watajua kwamba mimi ni Yahwe.”
Nami hivyo ndivyo nitakavyoonyesha ukuu wangu na utakatifu wangu, nami nitajijulisha mbele ya macho ya mataifa mengi. Ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.’

< Ezekieli 38 >