< Ezekieli 33 >

1 Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
Neno la Bwana likanijia kusema:
2 “Mwanadamu, sema hivi kwa watu wako; waambie, 'Nitakapoleta upanga juu ya nchi, kisha watu wa hiyo nchi wakamchukua mtu mmoja kutoka mingoni mwao na kumfanya awe mlinzi wao.
“Mwanadamu, sema na watu wako uwaambie, ‘Nitakapoleta upanga dhidi ya nchi, nao watu wa nchi wakamchagua mmoja wa watu wao na kumfanya awe mlinzi wao,
3 Atazamapo kwa upanga kama unakuja juu ya nchi, na apige tarumbeta kuwaonya watu!
naye auonapo upanga unakuja dhidi ya nchi na kupiga tarumbeta kuonya watu,
4 Kama watu wakisikia sauti ya tarumbeta lakini bila kusikia, na kama upanga ukija na kuwaua, kisha damu ya kila mmoja iko juu ya kichwa chake mwenyewe.
kama mtu yeyote asikiapo sauti ya tarumbeta hakukubali kuonywa, basi upanga ujapo na kuutoa uhai wake, damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe.
5 Kama mtu akisikia sauti ya tarumbeta na hakusikiliza, damu yake iko juu yake; lakini kama akisikia, ataokoa maisha yake mwenyewe.
Kwa kuwa alisikia sauti ya tarumbeta lakini hakukubali maonyo, damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe. Kama angekubali maonyo, angelijiokoa mwenyewe.
6 Bali, kama mlinzi akiona upanga unakuja, lakini kama asipopiga tarumbeta, pamoja na matokeo kwamba watu hawajaonywa, na kama upanga ukija na kuchukua uhai wa mtu yeyote, kisha yule mtu akafa kwenye dhambi yake mwenyewe, lakini nitaitaka damu yake kutoka mlinzi.'
Lakini kama mlinzi akiona upanga unakuja na asipige tarumbeta kuonya watu na upanga ukija na kutoa uhai wa mmoja wao, yule mtu ataondolewa kwa sababu ya dhambi yake, lakini damu yake nitaitaka mkononi mwa mlinzi huyo.’
7 Sasa wewe mwenyewe, mwanadamu! Nimekufanya kuwa mlinzi kwa ajili ya nyumba ya Israeli; utasikia maneno kutoka kinywani mwangu na uwaonye badala yangu.
“Mwanadamu, nimekufanya wewe kuwa mlinzi kwa ajili ya nyumba ya Israeli, kwa hiyo sikia neno nisemalo na uwape maonyo kutoka kwangu.
8 Kama nikimwambia mtu mwovu, 'Mwovu, hakika utakufa!' lakini kama hutangazi hivi ili kwa ajili ya kumuonya mtu mwovu kuhusu hii njia, kisha huyo mtu mwovu atakufa katika dhambi yake, lakini nitaitaka damu yake kutoka kwenye mkono wako!
Nimwambiapo mtu mwovu, ‘Ewe mtu mwovu, hakika utakufa,’ nawe hukusema neno la kumwonya ili atoke katika njia zake, yule mtu mwovu atakufa kwa ajili ya dhambi yake, mimi nitaitaka damu yake mkononi mwako.
9 Lakini wewe, kama ukimwonya mwovu kuhusu hii njia, hivyo basi anaweza kurudi kutoka hiyo, na kama kama asipogeuka kutoka njia yake, kisha atakufa katika dhambi yake, lakini wewe mwenyewe utakuwa umeokoa maisha yako.
Lakini kama utamwonya huyo mtu mwovu aache njia zake mbaya naye hafanyi hivyo, atakufa kwa ajili ya dhambi yake, lakini utakuwa umejiokoa mwenyewe.
10 Basi wewe, mwanadamu, sema kwa nyumba ya Israeli, 'Mnasema hivi, Makosa yetu na dhambi zetu zi juu yetu, na tunadhoofika kwa ajili yao! Je! tutaishije?”'
“Mwanadamu, sema na nyumba ya Israeli uwaambie, ‘Hili ndilo mnalosema: “Makosa yetu na dhambi zetu zimetulemea, nasi tunadhoofika kwa sababu ya hayo. Tutawezaje basi kuishi?”’
11 Waambie, 'Kama niishivyo-asema Bwana Yahwe-sifurahii kifo cha mwovu, kwa kuwa kama mwovu akitubu kutoka njia yake, kisha ataishi! Tubu! Tubu kutoka njia zako mbaya! Kwa nini mnataka kufa, nyumba ya Israeli?'
