< Ezekieli 32 >

1 Kisha ikawa katika mwezi wa kumi na mbili wa mwaka wa kumi na mbili, siku ya kwanza ya mwezi, lile neno la Yahwe likanijia, kusema,
ויהי בשתי עשרה שנה בשני עשר חדש באחד לחדש היה דבר יהוה אלי לאמר
2 “Mwanadamu, inua maombolezo kuhusu Farao mfalme wa Misri; mwambie, 'Wewe ni kama simba mdogo juu ya mataifa, lakini kama jitu la kutisha, unatoka kwenye maji, unayachafua maji kwa miguu yako na kuyachafua maji yao.
בן אדם שא קינה על פרעה מלך מצרים ואמרת אליו כפיר גוים נדמית ואתה כתנים בימים ותגח בנהרותיך ותדלח מים ברגליך ותרפס נהרותם
3 Bwana Yahwe asema hivi: Basi nitautandaza wavu wangu juu yako katika kusanyiko la watu wengi, na watawainua juu katika wavu wangu.
כה אמר אדני יהוה ופרשתי עליך את רשתי בקהל עמים רבים והעלוך בחרמי
4 Nitakuacha katika nchi. Nitakutupa kwenye shamba na kufanya ndege wote wa angani watue juu yako; njaa ya wanyama wote waishio juu ya nchi watashibishwa na wewe.
ונטשתיך בארץ על פני השדה אטילך והשכנתי עליך כל עוף השמים והשבעתי ממך חית כל הארץ
5 Kwa kuwa nitaiweka nyama yako juu ya milima, na nitayajaza mabonde kwa funza wako waliokufa.
ונתתי את בשרך על ההרים ומלאתי הגאיות רמותך
6 Kisha nitamwaga damu yako juu ya milima, na vitanda vya kijito vitajazwa kwa damu yako.
והשקיתי ארץ צפתך מדמך אל ההרים ואפקים ימלאון ממך
7 Kisha wakati nitakapokuzimisha, nitazifunika mbingu na kuzitia giza nyota zake; nitalifunika jua kwa mawingu, na mwezi hautatoa nuru yake usiku.
וכסיתי בכבותך שמים והקדרתי את ככביהם שמש בענן אכסנו וירח לא יאיר אורו
8 Mianga ya mbinguni nitaiweka giza juu yako, na nitaweka giza juu ya nchi-hivi ndivyo asemavyo Bwana Yahwe.
כל מאורי אור בשמים אקדירם עליך ונתתי חשך על ארצך נאם אדני יהוה
9 Hivyo nitaitisha mioyo ya watu wengi katika nchi ambao huwajui, wakati nitakapoleta kuhusu uvunjifu miongoni mwa mataifa, miongoni mwa nchi ambazo hukuzijua.
והכעסתי--לב עמים רבים בהביאי שברך בגוים על ארצות אשר לא ידעתם
10 Nitawashangaza watu wengi kuhusiana na wewe; wafalme wao watatetemeka kwa hofu kuhusiana na wewe nitakapoutikisa upanga wangu mbele yao. Kila wakati kila mmoja atatetemeka kwa sababu yako, katika siku ya kuanguka kwako.
והשמותי עליך עמים רבים ומלכיהם ישערו עליך שער בעופפי חרבי על פניהם וחרדו לרגעים איש לנפשו ביום מפלתך
11 Kwa kuwa Bwana Yahwe asema hivi: Upanga wa mfalme wa Babeli utakuja juu yako.
כי כה אמר אדני יהוה חרב מלך בבל תבואך
12 Nitawafanya watu wako kuanguka kwa panga za mashujaa-kila shujaa ni tishio la mataifa. Hawa mashujaa watateketeza kiburi cha Misri na kuangamiza watu wake wote.
בחרבות גבורים אפיל המונך עריצי גוים כלם ושדדו את גאון מצרים ונשמד כל המונה
13 Kwa kuwa nitaiharibu mifugo yote kutoka karibu na maji mengi; na mguu wa mtu hautayatibua tena, wala kwato za wanyama hazitayatibua.
