< Ezekieli 37 >

1 Mkono wa Yahwe ulikuwa juu yangu, na akanitoa kwa Roho wa Bwana Yahwe na kuniweka chini katikati ya bonde; lilikuwa limejaa mifupa.
耶和华的灵降在我身上。耶和华借他的灵带我出去,将我放在平原中;这平原遍满骸骨。
2 Kisha akanifanya kupita kati yao kuizunguka pande zote. Tazama! Mingi yao mikubwa ilikuwa katika bonde! Ilikuwa mikavu sana.
他使我从骸骨的四围经过,谁知在平原的骸骨甚多,而且极其枯干。
3 Akanambia, “Mwanadamu, Je! Hii mifupa inaweza kuishi kinyume?” Hivyo nikasema, “Bwana Yahwe, wajua wewe pekee.”
他对我说:“人子啊,这些骸骨能复活吗?”我说:“主耶和华啊,你是知道的。”
4 Kisha akanambia, “Tabiri juu ya hii mifupa na iambie, 'Mifupa mikavu. Lisikilizeni neno la Yahwe.
他又对我说:“你向这些骸骨发预言说:枯干的骸骨啊,要听耶和华的话。
5 Bwana Yahwe asema hivi kwenye hii mifupa: Tazama! nakaribia kuweka pumzi juu yenu, nanyi mtaishi.
主耶和华对这些骸骨如此说:‘我必使气息进入你们里面,你们就要活了。
6 Nitaweka mishipa juu yenu na kuleta nyama juu yenu. Nitawafunika kwa ngozi na kuweka pumzi ndani yenu hivyo mtaishi. Kisha mtajua kwamba mimi ni Yahwe.”'
我必给你们加上筋,使你们长肉,又将皮遮蔽你们,使气息进入你们里面,你们就要活了;你们便知道我是耶和华。’”
7 Hivyo nimetoa unabii kama nilivyokuwa nimeamriwa: nimetabiri, tazama, sauti ikaja, iliyokuwa ya mtetememo. Kisha mifupa ikasogeleana pamoja-mfupa juu ya mfupa.
于是,我遵命说预言。正说预言的时候,不料,有响声,有地震;骨与骨互相联络。
8 Nikatazama na, kumbe, mishipa ilikuwa juu sasa, na nyama ikatoka juu na ngozi ikazifunika. Lakini hapakuwa na pumzi juu yao.
我观看,见骸骨上有筋,也长了肉,又有皮遮蔽其上,只是还没有气息。
9 Kisha Yahwe akanambia, “Itabirie pumzi, tabiri, mwanadamu, na iambie pumzi, 'Bwana Yahwe asema hivi: Pumzi, hutoka pepo nne, na pumzi juu ya hawa walioawa, hivyo wanaweza kuishi.”'
主对我说:“人子啊,你要发预言,向风发预言,说主耶和华如此说:气息啊,要从四方而来,吹在这些被杀的人身上,使他们活了。”
10 Hivyo nimetabiri kama nilivyokuwa nimeamriwa; pumzi ikawajilia na wakaishi. Kisha wakasimama kwa miguu yao, jeshi moja kubwa sana.
于是我遵命说预言,气息就进入骸骨,骸骨便活了,并且站起来,成为极大的军队。
11 Kisha Yahwe akanambia, “Mwanadamu, mifupa hii yote ni ya nyumba ya Israeli. Tazama! Wanasema, 'Mifupa yetu imekauka, na tumaini letu limepotea. Tumekatwa.'
主对我说:“人子啊,这些骸骨就是以色列全家。他们说:‘我们的骨头枯干了,我们的指望失去了,我们灭绝净尽了。’
12 Kwa hiyo tabiri na waambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Nitayafunua makabiri yenu na kuwapandisha kutoka kwayo, watu wangu. Nitakurudisha hata katika nchi ya Israeli.
所以你要发预言对他们说,主耶和华如此说:‘我的民哪,我必开你们的坟墓,使你们从坟墓中出来,领你们进入以色列地。
13 Kisha mtajua kwamba mimi ni Yahwe, nitakapo yafunua makaburi yenu na kuwatoa kutoka kwao, watu wangu.
我的民哪,我开你们的坟墓,使你们从坟墓中出来,你们就知道我是耶和华。
14 Nitaweka Roho wangu ndani yenu hivyo mtaishi, na nitawafanya kupumzika katika nchi yenu mtakapojua yakwamba mimi ni Yahwe. Nasema na nitayafanya hayo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”'
我必将我的灵放在你们里面,你们就要活了。我将你们安置在本地,你们就知道我—耶和华如此说,也如此成就了。这是耶和华说的。’”
15 Kisha neno la Yahwe likanijia, likisema,
耶和华的话又临到我说:
16 “Sasa wewe, mwanadamu, chukua fimbo moja kwa ajili yako na andika juu yake, 'Kwa ajili Yuda na kwa ajili ya watu wa Israeli, wenzake,' Kisha fimbo nyingine andika juu yake, 'Kwa kuwa Yusufu, tawi la Efraimu, na kwa ajili ya watu wa Israeli, wenzake.