Waambie, ‘Hakika kama mimi niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, sifurahii kifo cha watu waovu, bali kwamba wageuke kutoka njia zao mbaya wapate kuishi. Geukeni! Geukeni kutoka njia zenu mbaya! Kwa nini mkafe, ee nyumba ya Israeli?’
12 Hivyo basi wewe, mwanadamu, waambe watu wako, 'Haki ya mwenye haki haitamwokoa kama akikosa! Uovu wa mtu mwovu hautamfanya kuangamia kama akitubu dhambi zake! Kwa kuwa mtu mwenye haki hataweza kuishi kwa sababu ya haki yake kama akikosa.
“Kwa hiyo, mwanadamu, waambie watu wako, ‘Haki ya mtu mwenye haki haitamwokoa wakati anapoacha kutii, wala uovu wa mtu mwovu hautamsababisha yeye kuanguka anapotubu na kuacha uovu. Mtu mwenye haki, kama akitenda dhambi, hataishi kwa sababu ya uadilifu wake wa awali.’
13 Kama nikisema kwa mwenye haki, “Hakika ataisha!” na kama akiamini katika haki yake na kisha akafanya udhalimu, sitokumbuka haki yake yoyote. Atakufa kwa ajili ya uovu alioufanya.
Kama nikimwambia mtu mwenye haki kwamba hakika utaishi, lakini akategemea hiyo haki yake na kutenda uovu, hakuna tendo lolote la haki alilotenda litakalokumbukwa, atakufa kwa ajili ya uovu alioutenda.
14 Hivyo kama nikisema kwa mwovu, “Utakufa hakika,” lakini kama akitubu kutoka kwenye dhambi zake na kufanya yaliyo halali na haki-
Nami kama nikimwambia mtu mwovu, ‘Hakika utakufa,’ kisha akageuka kutoka dhambi yake na kufanya lile lililo haki na sawa,
15 kama akirudisha dhamana ambayo aliyomnyang'anya, au kama akirudisha alichokipoteza, na kama akitembea katika amri zitoazo uhai na bila kufanya dhambi-kisha ataishi hakika. Hatakufa.
kama akirudisha kile alichochukua rehani kwa ajili ya deni, akarudisha alichoiba na kufuata amri zile ziletazo uzima, wala hafanyi uovu, hakika ataishi, hatakufa.
16 Dhambi alizozifanya hazitakumbukwa kwa ajili yake. Ametenda halali na haki, na hivyo, ataishi hakika!
Hakuna dhambi yoyote aliyoitenda itakayokumbukwa juu yake. Ametenda lile lililo haki na sawa, hakika ataishi.
17 Lakini watu wako husema, “Njia ya Bwana haiko sawa!” lakini ni njia zako ndizo haziko sawa!
“Lakini watu wako wanasema, ‘Njia ya Bwana si sawa.’ Lakini ni njia zao ambazo si sawa.
18 Wakati mtu mwenye haki ageukapo kutoka kwenye haki na kufanya dhambi, kisha atakufa katika hiyo!
Kama mtu mwenye haki akigeuka kutoka uadilifu wake na kufanya uovu, atakufa kwa ajili ya huo uovu.
19 Wakati mtu mbaya ageukapo kutoka kwenye ubaya wake na kufanya iliyo halali na haki, ataishi kwa sababu ya hayo mambo!
Naye mtu mwovu kama akigeuka kutoka uovu wake na kufanya lile lililo haki na sawa, kwa kufanya hivyo ataishi.
20 Lakini ninyi watu husema, “Njia ya Bwana haiko sawa!” Nitawahukumu kila mmoja wenu kulingana na njia yake, nyumba ya Israeli!”'
Lakini, ee nyumba ya Israeli, unasema, ‘Njia ya Bwana si sawa.’ Lakini nitamhukumu kila mmoja wenu sawasawa na njia zake mwenyewe.”
21 Ikawa katika mwaka wa kumi na mbili, siku ya tano ya mwezi wa kumi ya uhamisho wetu, mtu mmoja akatoroka kutoka Yerusalemuna kusema, “Mji umetekwa!”
Mwaka wa kumi na mbili wa uhamisho wetu, mwezi wa kumi, siku ya tano, mtu aliyekuwa ametoroka kutoka Yerusalemu akanijia na kusema, “Mji wa Yerusalemu umeanguka!”
22 Mkono wa Yahwe ulikuwa juu yangu jioni kabla yule mtoro hajaja, na mdomo wangu ulikuwa wazi mda huo alikuja kwangu wakati wa mapambazuko. Hivyo mdomo wangu ulikuwa wazi; sikuwa bubu tena!
Basi jioni kabla mtu huyo hajaja, mkono wa Bwana, ulikuwa juu yangu, naye alifungua kinywa changu kabla ya mtu yule aliyenijia asubuhi hajafika. Basi kinywa changu kilifunguliwa na sikuweza tena kunyamaza.