והאבדתי את כל בהמתה מעל מים רבים ולא תדלחם רגל אדם עוד ופרסות בהמה לא תדלחם
14 Kisha nitayafanya maji yao kuwa matulivu na kufanya mito yao kukimbia kama mafuta-hivi ndivyo asemavyo Bwana Yahwe.
אז אשקיע מימיהם ונהרותם כשמן אוליך--נאם אדני יהוה
15 Wakati nitakapoifanya nchi ya Misri sehemu iliyojitenga, wakati nchi iliyopungukiwa na vitu viijazavyo, wakati nitakapo washambulia wakaao ndani yake, watajua yakwamba mimi ni Yahwe.
בתתי את ארץ מצרים שממה ונשמה ארץ ממלאה--בהכותי את כל יושבי בה וידעו כי אני יהוה
16 Kutakuwa na maombolezo; binti za mataifa wataomboleza juu yake; wataomboleza juu ya Misri, juu ya watu wake wote wataomboleza-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”'
קינה היא וקוננוה בנות הגוים תקוננה אותה על מצרים ועל כל המונה תקוננה אותה נאם אדני יהוה
17 Kisha ikawa katika mwaka wa kumi na mbili, siku ya kumi na tano ya mwezi, lile neno la Yahwe likanijia, kusema,
ויהי בשתי עשרה שנה בחמשה עשר לחדש היה דבר יהוה אלי לאמר
18 “Mwanadamu, omboleza kwa ajili watu wa misri na walete chini-yeye na binti za mataifa mashuhuri-hata chini ya dunia pamoja na wale walioshuka chini kwenye shimo.
בן אדם--נהה על המון מצרים והורדהו אותה ובנות גוים אדרם אל ארץ תחתיות--את יורדי בור
19 'Je! wewe ni mzuri zaidi kuliko mtu mwingine yeyote? Nenda chini na lala chini pamoja na wasiotahiriwa.'
ממי נעמת רדה והשכבה את ערלים
20 Wataanguka miongoni mwao waliokuwa wameuawa kwa upanga. Upanga ulikuwa umewekwa! Alikuwa amepatiwa upanga; watamkamata na watu wake.
בתוך חללי חרב יפלו חרב נתנה משכו אותה וכל המוניה
21 Hodari wa wapiganaji katika Sheoli atasema kuhusu Misri na rafiki zake, 'Wameshuka chini hapa! Watalala pamoja na wasiotahiriwa, pamoja na wale waliokuwa wameuawa kwa upanga.' (Sheol h7585)
ידברו לו אלי גבורים מתוך שאול--את עזריו ירדו שכבו הערלים חללי חרב (Sheol h7585)
22 Ashuru yupo huko pamoja na kusanyiko lake. Makaburi yake yamemzunguka; wote waliuawa kwa upanga.
שם אשור וכל קהלה סביבותיו קברתיו כלם חללים הנפלים בחרב
23 Wale ambao makaburi yao yamewekwa katika maficho ya mashimo yaliyo huko, pamoja na kusanyiko lake. Makaburi yake yakiwazunguka wote waliokuwa wameuawa, walioanguka kwa upanga, wale walioleta hofu juu ya nchi ya walio hai.
אשר נתנו קברתיה בירכתי בור ויהי קהלה סביבות קברתה כלם חללים נפלים בחרב אשר נתנו חתית בארץ חיים
24 Elamu yupo huko pamoja na watu wake wote. Makaburi yake yamemzunguka; wote walikuwa wameuawa. Wale walioawa kwa upanga, walioshuka chini wasiotahiriwa hata sehemu ya chini kabisa ya dunia, waliowatia hofu juu ya nchi ya walio hai na wale waliobeba aibu yao wenyewe, pamoja na wale washukao chini kwenye shimo.