“人子啊,你要取一根木杖,在其上写‘为犹大和他的同伴以色列人’;又取一根木杖,在其上写‘为约瑟,就是为以法莲,又为他的同伴以色列全家’。
17 Walete wote pamoja kwenye fimbo moja, ili wawe kitu kimoja katika mkono wako.
你要使这两根木杖接连为一,在你手中成为一根。
18 Wakati watu wako watakapokwambia na kusema, 'Je! hutatuambia haya mambo yako yana maana gani?'
你本国的子民问你说:‘这是什么意思?你不指示我们吗?’
19 kisha waambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Nalichukua tawi la Yusufu ambalo lipo kwenye mkono wa Efraimu na kabila za Israeli wenzake na kuungana nalo hata kwenye tawi la Yuda, ili kwamba wawe tawi moja, na watakuwa kitu kimoja katika mikono yangu.'
你就对他们说:‘主耶和华如此说:我要将约瑟和他同伴以色列支派的杖,就是那在以法莲手中的,与犹大的杖一同接连为一,在我手中成为一根。’
20 Shika kwenye mkono wako na matawi uliyoandika mbele ya macho yao.
你所写的那两根杖要在他们眼前拿在手中,
21 Waambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! nakaribia kuwachukua watu wa Israeli kutoka miongoni mwa mataifa walipoenda. Nitawakusanya kutoka nchi zilizozunguka na nitawaleta kwenye nchi yao.
要对他们说,主耶和华如此说:我要将以色列人从他们所到的各国收取,又从四围聚集他们,引导他们归回本地。
22 Nitawafanya kuwa taifa moja katika nchi, juu ya milima ya Israeli, na kutakuwa na mfalme mmoja kama mfalme juu yao wote, na hawatakuwa mataifa mawili tena. Hawatagawanyika kwenye falme mbili tena.
我要使他们在那地,在以色列山上成为一国,有一王作他们众民的王。他们不再为二国,决不再分为二国;
23 Kisha hawatajitia unajisi tena kwa sanamu zao, mambo yao yachukizao, au dhambi zao nyingine. Kwa kuwa nitawaokoa kutoka matendo yao ya uongo ambayo wamefanya dhambi, na nitawatakasa, hivyo watakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wao.
也不再因偶像和可憎的物,并一切的罪过玷污自己。我却要救他们出离一切的住处,就是他们犯罪的地方;我要洁净他们,如此,他们要作我的子民,我要作他们的 神。
24 Daudi mtumishi wangu atakuwa mfalme juu yao. Hivyo kutakuwa na mchungaji mmoja juu yao wote, na wataishi kulingana na sheria zangu na watazitunza amri zangu na kuzitii.
“我的仆人大卫必作他们的王;众民必归一个牧人。他们必顺从我的典章,谨守遵行我的律例。
25 Wataishi katika nchi niliwapatia watumishi wangu Yakobo, ambapo baba zenu walipoishi. Wataishi humo milele-wao, watoto wao, na wajukuu zao, kwa Daudi mtumishi wangu atakuwa mkuu wao milele.
他们必住在我赐给我仆人雅各的地上,就是你们列祖所住之地。他们和他们的子孙,并子孙的子孙,都永远住在那里。我的仆人大卫必作他们的王,直到永远。
26 Nitaweka agano la amani pamoja nao. Litakuwa agano la milele pamoja nao. Nitawaweka na kuwazidisha na kupaweka mahali patakatifu pangu katikati yao milele.
并且我要与他们立平安的约,作为永约。我也要将他们安置在本地,使他们的人数增多,又在他们中间设立我的圣所,直到永远。
27 Maskani yangu yatakuwa pamoja nao; Nitakuwa Mungu wao, na watakuwa watu wangu.
我的居所必在他们中间;我要作他们的 神,他们要作我的子民。
28 Kisha mataifa watajua yakwamba mimi ni Yahwe niliyewatenga Israeli, wakati mahali pangu patakatifu patakapokuwa katikati yao milele.”
我的圣所在以色列人中间直到永远,外邦人就必知道我是叫以色列成为圣的耶和华。”

< Ezekieli 37 >