< Ezekieli 35 >
1 Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
καὶ ἐγένετο λόγος κυρίου πρός με λέγων
2 “Mwanadamu, weka uso wako juu ya Mlima Seiri na tabiri dhidi yake.
υἱὲ ἀνθρώπου ἐπίστρεψον τὸ πρόσωπόν σου ἐπ’ ὄρος Σηιρ καὶ προφήτευσον ἐπ’ αὐτὸ
3 Uiambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! ni juu yako, Mlima Seiri, nitakupiga kwa mkono wangu na kukufanya ukiwa na tishio.
καὶ εἰπόν τάδε λέγει κύριος κύριος ἰδοὺ ἐγὼ ἐπὶ σέ ὄρος Σηιρ καὶ ἐκτενῶ τὴν χεῖρά μου ἐπὶ σὲ καὶ δώσω σε ἔρημον καὶ ἐρημωθήσῃ
4 Nitaiharibu miji yenu, na wewe mwenyewe utakuwa ukiwa; kisha utajua kuwa mimi ni Yahwe.
καὶ ταῖς πόλεσίν σου ἐρημίαν ποιήσω καὶ σὺ ἔρημος ἔσῃ καὶ γνώσῃ ὅτι ἐγώ εἰμι κύριος
5 Kwa sababu umekuwa adui kwa watu wangu Israeli siku zote, na kwa sababu umewatoa kwenye mikono ya upanga wakati wa mateso yao, wakati adhabu yao itakapokuwa katika ukubwa wake.
ἀντὶ τοῦ γενέσθαι σε ἐχθρὰν αἰωνίαν καὶ ἐνεκάθισας τῷ οἴκῳ Ισραηλ δόλῳ ἐν χειρὶ ἐχθρῶν μαχαίρᾳ ἐν καιρῷ ἀδικίας ἐπ’ ἐσχάτῳ
6 Kwa hiyo, kama niishivyo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-nitaandaa kwa ajili ya damu, na damu na kukufutilia! Kwa kuwa hukuchukia damu, damu itakufuatilia.
διὰ τοῦτο ζῶ ἐγώ λέγει κύριος κύριος εἰ μὴν εἰς αἷμα ἥμαρτες καὶ αἷμά σε διώξεται
7 Nitaufanya Mlima Seiri mkamilifu na ukiwa wakati nitakapoukatilia mbali kutoka huo yeyote apitaye na arudiye tena.
καὶ δώσω τὸ ὄρος Σηιρ εἰς ἔρημον καὶ ἠρημωμένον καὶ ἀπολῶ ἀπ’ αὐτοῦ ἀνθρώπους καὶ κτήνη
8 Kisha nitaijaza milima kwa watu wao waliokufa. Milima yako na mabonde na mifereji-wale walioawa kwa upanga wataanguka kati yao.
καὶ ἐμπλήσω τῶν τραυματιῶν σου τοὺς βουνοὺς καὶ τὰς φάραγγάς σου καὶ ἐν πᾶσι τοῖς πεδίοις σου τετραυματισμένοι μαχαίρᾳ πεσοῦνται ἐν σοί
9 Nitakufanya mkiwa daima. Miji yako haitakaliwa na watu, lakini mtajua kwamba mimi ni Yahwe.
ἐρημίαν αἰώνιον θήσομαί σε καὶ αἱ πόλεις σου οὐ μὴ κατοικηθῶσιν ἔτι καὶ γνώσῃ ὅτι ἐγώ εἰμι κύριος
10 Umesema, “Haya mataifa mawili na hizi nchi mbili zitakuwa zangu, na tutazimiliki,” hata wakati Yahwe alipokuwa pamoja nao.
διὰ τὸ εἰπεῖν σε τὰ δύο ἔθνη καὶ αἱ δύο χῶραι ἐμαὶ ἔσονται καὶ κληρονομήσω αὐτάς καὶ κύριος ἐκεῖ ἐστιν
11 Kwa hiyo, kama niishivyo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-hivyo nitafanya kulingana na hasira yako na kulingana na wivu wako ambao uliousikia katika chuki yako ya Israeli, na nitajidhihirisha kwao nitakapokuhukumu.
διὰ τοῦτο ζῶ ἐγώ λέγει κύριος καὶ ποιήσω σοι κατὰ τὴν ἔχθραν σου καὶ γνωσθήσομαί σοι ἡνίκα ἂν κρίνω σε
12 Hivyo utajua kwamba mimi ni Yahwe. Nimeyasikia matukano yako yote uliyasema dhidi ya milima ya Israeli, uliposema, “Wameharibiwa; wametolewa kwetu tuwale.
καὶ γνώσῃ ὅτι ἐγώ εἰμι κύριος ἤκουσα τῆς φωνῆς τῶν βλασφημιῶν σου ὅτι εἶπας τὰ ὄρη Ισραηλ ἔρημα ἡμῖν δέδοται εἰς κατάβρωμα
13 “Nanyi mmejitukuza juu yangu kwa kile mlichokisema, na mmeongeza maneno juu yangu; na kuyasikia yote.
καὶ ἐμεγαλορημόνησας ἐπ’ ἐμὲ τῷ στόματί σου ἐγὼ ἤκουσα
14 Bwana Yahwe asema hivi: Nitakufanya ukiwa, wakati dunia nzima itakapofurahi.
τάδε λέγει κύριος ἐν τῇ εὐφροσύνῃ πάσης τῆς γῆς ἔρημον ποιήσω σε
15 Kama vile unavyofurahi juu ya urithi wa watu wa Israeli kwa sababu ukiwa ya wake, ndivyo nitakavyokutenda wewe. Utakuwa ukiwa, Mlima Seiri, na Edomu yote! Kisha watajua kwamba mimi ni Yahwe.”'
ἔρημον ἔσῃ ὄρος Σηιρ καὶ πᾶσα ἡ Ιδουμαία ἐξαναλωθήσεται καὶ γνώσῃ ὅτι ἐγώ εἰμι κύριος ὁ θεὸς αὐτῶν