23 Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
Ndipo neno la Bwana likanijia kusema:
24 “Mwanadamu, wale waishio mahali palipoharibika katika nchi ya Israeli huongea na kusema, 'Ibrahimu alikuwa mtu pekee, na alirithi nchi, lakini sisi tukowengi! Tumepewa nchi kama wamiliki.”
“Mwanadamu, watu wanaoishi katika magofu hayo katika nchi ya Israeli wanasema hivi, ‘Abrahamu alikuwa mtu mmoja tu, hata hivyo akaimiliki nchi. Lakini sisi ni wengi, hakika tumepewa nchi kuwa milki yetu.’
25 Kwa hiyo waambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Mnakula damu, na mmeziinulia macho yenu sanamu, kisha mnazimwagia damu za watu. Je! mna uhakika wa kuimiliki hii nchi?
Kwa hiyo waambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kwa kuwa mnakula nyama pamoja na damu na kuinulia sanamu zenu macho na kumwaga damu, je, mtaimiliki nchi?
26 Mnategemea upanga wenu na mmetenda mambo maovu; kila mtu amemnajisi mke wa jirani yake. Je! kweli mtaimiliki nchi?'
Mnategemea panga zenu, mnafanya mambo ya machukizo na kila mmoja wenu humtia unajisi mke wa jirani yake. Je, mtaimiliki nchi?’
27 Utawaambia hivi, 'Bwana Yahwe asema hivi: Kama niishivyo, hakika wale walio katika uharibifu wataanguka kwa upanga, na nitawapatia wale walio katika mashamba viumbe hai kama chakula, na wale walio katika ngome na mapango watakufa kwa tauni.
“Waambie hivi: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Hakika kama niishivyo, wale waliobaki katika magofu wataanguka kwa upanga, wale walio nje mashambani nitawatoa wararuliwe na wanyama pori, nao wale walio katika ngome na kwenye mapango watakufa kwa tauni.
28 Kisha nitairudisha nchi kwenye ukiwa na tishio, na kiburi cha uwezo wake kitakoma, kwa kuwa milima ya Israeli itakuwa jangwa, na hakutakuwa na mtu yeyote atakayewapitia.'
Nitaifanya nchi kuwa ukiwa na utupu na kiburi cha nguvu zake zitafikia mwisho, nayo milima ya Israeli itakuwa ukiwa ili mtu yeyote asipite huko.
29 Hivyo watajua kwamba mimi ni Yahwe, nitakapoifanya nchi ukiwa na tishio kwa sababu ya machukizo yote waliyoyafanya.
Kisha watajua kuwa Mimi ndimi Bwana, nitakapokuwa nimeifanya nchi kuwa ukiwa na utupu kwa sababu ya mambo yote ya machukizo waliyotenda.’
30 Hivyo basi wewe, mwanadamu-watu wako wanasema mambo yako karibu na kuta na malango ya nyumba, na kila mmoja anaambizana na mwenzake-kila mtu na ndugu yake, 'Twende na tukasikilize neno la nabii lililotoka kwa Yahwe!
“Kwa habari yako wewe, mwanadamu, watu wako wanaongea habari zako wakiwa karibu na kuta na kwenye milango ya nyumba, wakiambiana kila mmoja na mwenzake, ‘Njooni msikie ujumbe ule utokao kwa Bwana.’
31 Hivyo watu wangu watakuja kwako, kama wafanyavyo mara nyingi, na nitaketi mbele yako na kusikiliza maneno yako, lakini mioyo yao inafuata udhalimu kwa faida yao.
Watu wangu wanakujia, kama wafanyavyo, nao wanaketi mbele yako kama watu wangu na kusikiliza maneno yako, lakini hawayatendi. Kwa maana udanganyifu u katika midomo yao, lakini mioyo yao ina tamaa ya faida isiyo halali.
32 Kwa kuwa umekuwa kama wimbo mzuri kwao, sauti nzuri awezaye kucheza kinanda vizuri, hivyo watasikia maneno yako, lakini hakuna atakaye yatii.
Naam, mbele yao umekuwa tu kama yeye aimbaye nyimbo za mapenzi kwa sauti nzuri za kuvutia na kupiga vyombo kwa ustadi, kwa kuwa wanasikia maneno yako lakini hawayatendi.
33 Hivyo wakati haya yote yatakapotokea-tazama! itatokea! -watajua yakwamba nabii alikuwa miongoni mwao.”
“Wakati mambo haya yote yatakapotimia, kwa kuwa hakika yatatokea, ndipo watakapojua kwamba nabii amekuwepo miongoni mwao.”

< Ezekieli 33 >