שם עילם וכל המונה סביבות קברתה כלם חללים הנפלים בחרב אשר ירדו ערלים אל ארץ תחתיות אשר נתנו חתיתם בארץ חיים וישאו כלמתם את יורדי בור
25 Wamemuwekea kitanda kwa ajili ya Elamu na watu wake wote kati ya wachinjaji; kaburi lake limemzunguka. Wote hawajatahiriwa, kukatwa vipande kwa upanga, kwa sababu waliwaleta mashujaa wao juu ya nchi ya walio hai. Hivyo wamechukua aibu yao wenyewe, pamoja na wale washukao kwenye shimo miongoni mwa wote waliouawa, wale washukao kwenda shimoni. Elamu yu miongoni mwa wale waliokuwa wameuawa.
בתוך חללים נתנו משכב לה בכל המונה--סביבותיו קברתה כלם ערלים חללי חרב כי נתן חתיתם בארץ חיים וישאו כלמתם את יורדי בור בתוך חללים נתן
26 Mesheki, Tubali, na watu wake wote wako huko! Makaburi yao yamewazunguka. Wote hawajatahiriwa, wameuawa kwa upanga, kwa sababu walileta utiisho wao juu ya nchi ya walio hai.
שם משך תבל וכל המונה סביבותיו קברותיה כלם ערלים מחללי חרב כי נתנו חתיתם בארץ חיים
27 Wasilale pamoja mashujaa walioanguka wa wasiotahiriwa walioshuka chini kwa Sheoli pamoja na silaha zao zote za vita, na pamoja na panga zao zote walizoziweka chini ya vichwa vyao na maovu yao juu ya mifupa yao. Kwa kuwa walikuwa tishio kwa mashujaa katika nchi ya walio hai. (Sheol h7585)
ולא ישכבו את גבורים נפלים מערלים אשר ירדו שאול בכלי מלחמתם ויתנו את חרבותם תחת ראשיהם ותהי עונתם על עצמותם--כי חתית גבורים בארץ חיים (Sheol h7585)
28 Basi wewe, Misri, utavunjika kati yao wasiotahiriwa! Utalala karibu nao waliokuwa wamekatwa vipande vipande kwa upanga.
ואתה בתוך ערלים תשבר ותשכב--את חללי חרב
29 Edomu yuko huko na wafalme na viongozi wake wote. Walikuwa wamehifadhiwa katika uwezo wao pamoja na wale walioawa kwa upanga. Pamoja na wasiotahiriwa wamelala, pamoja na wale walioshuka kwenye shimo.
שמה אדום מלכיה וכל נשיאיה אשר נתנו בגבורתם את חללי חרב המה את ערלים ישכבו ואת ירדי בור
30 Wakuu wa kaskazini wako huko-wote na Wasidoni wote walioshuka chini pamoja na hao waliokuwa wamekatwa vipande vipande. Walikuwa na nguvu na kuwafanya wengine kuogopa, lakini sasa wako huko kwa aibu, wasiotahiriwa pamoja na wale waliokatwa vipande vipande kwa upanga. Wamebeba aibu yao wenyewe, pamoja nao waendao kwenye shimo.
שמה נסיכי צפון כלם וכל צדני אשר ירדו את חללים בחתיתם מגבורתם בושים וישכבו ערלים את חללי חרב וישאו כלמתם את יורדי בור
31 Farao ataona na kupata faraja kuhusu kundi lake waliokatwa vipande vipande kwa upanga -Farao na jeshi lake lote-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
אותם יראה פרעה ונחם על כל המונה--חללי חרב פרעה וכל חילו נאם אדני יהוה
32 Natamuweka kama utiisho wangu katika nchi ya walio hai, lakini atakuwa amelazwa chini katikati yao wasiotahiriwa, miongoni mwa wale walio katwa vipande kwa upanga, Farao na makundi yake yote-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
כי נתתי את חתיתו (חתיתי) בארץ חיים והשכב בתוך ערלים את חללי חרב פרעה וכל המונה--נאם אדני יהוה

< Ezekieli 32 >